latest Post

FAIDA YA MAZOEZI YA CARDIO

          Kwanza ni vyema kujua nini maana ya neno "Cardio" kabla ya kitu chochote; cardio ni neno la kingereza linalo ashiria usambazaji wa damu yenye oxygen unaoambatanishwa na mapigo ya moyo kwenda kwenye maeneo mbalimbali katika mwili. Usambazaji huo wa damu hulenga misuli inayofanya kazi kwa nia ya kuisambazia oxygen inayo safirishwa sambamba na damu kupitia mirija ya damu iliyo ungana na moyo.
         Mazoezi ya Cardio uhusiana na mazoezi yale yote yanayo mfanya mtu kuongezeka mapigo ya moyo na uvutaji pumzi kwa kiasi kikubwa ili kuweza kuongeza hewa ya oxygen mwilini. Mazoezi haya ya Cardio yapo ya aina nyingi  na mfano wake ni kama vile "urukaji wa kamba,burpeejumping jacks, mazoezi ya aerobics na kadhalika".
 Mazoezi ya cardio yana umuhimu mkwubwa sana kwa mtu anayetaka na kwa anayefanya mazoezi, na baadhi ya muhimu hizo ni


  •   Hupunguza mafuta ya mwili na vitambi
Kulingana na utafiti kwa kupitia vipimo vya tape measure ni kwamba tumbo la mwanaume likizidi  (140cm) na pia la mwanamke likizidi (35cm)  basi mtu huyo anasadikika kuwa na kitambi na hivyo anapaswa kukipunguza mafuta ya kwenye tumbo na mwili kiujumla.
Mazoezi ya Cardio husaidia sana kuondoa mafuta ya mwili yasiyo hitajika, kwa kusaidia misuli ya mwili kupokea hewa ya oxygen kwa wingi hvyo kuchoma mafuta hayo.

  • Huongeza ufanisi wa kimetabolic
Metabolic ni neno lakitaalamu la kigiriki linalo ashiria jinsi mwili unavyoweza kume'ngenya chakula na kufyonza chakula hicho kikemikali ili kuweze kutengeneza nguvu , na hivyo mwili kuweza kufanya kazi zake za kila siku. Hivyo kwa kufanya mazoezi ya Cardio mwili hulazimika kutumia jitihada zaidi ya kawaida ili nguvu inayohitajika mwilini kuweza kupatikana, na hivyo huongeza hamu ya mtu kula zaidi ya kwaida.


  • Huongeza ufanisi na kuimarisha mapigo ya moyo 
Ni dhairi ya kwamba kwa kufanya mazoezi ya Cardio hulazimu moyo kutumia nguvu kubwa kusambaza damu yenye hewa ya oxygen kwenye misuli ya mwili ili iweze kufanya kazi kwa ufanisi unao hitajika. Kitendo cha moyo kusambaza damu hulazimu kuongeza mapigo yake kwa kasi zaidi ya kawaida, na hivyo kuisaidia misuli ya moyo kuhimarika na ata mapigo ya moyo kuwa yenye afya hivyo kupunguza uwezekano wa kupata magonjwa ya moyo.


  • Huimarisha misuli ya mwili
kwa kufanya mazoezi ya Cardio misuli ya mwili hupata nguvu na anfya zaidi, na hivyo basi husaidia watu kufanya kazi zao za kila siku kama vile kubeba mizigo mizito kufanya kazi zinazolazimu nguvu zaidi kuliko kazi zingine. Kwa sababu hyo basi mtu hujihisi fiti na mwenye nguvu mda wowote.


  • Husaidia kupata usingizi kirahisi
Mazoezi ya Cardio hutumia nguvu nyingi kufanya na hvyo hufanya mwili kuchoka na hivyo kuhitaji kupumzika. Hivyo basi kwa watu wanao pata shida kupata usingizi wanashauriwa wajitaidi kufanya mazoezi hayo ili kuweza kuondokana na hali hiyo 


  • Huongeza uwezo wa kukumbuka na kuelewa
Kutokana na utafiti wa kitaalamu kutoka "University of British Colombia" ni kwamba mazoezi ya Cardio huathiri sana eneo la ubongo litwaalo hippocampus linaloshuhulika na kumbukumbu na uwelewa.
Hivyo mtu mwenye kufanya mazoezi hayo anaweza kuongeza uwezo wa ubongo wake kwa asilimia kubwa,


  • Huongeza ufanisi kwenye tendo la ndoa
Mazoezi ya Cardio husaidia sana kuhimarisha maongo ya siri kwa kigezo cha usambazaji damu kwa kiasi kikubwa na pia kwa kigezo cha kukaza misuli ihusianayo na maungo hayo, na hupunguza uwezekano wakutoweza kusimamisha kwa wanaume  .
 Mtu afanyaye mazoezi hayo huwa na stamina zaidi na huenda mda mrefu bila kuchoka mapema, hivyo basi kuhimarisha mahusiano zaidi kati ya pande mbili.

Kama umeipenda andiko hili basi gonga NZURI  na  kwa maswali na maoni zaidi basi tuandikie baada ya andiko hili, na pia kama ungependa kusoma andiko jengine kama hili basi jisajili kwa kuweka anuani yako juu kwenye linki ya KUJISAJILI.
Pia waweza tuandikia kwa email yetu Kuafit08@gmail.com
Kwa number yetu ya Tigo +255653009477
Instagram account yetu  (KUAFITI), Facebook-(kuafit),
 twitter-(kuafit) 


About benson godfrey

benson godfrey
Recommended Posts × +

DIET YA KUTOA SUMU MWILINI NA KUPUNGUZA UNENE KWA HARAKA

Habari zenu wadau wa KUAFIT! leo tutaongelea kuhusiana na elimu ya lishe ambayo itahusiana na diet ambapo tutaelezea mambo mengi san...