latest Post

FAIDA YA KUNYWA MAZIWA FRESH



Maziwa fresh ni kati ya vyakula muhimu sana na ni kati ya vyakula vyenye mchango mkubwa katika kujenga na kuhifadhi afya ya mwili wa mtu. Kikawaida katika jamii yetu maziwa hutumika kutengeneza chai, gee na hata vyakula vya kiasili hivyo basi maziwa hutumika kwa matumizi mengi sana.
Kutokana na virutubisho vingi vilivyomo ndani ya maziwa vikiwemo protini, vitamini na kadhalika, kunafanya chakula hiki kuwa muhimu na hushauriwa kwamba mtu aweze kunywa maziwa mara nyingi awezavyo katika wiki.




Faida za kunywa maziwa zipo nyingi bali tutaongelea sababau 3 za kunywa maziwa fresh ya Ng'ombe.




                                       
  • Kuhimarisha mifupa ya mwili na hii ni kutokana na virutubisho kama vile calcium, vitamini D na phosphorus ambavyo vyote kwa pamoja huimarisha sana mifupa ya mwili. Kwa watu wanaofanya shughuli ngumu na za kutumia nguvu maziwa yanaweza yakawa ni chakula kizuri sana.



                                    
  • kujenga misuli ya mwili kutokana na protini inayopatikana katika maziwa. Mtu anayefanaya mazoezi hasa mazoezi ya kujenga misuli kwa kunyanyua uzito anauwezo mkubwa kujenga misuli. Watu wakufanya mazoezi ya kujenga misuli hasa (bodybuilding) kinaweza kumsaidia kupata matokeo ya haraka



                                     
  • kusaidia kupunguza unene wa mwili kwa kipindi kirefu. Maziwa fresh yanasemekana huwa na tabia ya kupunguza unene wa mtu endapo mtu huyo atatumia chakula hiko cha maziwa yakiwa fresh na kuhakikisha kiwango cha mafuta ni kidogo sana kwa kuangalia jeduali lililopo nyuma ya chombo kilichohifadhi maziwa kwa wale wasioweza kupata maziwa ya ngombe. 


                                     
  • Maziwa husaidia pia kutibu mtu mwenye jeraha la ngozi hasa pale mtu anapojaribu kuotesha ngozi pale ilipoharibika.Kutibu jeraha kunawezekana kutokana na kwamba maziwa yenye kiwango kidogo cha mafuta huwa na uwezo mkubwa wa kurudisha ngozi iliyochubuka.    


 
                                        
Bali pia inapaswa kufahamika ya kwamba sio kila mtu anaweza kutumia maziwa hasa kwa kupata tatizo la kutoweza kumeng'enya chakula tumboni(lactose intolerance), hivyo sasa inabidi ifahamike ya kwamba kuna aina zaidi ya moja ya maziwa . Aina zingine za maziwa ni pamoja na

(I) maziwa ya soy


(II)maziwa ya Nazi nakadhalika.


 Maziwa haya mengine yanaweza kutumika na watu wasio tumia maziwa fresh ya Ng'ombe bali mnakumbushwa kyangalia kwenye jeduali ya yaliyomo kwenye chombo kilichohifadhi maziwa maana kwa mara nyingi maziwa hayo huongezewa mafuta, ladha na kadhalika hivyo kuweza kuongeza uzito na pia kemikali hatarishi mwilini
Kama umelipenda andiko hili basi gonga NZURI  na  kwa maswali au maoni zaidi basi tuandikie baada ya andiko hili, na pia kama ungependa kusoma andiko jengine kama hili basi jisajili kwa kuweka anuani yako  kwenye linki ya SUBSCRIBE.


Pia waweza tuandikia kwa email yetu Kuafit08@gmail.com 


Kwa number yetu ya Tigo +255 653 009 477  

About Kuafit

Kuafit
Recommended Posts × +

0 comments:

KUPUNGUZA UZITO KWA MAJI YA BARIDI

Watu wengi katika jamii hupendelea kuoga na maji ya moto katika majira yote ya hewa lakini kutokana na utafiti uliofanywa na wanasayansi kam...