latest Post

JE! NI MARA NGAPI UNAPASWA KUFANYA MAZOEZI YA KUNYANYUA VYUMA NDANI YA WIKI?


 Hili ni swali tunaloulizwa mara kwa mara na watu wengi wanaoenda gym wakitaka kuongeza ukubwa wa misuli ya miili yao kwa kunyanyua vyuma vizito. Kutokana na pilika na majukumu ya kimaisha mda umekuwa ni kitu hadimu kupata hasa pale mtu anapotaka kufanya mazoezi na pia kuzingatia kwenda gym. Ni kweli kwamba mtu napo pata mda wa kwenda gym huwa analengo la kuona matokeo mazuri, na pia wengi huanza mazoezi bila kupata muongozo wa jinsi ya kufanya mazoezi. Tatizo hili la kuto kupata muongozo huweza kusababisha mtu kukata tamaa hasa pale anaposhindwa kupata matokeo aliyoyatazamia kuyapata.

  Mazoezi ya kunyanyua vyuma vizito ni moja wapo kati ya mazoezi iitwayo spot resistance training yanayolenga kugusa kundi la misuli ya aina moja kwa kila zoezi moja. Utafiti unaonyesha yakwamba kwa mtu anae enda gym na kufanya mazoezi ya kunyanyua uzito kwa angalau mara 2 ama 3 na dakika zisizo pungua 40 ndani ya wiki, basi mtu huyo anauwezo mkubwa wa kuongeza nguvu na ukubwa wa misuli yake kwa kiwango cha kuridhisha. Hivyo kulingana na utafiti huo ni sawa kusema kwamba ili mtu kupata matokeo mazuri, basi mtu huyo atapaswa kufanya mazoezi ya kunyanyua vyuma vizito angalau mara 3 mpaka 4 kwa wiki.


  • Mambo muhimu ya kuzingatia wakati wa kufanya mazoezi ya vyuma vizito
Kunyanyua vyuma vizito kunahitaji elimu ilikuweza kumsaidia mtu kupata matokeo anayoyatazamia na hata pia kupunguza uwezekano wa majeraha. yafwatayo ni mambo ya msingi kuzingatia.
1. Usirudie kufanya mazoezi ya ania moja siku 2 mfululizo

  Nianze kwa kusema kwamba kufanya mazoezi ya vyuma ya aina moja haina tatizo bali huweza kusababisha majera ya ndani kwa ndani. Kwa mfano; kwa kufanya mazoezi ya kunyanyua vyuma ilikujenga misuli ya mbele ya mkono(biceps) kwa siku 2 ama 3 mfululizo kunaweza sababisha maumivu makali kwenye viwiko.
 Hivyo inashauriwa mtu kufanya mabadiliko kwa kubadilisha mazoezi na kwa kulenga kundi la misuli tofauti kila siku.
 kwa mfano: siku 1 fanya mazoezi ya mikono na squat
                     siku 2 fanya mazoezi ya kifua na mgongo
Kwa kufanya hivyo kunahakikisha kuwa misuli itapata mda mzuri wa kupumzika na pia kutanuka.

2. Ongeza kiwango cha mazoezi kila baada ya wiki 2

  Utafti unaonyesha yakwamba mtu atakapo ongeza kiwango cha ufanyaji mazoezi eidha kwa kuongeza idadi(sets) ama marudio(reps) ya mazoezi kunaweza kuleta tija hasa pale mazoezi ya vyuma yanapo husika.
Kwa kuongeza idadi ya ufanyaji wa mazoezi kunaweza kuongeza ukubwa wa misuli, na pia kwa kufanya hivyo kunaongeza nguvu na uwezo wa kunyanyua uzito mkubwa zaidi ya awali.

3. Punguza uzito wa vyuma na kiwango cha mazoezi angalau mara 2 kila baada ya wiki 4


   Najua utakuwa unajiuliza, "kupunguza!!" ndio nipo sahihi. Misuli kwa ualisia wake huwa na tabia ya kutanuka na kunyauka, na hivyo ili mtu aweze kupata matokeo mazuri anapaswa kupumzisha misuli yake pale atakapo kuwa akifanya mazoezi makali kwa wiki 3 mfululizo. kwa kufanya hivyo kunaipa misuli mda wa kujirudi na kupumzika ili iweze kutanuka zaidi.

Kumbuka ni muhimu kuzingatia yaliyoainishwa awali, na pia kwa kutumia dakika 40 na zaidi kwa kila siku ya mazoezi bila kusahau mlo sahihi wa protein ili kujenga misuli na wanga ili kukupa nguvu kutakuhakikishia matokeo mazuri zaidi.

Kama umelipenda andiko hili basi gonga NZURI  na  kwa maswali au maoni zaidi basi tuandikie baada ya andiko hili, na pia kama ungependa kusoma andiko jengine kama hili basi jisajili kwa kuweka anuani yako  kwenye linki ya SUBSCRIBE.


Pia waweza tuandikia kwa email yetu Kuafit08@gmail.com 


Kwa number yetu ya Tigo +255 653 009 477  


Instagram account yetu  (KUAFITI), Facebook-(kuafit) na twitter-(kuafit

About benson godfrey

benson godfrey
Recommended Posts × +

DIET YA KUTOA SUMU MWILINI NA KUPUNGUZA UNENE KWA HARAKA

Habari zenu wadau wa KUAFIT! leo tutaongelea kuhusiana na elimu ya lishe ambayo itahusiana na diet ambapo tutaelezea mambo mengi san...