latest Post

JINSI YA KUJENGA NA KUONGEZA MWILI KWA KUTUMIA VYAKULA





Nikweli kuwa watu wengi hutamani kupungua mwili bali wengi  hutamani kuongeza miili yao, kutokana na maombi ya wengi leo nitaongelea jinsi ya kuongeza na kujenga mwili kupitia vyakula vyaa aina tofauti na umuhimu wake pia katika mwili.

Kwanza inabidi kujua kuwa kuongezeka na kupungua kwa mwili unawezekana inagawa sio kitu kirahisi sana kufanya, na kulingana na utafiti inaonyesha watu wanaotamani kuongeza mwili ni wengi(asilimia 54%)  kulinganisha na watu wanaotamani kuongeza mwili(asilimia 46%) kwa mwaka. Kuongeza mwili kunachangamoto nyingi ambazo huchangia watu wengi kukata tamaa kama vile kujua ni vyakula gani kula na nidhamu ipi inapaswa kuzingatiwa. Basi leo tutagusia aina mbalimbali vya vyakula, vyakula hivyo ni....


  • Nyama nyekundu
Nyama nyekundu kama vile nyama ya ngombe ni muhimu sana hasa kwenye kujenga mwili, nyama nyekundu hwua na leucine(amino acid) yenye kusaidia misuli ya mwili kwenye kutanuka kwa kutumia protini. Hivyo ni vyema kutumia nyama nyekundu zaidi ya mara mbili kwa wiki ili kuhakikishia ukuaji na utanuzi wa misuli ya mwili.



  • Karanga na siagi
Karanga ni aina ya chakula ambacho kimejaliwa mafuta na calorie(ni aina ya kipimo cha nguvu kilio ndani ya chakula kinachopimwa kwa uwezo wa kupandisha gram moja ya maji kwa nyuzi 1celsius).
Karanga na siagi kwa pamoja hua na ladha nzuri mdomoni na pili huchangia uongezekaji wa mwili kwa kiasi kikubwa.


  • Parachichi
Parachichi ni tunda zuri na hupendwa na wengi na pia huwa na ladha ya kuridhisha mdomoni na hutumika na wengi duniani. Mbali na hapo parachichi ni tunda lenye uwezo wa kuongeza calorie 322 kwa kila parachichi moja mtu atakalo kula. Pia parachichi huongeza mafuta kwenye mwili ambayo ni muhimu kwenye kujenga misuli ya mwili


  • Mafuta ya asilia
Watu wengi hula na kupikia mafuta mbalimbali majumbani bila kujua adhari na faida ya mafuta hayo, hivyo leo ntawajuza kwa kugusia swala hili. Mafuta hasa ya asili kama vile mafuta ya Olive na  Karanga yanajenga na kuhimarisha zaidi mwili kwani hutokana na mimea asilia ambayo ni rahisi kutumika na mwili tumboni kulinganisha na mafuta mengine. Hivyo na pendekeza mtu anyetaka kuongeza mwili atumie mafuta asili


  • Maziwa 
Maziwa ni aina moja ya lishe iliojaa virutubisho vingi ambavyo vingi  huitajiaka mwilini kama vile carbs,protini na mafuta. Maiziwa ni muhimu sana kwa watu wenyekutaka kuongeza mwili na inashauriwa sana kwa wa beba vyuma kunywa angalau lita 1 mpaka mbili kwa siku ili kuhakikishia uongezekaji wa mwili


  • Matunda yaliyo kaushwa
Matunda yaliyo kaushwa ni muhimu sana kwa maana hua na vitamini, fiber na madini zaidi kulinnganisha na matunda ambayo hayajakaushwa na hivyo kuongeza utengenezaji wa misuli kwa kuongea calorie nyingi mwilini. Hivyo basi inashauriwa kula japo mara mbili na zaidi ilikuhakikisha ukuaji wa mwili


  • Viazi
Viazi ni aina ya  vya vyakula ambavyo hutajika sana mwilini kwa mtu ambaye anayetamani kuongeza mwili, Mbali na sifa zake za  kuwa na uwezo wa kusaidia misuli ya mwili kwenye uhifadhi glycogen, viazi hua na fiber na madini mengi. Hivyo basi ningependa kushauri watu wengi kutumia viazi hasa wenye kutaka kujenga miili kwa vyuma.

Kwa vyakula hivyo basi ni rahisi sana mtu kuongeza mwili wake na akwa anafanya mazoezi basi hua rasi zaidi kwake kua na monekano mzuri,
Basi kama andiko hili limekuvutia weka nzuri na comment chini baada ya andiko hili, na jiunge na jamii ya KUAFIT kwa kujiunga kupitia link ya kujisajili hapo juu kwa kuweka email ili kupata maandiko mapya ya kila siku.

About Kuafit

Kuafit
Recommended Posts × +

0 comments:

KUPUNGUZA UZITO KWA MAJI YA BARIDI

Watu wengi katika jamii hupendelea kuoga na maji ya moto katika majira yote ya hewa lakini kutokana na utafiti uliofanywa na wanasayansi kam...