latest Post

AINA 6 ZA TIBA MBADALA ILI KUPUNGUZA MAUMIVU YA MAGOTI NA MABEGA


  Maumivu ya magoti na mabega ni hali ya kawaida na inayowakabili watu wengi ambapo hujitokeza kutokana na sababu nyingi ambazo huasbabisha msuguano na michubuko kwa maungo yanayounga magoti na mabega. Kati ya sababu kuu za kusababisha michubuko katika maungo ya magoti na mabega ni maumivu yatokanayo na mazoezi, uzee, kufahama kwa maungo ya magoti na mabega(dislocation)

Maumivu ya magoti na mabega yanaweza kuwaadhiri watu warika zote kwaanzia watoto hadi watu wazima, na kulingana  utafiti inasemekana kwamba wanawake wana uwezekano mkubwa wa kusumbuliwa zaidi kutokana na matumizi makubwa ya calcium kwenye kipindi cha uzazi.

Kati ya dalili za kujua kwamba mtu anatatizo la magoti na mabega ni kushindwa kutembea vizuri kwa kukwepa maumivi kwenye magoti, uvimbe kwenye magoti na mabega na pia kushindwa kubeba kitu kizito kwa kuhofia maumivu kwenye bega.

Watu wengi huteseka kutokana na maumivu ya viungo hasa ya magoti na mabega, bali kutokana na uwepo wa tiba asilia na mbadala basi kutibu maumivu hayo imekuwa ni swala la raisi. Tiba hizi asilia na mbadala huweza kupatikana kirahisi majumbani na hivyo kusemekana ni tiba iliyo nafuu.

Basi tutagusia aina sita za tiba mbadala anayoweza kuitumia mtu kutibu matatizo ya magoti na mabega.

1. Pilipili kichaa

 Pilipili hii ni kati ya pilipili zinazopatikana na kujulikana na wengi, na kutokana na pilipili hii kuwa na kemikali itwayo caspsaicin basi pilipili hii inasemekana kuwa kati ya tiba mbadala iliyo bora. Kemikali ya caspsaicn huleta hali ya joto kwenye maungo ya magoti na hata mabega na hivyo kusababisha maumivu kupungua.
Jinsi ya kuandaa pilipili kwa ajili ya matumizi

 • Tengeneza mchanganyiko wa vijiko viwili vya chai ya pilipili kichaa iliyokuwa kwnye mfumo wa unga na kisha weka kwenye nusu kikombe cha mafuta ya olive yaliyo na joto la wastani na kisha koroga. paka mchanganyiko huo kwenye sehemu unayosikia maumivu angalu mara mbili kwa siku kwa mda wa wiki moja na zaidi.

2. Manjano

 Manjanio ni kati mitishamba ambayo hutumiwa na watu wengi kwa maswala mablimbali kama vile urembo, bali kutokana na manjano kuwa na kemikali itwayo turmeric basi manjano imesemekana kuwa kati ya tiba mbadala bora ya kutibu maumivu ya magoti na mabega.
Jinsi ya kuandaa manjano kwa ajili ya matumizi

 • Chemsha kijiko kimoja cha manjano kwenye kikombe kimoja cha maziwa na weka kijiko kidogo cha asali na kisha kunywa kila siku

  Aangalizo: manjano huwa na tabia ya kufanya damu kuwa nyepesi endapo itatumika mara nyingi zaidi ya kawaida hivyo mtu anapaswa kutumia tiba hii kwa uwangalifu ingawa ni kati ya tiba bora.

