latest Post

MAAJABU KUMI YA TANGO KIAFYA


Karibu tena katika makala nyingine ya kaufit.Siku zote mwili wa binadamu ili uweze kuwa katika afya nzuri nahitaji virutubisho mbalimbali ambavyo vinapatikana katika  vyakula tunavyokula kila siku.Pale mwili unapokosa virutisho hivyo basi upelekea mwili  kuwa dhaifu kiafya(kumbuka mwili haujengwi na matofali).

Tango ni tunda mojawapo ambalo linafahamika sasa na ni moja ya tunda lenye virutubisho vingi sana ambayo uwezesha mwili kuwa na afya njema.Tango ni chanzo kizuri cha Kashiamu, Chuma, Vitamini C, Phosforas, Potasiamu, Zinki, Kambalishe, Vitamini B complex na Vitamin E.

Unapojua umuhimu wa kitu inakuwa ni rahisi sana kuanza kuchukua uamuzi na kufanyia kazi.Vivyo hivyo katika swala zima  la virutubisho katika mwili wako, pale unapojua umuhimu wa kula tunda fulani  na faida zake katika afya ya mwili wako,utachukua uamuzi wa kuanza kulila mara kwa mara.

kabla sijakupa faida za tunda la Tango ningependa ufahamu hili ya kuwa  kujua umihimu au faida  za kula matunda ni tofauti na mtu aliyechukua hatua ya kuanza kula matunda mara kwa mara.Watu wengi wanafahamu umuhimu wa kula matunda lakini sio wote waliochukua hatua ya kula matunda mbalimbali hata kama yanapatikana kwa urahisi.Nategemea msomaji wangu  wewe utakuwa wa tofauti unapojua faida za kula matunda  ni vyema ukaanza kula mara kwa mara .


FAIDA ZA KULA TUNDA LA TANGO


1.HUSAIDIA MMENG'ENYO WA CHAKULA MWILINI

Tango husifika katika kusaidia katika mmeng'enyo wa chakula na pia kuondoa sumu tumboni na kurahisisha ufyonzwaji wa protein mwilini kutokana na uwepo wa erepsin enzyme.


2.UPUNGUZA HATARI YA KUPATA KANSA

Tango husaidia kuondoa hatari ya mtu kupata kansa kwa  sababu zina kiwango kikubwa cha virutumbisho viitavyo lignas ambavyo husaidia kuondoa sumu mbalimbali na kuiboresha kinga ya mwili.

3.HUONGEZA VITAMIN C MWILINI

Tango linakiwango kikubwa na vitamini C ambayo husaidia kuondoa matatizo mbalimbali yanayosababishwa na ukosefu wa vitamin C kama vile kuota meno na mifupa vibaya pia kutokwa na damu kwenye fizi.

4.HUBORESHA KIWANGO CHA MAJI MWILINI

Mwili wa binadamu unahitaji kuwa na maji muda wote ,pale mwili wako unapokosa kuwa na maji afya ya mwili wako ipo hatarini.Ulaji wa matango usaidia kuboresha kiwango cha maji mwilini ambayo husaidia kuondoa taka mwilini na sumu zilizopatikana katika ulaji wa vyakula mbalimbali.


5.HUONDOA HARUFU MBAYA KINYWANI

Kwa wale wanaosumbuliwa na kuwa na harufu mbaya kinywani wanashauriw kula  matango mara kwa mara kwa sababu huweza kuua bakteria mbalimbali wasababishao magonjwa mbalimbali ya kinywa na harufu mbaya kinywani.


6.NI TIBA YA HANGOVER

Kwa wale wanaosumbuliwa na hangover au kichwa kuuma nyakati za asubuhi,wanashauriwa kula tango kabla ya kwenda kulala,matango yana vitamini B  na electrolyte ambayo husaidia kuondoa hali ya hangover.


7.KINGA DHIDI YA SARATANI

Kula tango mara kwa mara humsaidia mlaji kujikinga dhidi ya saratani za aina mbalimbali,tango lina kiwango kikubwa cha  uchachu(alkaline) ambacho huzuia seli za saratani kuishi kwani haziwezi kuishi kwenye mazingira ya uchachu.


8.UBORESHA AFYA YA NYWELE NA KUCHA 

Madini ya silicon na sulfur yaliyopo kwenye tango husaidia ukuaji wa nywele zako na kucha kung’aa na kuwa imara Zaidi.

9.UPUNGUZA MSONGO WA MAWAZO

Tunda hili aina ya tango lina kiwango kikubwa cha vitamini B ambayo husaidia kuboresha utendaji mzima wa mishipa mbalimbali ya ufahamu mwilini,hivyo husaidia kuondoa hatari ya mtu kuathirika na msongo wa mawazo.

10.HUSAIDIA KUPATA CHOO

Kama unasumbuliwa na kupata choo mara kwa mara,pend kula tunda hili la tango kwani litakusaidia kupata choo laini.Tunda lingine linaloweza kukusaidia kupata choo ni pamoja na ulaji wa mapapai.

Kama umeipenda chapisho hili basi gonga NZURI  na  kwa maswali au maoni zaidi basi tuandikie baada ya andiko hili, na pia kama ungependa kusoma andiko jengine kama hili basi jisajili kwa kuweka anuani yako  kwenye linki ya SUBSCRIBE.

Pia waweza tuandikia kwa email yetu Kuafit08@gmail.com 
Kwa number yetu ya Tigo +255 653 009 477  
Instagram account yetu  (KUAFITI), Facebook-(kuafit)

About Davis David

Davis David
Recommended Posts × +

DIET YA KUTOA SUMU MWILINI NA KUPUNGUZA UNENE KWA HARAKA

Habari zenu wadau wa KUAFIT! leo tutaongelea kuhusiana na elimu ya lishe ambayo itahusiana na diet ambapo tutaelezea mambo mengi san...