latest Post

VIGEZO VYA KUPATA MATOKEO MAZURI MAZOEZINI




Ni Mara nyingi sana watu hulalamika kwamba hawaoni matokeo mazuri ambayo wanatarajia kwa kufanya mazoezi wanayofanya na wengi hukata tamaa kutokana na changamoto kama hii.
Inapaswa kufahamika kwamba ili mtu aweze kupata matokeo anayotaka anapaswa kujua yafwatayo.
1. Ili mtu aweze kufanikiwa katika kupata matokeo anayoyataka anapaswa kujua ni mwili wa aina gani alionao na anapswa kufanya mazoezi ya aina gani kulingana na aina ya mwili wake. Miili ya watu imegawanyika katika makundi matatu kulingana na ukubwa ambayo ni
(I) Mesomorph- mwili wa wastani
(II)Endomorph - mwili mkubwa
(III) Ectomorph - mwili mdogo


Mfano: mwili mdogo(ectomorph) anashauriwa kupunguza mazoezi ya cardio( kama vile kukimbia sana n.k) ambayo yanaweza kumpunguza akizidisha na inamfaa aweanafanya mazoezi ya kujenga mwili eidha kwa mazoezi ya kawaida ama kupitia vyuma.


2.Nidhamu ni kitu cha msingi sana kuliko vyote maana bila nidhamu huwezi kupunguza ama kuacha chakula kisichokufaa kulingana na malengo yako, na pia nidhamu ni muhimu hasa pale unapojisikia kutokufanya mazoezi lakini inabidi. Watu wengi hawana nidhamu na ndipo wanashindwa kupata matokeo wanayohitaji.




3. Chakula ni kigezo kikubwa sana katika kuongeza, kupunguza ama kutunza taswira ya mwili wako. Hivyo kama mtu hawezi kuangalia anachokula basi kupata matokeo anayoyahitaji itakuwa vigumu.
Ni vyema mtu azingatie sana haya ili aweze kupata matokeo mazuri

Kama umelipenda andiko hili basi gonga NZURI  na  kwa maswali au maoni zaidi basi tuandikie baada ya andiko hili, na pia kama ungependa kusoma andiko jengine kama hili basi jisajili kwa kuweka anuani yako  kwenye linki ya SUBSCRIBE.


Pia waweza tuandikia kwa email yetu Kuafit08@gmail.com 


Kwa number yetu ya Tigo +255 653 009 477 

About Kuafit

Kuafit
Recommended Posts × +

0 comments:

KUPUNGUZA UZITO KWA MAJI YA BARIDI

Watu wengi katika jamii hupendelea kuoga na maji ya moto katika majira yote ya hewa lakini kutokana na utafiti uliofanywa na wanasayansi kam...