3. Barafu

  Maji ya baridi ama barafu ni kati ya tiba mbadala bora ambayo husaidia kupunguza kuvimba kwa magoti ama mabega yaliyo na majeraa kwa kubana mishipa ya damu iliyotanuka. Kwa kubana mishipa  hiyo ya damu iliyotanuka kutokana na majeraa basi maumivu ni rahisi sana kuisha mpaka pale mtu atakapo weza kupata matibabu mengine kutoka hosipitali.
Jinsi ya kuandaa tibaa hii
 • Weka barafu ndani ya taulo na kisha funga, na chukua taulo lako na uweke kwenye sehemu inayo uma.
 • fanya zoezi hili angalau kwa siku 5.
4. Limao

  Limao ni kati ya tiba bora ambayo husaidia kuondoa maumivu hasa kwa watu wazima wenye kusumbuliwa na ugonjwa wa maumivu ya viungo vya mwili (arthritis). Kutokana na kemikali iliyopo kwenye malimao itwayo citric basi limao inasemekana kuwa ndio tiba mbadala iliyo bora kwa kutibu shida ya maumivu ya viungo vya mwili.
Jinsi ya kuandaa tiba hii ya limao
 • Kata malimao mawilli hadi kuwa vipisi vidogo na vifunge vipisi hivyo kwenye kipipande cha nguo ya kotoni na kisha chovya kwenye mafuta ya ufuta.
 • Weka kipande hicho cha nguo yenye liamao kwenye sehemu unayoskia maumivu angalau mara mbili kwa siku kwa kipindi cha wili moja na zaidi.
5. Tangawizi

 Tangawizi ni kati ya mitishamba inayofahamika kwa mambo mengi na hasa hutumiwa na wtu wengi kwenye maswala ya vyakula kama kiungo na pia kama tiba ya kifua na kichefuchefu. Ingawa tangawizi inafahamika na watu kwa machache hayo ila pia tangawizi yaweza pia kutumika kutibu maumivu ya viungo vya mwili kama vile magoti na mabega.
Jinsi ya kuandaa tiba ya tangawizi 
 • Saga kipisi cha tangawizi na weka kwenye kikombe kimoja cha maji na kisha chemsha kwa dakika 15.
 • weka kijiko kidogo cha asali na kisha minyia maji ya malimao kidogo.
 • kunywa mchanganyiko huo angalau mara mbili kwa siku kwa mda wa wiki mbili.
 6. Mafuta ya haradali

 Kutokana na uwezo wake wa kuongeza na kuboresha  mzunguko wa damu kwenye sehemu yenye maumivu basi mafuta ya haradali yenye kujulikana kwa uzito wake husemkana ni kati ya mafuta bora ya kusaidia kupunguza maumivu.
Jinsi ya kuandaa mafuta haya kwaajili ya tiba
 • Weka vijiko viwili vya karafuu kwenye chombo(sufuria) pamoja na kitungu saumu na karafuu na kisha kaanga mpaka vitungu viwe yangi ya kaawia.
 • Chuja mafuta hayo na kisha yaache ya poe na kisha chua sehemu yenye maumivu na mafuta hayo.
 • fanya zoezi hili mara mbili kwa siku  kwa angalu wiki tatu.
Kumbuka kama unaona tatizo lako linaongezeka tafadhali muone daktari ili uweze kupata ushauri, vipimo na tiba zaidi

Kama umeipenda andiko hili basi gonga NZURI  na  kwa maswali au maoni zaidi basi tuandikie baada ya andiko hili, na pia kama ungependa kusoma andiko jengine kama hili basi jisajili kwa kuweka anuani yako  kwenye linki ya SUBSCRIBE.


Pia waweza tuandikia kwa email yetu Kuafit08@gmail.com 


Kwa number yetu ya Tigo +255 653 009 477  


Instagram account yetu  (KUAFITI), Facebook-(kuafit) na twitter-(kuafit

About benson godfrey

benson godfrey
Recommended Posts × +

DIET YA KUTOA SUMU MWILINI NA KUPUNGUZA UNENE KWA HARAKA

Habari zenu wadau wa KUAFIT! leo tutaongelea kuhusiana na elimu ya lishe ambayo itahusiana na diet ambapo tutaelezea mambo mengi san...