latest Post

NJIA YAKUJENGA MAKALIO NA HIPS KUPITIA MAZOEZI

Wakina dada wengi  huuliza "je ni njia gani wanaweza jenga mmili yao vizuri hususani makalio na hips?" jibu lake ni kuna njia nyingi za kujenga  misuli ya hips na kalio. aina hizo za mazoezi hutegemeana na matakwa ya mtu binafsi na sehemu hususani anapotaka apashuhulikie. Mazoezi yapo mengi ya kujenga sehemu hizo, na hayo ni kama vile....


LUNGES
Haya ni mazoezi ambayo hugusa misuli ya makalio na pia hips kwa sana, hufanywa kwa namna tatu ambazo ni
  •  ya kukunja mgu mmoja mbele na nyuma  kwa uendelevu bila kutoka eneo ulilopo (1.Static)
  • kukunja miguu pembeni kwazamu kwa kila mguu, na hii hugusa sana hips (2.side)
ya kukunja mgu mmoja mbele na nyuma  kwa uendelevu bali nikwakuelekea mbele


SUMO SQUARTS

Hii ni aina ya squart ambayo humtaka mtu atanue miguu pembeni mwa mwili wake na akunje kwa kusimama na kushuka. hili zoezi hugusa zaidi  makalio zaidi ya hips

SQUART YA KAWAIDA
hii ni aina ya suart ya kawaida (Regular squart), zoezi hili humuitaji mtu akunje miguu na magoti kuelekea mbele. zoezi hili uathiri hips pamoja na makalio kwa ujumla.

BRIDGE PAUSE
bridge pause ipo ya namna mbili ambazo  ni yakawaida(1.regular) hii huweka sehemu ya juu ya mgongo chini na huweka gimuu chini na kiuno juu. (2. one-legged bridge)  hii huweka sehemu ya juu ya mgongo chini na huweka mguu moja chini na mwingine huelekezewa juu humalizia kwa kuweka kiuno juu.
mazoezi haya hugusa makalio kwa sana

DONKEY KICK
Mguu wa punda (Donkey kick) ni zoezi linalo muhitaji mtu aweke goti moja chini akiweka na support ya viwiko na kunyanyua mguu juu. zoezi hili hujenga kalio na hips bali hugusa sana misuli ya makalio

STEP UP
hili ni zoezi ambalo uhusisha mguu mmoja kukanyaga pahali palipo inuka kama vile ngazi na kusimamia mguu huohuo uliokanyaga chini,  pia zoezi hilo hufanywa na miguu yote miwili na kila mguu hufanya kwa kurudia kwa Marudio(Set) kadhaa

DEAD LIFT
Zoezi hili uhusisha mtu kushika uzito wowote kwa kutegemea kwa viwango, hufanywa pale mtu anapoinama mbele bila kujikunja miguu na kushuka na uzito huku miguu imekaa usawa wa miguu na kurudi katika usawa wa wima. zoezi hili lina sadikika kua ndilo zoezi pekee lenye kuonyesha mabadiliko halisi na huongeza makalio kwa kiasi kikubwa mno

kwa maswali zaidi na maoni tafadhali uliza baada ya chapisho hili
KAMA UMEPENDA CHAPISHO HILI PIA WAWEZA COMMENT


About benson godfrey

benson godfrey
Recommended Posts × +

DIET YA KUTOA SUMU MWILINI NA KUPUNGUZA UNENE KWA HARAKA

Habari zenu wadau wa KUAFIT! leo tutaongelea kuhusiana na elimu ya lishe ambayo itahusiana na diet ambapo tutaelezea mambo mengi san...