latest Post

FAIDA 6 ZA KUNYWA MAZIWA YA MTINDI



Maziwa aina ya mtindi yanaorodheshwa kuwa ni miongoni mwa vyakula bora na muhimu katika afya ya binadamu.Maziwa haya ya mtindi huwa na virutubisho vingi ambavyo vina faida nyingi katika mwili wa binadamu.

Baadhi ya virutimbo vilivopo katika maziwa ya mtindi ni ‘Molybdenum’,‘Potassium’, ‘Riboflavin (vitamin B2),Iodine’,‘Phosphorus’,‘Pantothenic acid (vitamin B5) ‘Zinc’,‘Calcium’ na ‘vitamin B12’.Mbali na virutimbo vinavyopatikana kwenye mtindi pia ndani ya mtindi kuna 'bakteria hai' ambao ni muhimu katika afya yako.

Ni lini mara yako ya mwisho kupata maziwa mtindi? Ni vyema  ukayafanya kama sehemu ya chakula chako ama baada ya chakula ama kabla ya chakula, yatakusaidia. Soma faida zake hapa.


FAIDA YA MAZIWA YA MTINDI

1.Kinga ya Mwili


unywaji wa mtindi kila siku, huamsha na kuupa nguvu mfumo wa kinga ya mwili kupambana na magonjwa kadhaa ya maambukizi, ikiwemo saratani ya utumbo.


2.Kupunguza Uzito


Mbali ya faida hizo, mtindi pia umeonekana kupunguza mafuta (fat) mwilini na kwa maana hiyo una uwezo wa kupunguza unene unaotokana na mafuta mengi mwilini.kwa watu wenye mpango wa kupunguza uzito wanashauriwa kunywa mtindi mara kwa mara huku wakiendelea kufanya mazoezi mbalimbali ya kupunguza uzito.


3.Kujenga Misuli

Maziwa ya mtindi yana mchango mkubwa katika ukuaji wa misuli. Hili ni kutokana na protini zinazopatikana katika maziwa.Maziwa huzuia maumivu ya misuli pamoja na kurudisha ute ulipotea kwenye maungo ya magoti na viwiko wakati wa kazi mbalimbali.Unashauriwa kunywa maziwa ya mtindi mida ya joini baada ya kutoka katika shughuli zako za siku nzima.

4.Hurefusha Maisha


Utafiti unaonesha kuwa unywaji wa mtindi mara kwa mara, hasa katika kundi la wazee umeongeza uwezo wa mwili kupambana na magonjwa mbalimbali na kuufanya mfumo wa kinga mwilini kuwa imara zaidi.


5.Kuupa mwili Nguvu


Watu ambao huwa wanaishiwa na nguvu mwilini mara kwa mara wanashauriwa kupenda kunywa maziwa ya mtindi kwani huwa na uwezo wa kuupa mwili nguvu kupitia virutubisho vya wanga vinavyopatikana katika maziwa ya mtindi.

6.Kupunguza Lehemu mbaya mwilini


Maziwa ya mtindi pia husaidia kupunguza kiwango cha lehemu mbaya mwilini (Low Density Lipoproteins-bad cholesterol) ambayo huweza kuongeza hatari ya matatizo kama shinikizo la damu, magonjwa ya moyo na kiharusi.Maziwa ya mtindi pia uweza kupandisha kiwango cha lehemu nzuri mwilini (High Density Lipoproteins–good cholesterol) ambayo huruhusu mwili kutengeneza vitamin D na kusaidia mwili kutengeneza baadhi ya homoni. .


Unashauriwa  kunywa mtindi halisi uliotengenezwa kutokana na maziwa halisi ya ng’ombe, siyo mtindi uliotengenezwa kutokana na maziwa ya unga. Mtindi halisi utambulika kutokana na ule uchachu unaotokana na ‘bakteria hai’ wanaopatikana baada ya maziwa kuganda na kuchachuka.


Kama umeipenda andiko hili basi gonga NZURI  na  kwa maswali au maoni zaidi basi tuandikie baada ya andiko hili, na pia kama ungependa kusoma andiko jengine kama hili basi jisajili kwa kuweka anuani yako  kwenye linki ya SUBSCRIBE.

Pia waweza tuandikia kwa email yetu Kuafit08@gmail.com 
Kwa number yetu ya Tigo +255 653 009 477  
Instagram account yetu  (KUAFITI), Facebook-(kuafit) na twitter-(kuafit

About Unknown

Unknown
Recommended Posts × +

0 comments:

KUPUNGUZA UZITO KWA MAJI YA BARIDI

Watu wengi katika jamii hupendelea kuoga na maji ya moto katika majira yote ya hewa lakini kutokana na utafiti uliofanywa na wanasayansi kam...