latest Post

FAIDA ZA MCHAICHAI KWA AFYA YAKO



Leo nakuletea faida zitokazo na Mchaichai kwa lunga ya kiingereza ni maarufu kwa jina la lemon grass na cymbopogon kwa lugha za wataalam  wa mimea.Kwanza inabidi tufahamu mchaichai nini hasa? Mchaichai ni mmea ambao unatambulika hapa nchini pamoja na Afrika kwa ujumla wake, lakini hapa nchini wengi huutambua mmea huu kama kiungo katika chai na husaidia kinywaji hicho kuwa na harufu nzuri zaidi na kuwavutia watumiaji wake.

Kihistoria mchaichai ulianza kulimwa  nchini ufilipino mnamo Karne ya 17 baadae ukaingia katika nchi ya Haiti mwaka 1799  ambapo huko kilimo kilikuwa sana hadi mwaka 1917 Baadhi ya wataalam wa mimea wakaanzisha mashamba ya mchaichai kwa ajili ya utafiti Nchini marekani, miaka ya 1947 soko la mchaichai ukarasimishwa katika jimbo la calfonia.

Mchaichai hufahamika sana kwa watu wengi lakini si watu wengi wanaofahamu faida ipatikanayo na mchachai wengi wetu tumeufahamu kama kiungo tu cha chai ila atufahamu  faida nyingi zipatikanazo katika mchaichai.Mchaichai una virutubisho mbalimbali ambayo ni muhimu sana kwa afya ya binadamu kama vile Vitamin A,B1 (thiamine ),B2(Riboflavin ),B3 (niacin ),B5 (pantothenic acid ),B6 (pyridoxine),folate na vitamin C pamoja na madini ya potassium, madini Chokaa, magnesium, manganese, Copper, zinc na  phosphorus.


FAIDA ZA KUTUMIA MCHAICHAI


1.KUSAFISHA FIGO NA MKOJO

Mchaichai una kazi ya kusafisha figo ambayo kazi yake kubwa ni kusafisha damu katika mwili, kuondoa mafuta mabaya mwilini ambayo mengi yanatengenezwa na kemikali za viwandani na hivyo mwili kushindwa kuziondoa na baadaye kusasababisha magonjwa mbalimbali.Figo inapokuwa safi na imara,hata kazi nyingine kama kusafisha mkojo zinafanyika
kirahisi

2.HUSAIDIA UMENGENYWAJI WA CHAKULA MWILINI

Mchaichai husifika kusaidia urahisishaji wa mmengenyo wa chakula mwilini  na kutibu maumivu ya tumbo kama vile hali ya tumbo kujaa gesi.


3.KUZUIA HALI YA KUHARISHA MARA KWA MARA

Mchaichai pia ni dawa nzuri kwa wale wanaosumbuliwa na hali ya kuarisha mara kwa mara,kwani inauwezo wa kupambana na mdudu aina ya protozoa anayesababisha ugonjwa huu.

4.HUSAIDIA KUSAFISHA DAMU

Faida nyingine ya mchaichai ni kusafisha damu mwilini hasa kwa watu ambao wamekuwa na tabia ya kupata magonjwa ya ngozi kama mapele na kutoka majipu.

5.HUUPA MWILI KINGA DHIDI YA UGONJWA WA SARATANI.

Mchaichai umegundulika pia unauwezo wa kuua seli zinazoweza kusababisha ugonjwa wa saratani.Kwani kwenye kila gram 100 ya mchaichai kuna virutumbisho ambavyo vinaweza kuondoa na kuukinga mwili dhidi ya sumu ambayo inasababisha ugonjwa wa saratani.


6.KUONDOA MLUNDIKANO WA MAFUTA KATIKA MISHIPA YA DAMU

Mchaichai husaidia  kuondoa mafuta katika mishipa ya damu  hivyo kuruhusu damu kupita vizuri katika sehemu mbalimbali za mwili na kuifanya mishipa hiyo kuwa na afya njema.Pia kusaidia mapigo ya moyo kuwa katika hali nzuri wakati wote.


JINSI YA KUTUMIA MCHAICHAI

Kupata faida hizi unashauriwa majani ya mchaichai yalowekwe katika maji ya moto kiasi cha vikombe vitatu vya chai, weka majani ya mchaichai kisha kunywa maji hayo kiasi cha kikombe kimoja  cha chai kabla ya kula chochote asubuhi, mchana, nusu saa kabla ya mlo, na jioni kabla ya chakula cha jioni.Pia unaweza kutia sukari kwa kiasi kidogo mno. Unaweza fanya jambo hili kuwa endelevu kwa kutumia chai ambayo imepikwa kwa majani ya mchaichai mara kwa mara.

Kumbuka faida zilizo tajwa hapo juu ni chache tu ambazo nimekuletea siku ya leo na  ni matumaini yangu utanza kutumia mchaichai kuwa sehemu ya lishe yako ili kupata virutubisho mbalimbali  na kujikinga dhidi ya magonjwa mbalimbali.

Kama umeipenda chapisho hili basi gonga NZURI  na  kwa maswali au maoni zaidi basi tuandikie baada ya andiko hili, na pia kama ungependa kusoma andiko jengine kama hili basi jisajili kwa kuweka anuani yako  kwenye linki ya SUBSCRIBE.

Pia waweza tuandikia kwa email yetu Kuafit08@gmail.com 
Kwa number yetu ya Tigo +255 653 009 477  
Instagram account yetu  (KUAFITI), Facebook-(kuafit)



About Unknown

Unknown
Recommended Posts × +

0 comments:

KUPUNGUZA UZITO KWA MAJI YA BARIDI

Watu wengi katika jamii hupendelea kuoga na maji ya moto katika majira yote ya hewa lakini kutokana na utafiti uliofanywa na wanasayansi kam...