latest Post

AINA TANO ZA MAZOEZI YA KUKUZA KIFUA BILA VIFAA VYA UZITO


Watu wengi wamekua wakiniuliza ni namna gani mtu anaweza kujenga misuli ya kifua bila ya kubeba vitu vizito, basi leo ntagusia swala hilo na natumae litawasaidia. Kifua kimejengwa na misuli iitwayo pectoralis major  ambayo ipo karibu na torso(munganiko wa mabega na mikono). Kikubwa kinachohitajika ni kufanyisha mazoezi yakutanua misuli hyo eidha kwa kutumia vifaa vizito ama mazoezi ya kutumia mwili pekee. Sasa basi leo tutaongelea njia ya kukuza misuli hiyo ya kifua kwa kutumia mwili pekee, na njia hizo ni;  •  Pushups za kawaida

Push ups za kawaida uhitaji mtu kusukuma mwili kutoka chini na kuiweka nyuzi tisini(90*), ambapo itakuhitaji ufanye marudio kulingana na idadi utakayo pendelea kufanya. Hili zoezi husaidia kukaza misuli ya kifua na pia kutengeneza muonekano mzuri wa kifua.


  •  pushups za inklin 

Hii ni aina ya pushup inayo muhitaji mtu aweke mikono pahali pajuu palipo inuka kidogo kutoka chini(kama mita moja) nakuweka mikono nyuzi tisini(90*) kutoka pahali ulipoweka viganya vya mikono. Zoezi hili lina kulazimisha kujinyanyua juu na chini, kwa mizunguko kadha(set) kwa idadi(count) unazozitaka...Hili zoezi hugusa kwenye wsala kubwa lakukaza misuli ya mikono(bicep na tricep) na pia kutengeneza kifua cha chini.


  • Pushups za muinuko
Hii ni aina ya pushup inayo muhitaji mtu aweke mikono pahali palipo shuka kutoka sehemu ulipo weka miguu. Hapo inampasa mtu aweke mikono chini ikiwa imekaa usawa wamabega na nyuzi tisini(90*) kutoka chini Zoezi hili lina kulazimisha kujinyanyua juu na chini, kwa mizunguko kadha(set) kwa idadi(count) unazozitaka.Hili zoezi hugusa kwenye wsala kubwa lakukaza misuli ya mikono na pia kutengeneza kifua cha juu  • Zoezi la kujivuta juu
Hili zoezi humuhitaji mtu kujishikilia pahali pa juu palipo inuka ambapo miguu haigusi chini kirahisi, na kujishkiza mikoni kwenye sehemu kama vile(chuma). umuhimu wa zoezi hili ni kwamba husaidia kuvuta kifua cha juu( chini ya kidevu) na hivyo kuweka muonekano mzuri wa kifua.


  • Zoezi la kujididimiza
Zoezi hili lina muhitaji mtu adidimize mwili(katikati) kwanzia kiuno mpaka miguu chini huku akijishkiza mikono yake pande mbili( kulia na kushoto) kwenye vyuma viwili tofauti. Zoezi hili husaidia kukaza misuli chini ya torso itwayo litissimal dorsi ambayo huchangia zaidi kwenye muonekano wa kifua.
Mazoezi hayo yote huwezekana kufanyika sehemu yoyote pale kwa sababu haitaji uzito wowote ule na pia haikulazimu kuingia GYM ili ufanikishe hilo.
Kwa maoni ama ushauri tafadhali tuandikia chini baada ya andiko hili, na kama umeipenda pia weza kutuandikia.

About benson godfrey

benson godfrey
Recommended Posts × +

DIET YA KUTOA SUMU MWILINI NA KUPUNGUZA UNENE KWA HARAKA

Habari zenu wadau wa KUAFIT! leo tutaongelea kuhusiana na elimu ya lishe ambayo itahusiana na diet ambapo tutaelezea mambo mengi san...