latest Post

MAZOEZI ANAYOPASWA KUFANYA MAMA MJAMZITO





 Je! wajua kwamba mwanamke mjamzito anapaswa kufanya mazoezi kulingana na wiki alizofikia?


Ndio! ni kulingana na wiki.

kwa kitaalamu kipindi cha ujauzito wa mwanamke umegawanyika katika vipindi vitatu, na vipindi hivyo hutambulika kulingana na wiki alizofikia mwanamke mjamzito kwenye kipindi cha ujauzito wake.
Inapendekezwa kwamba mazoezi kwa wanawake wajawazito yafanywe kulingana na wiki ili asiweze kuadhiri ukuaji wa mtoto tumboni na pia kuadhiri afya ya mwanamke mjamzito kutokana na ufanyaji mbovu wa mazoezi. Wiki hizo zimegawanyika kulingana na wiki kama ifwatavyo; 
  1. Trimester ya kwanza ni kwanzia wiki ya kwanza(1) mpaka wiki ya kumi na mbili(12)
  2. Trimester ya pili nu kwanzaia wiki ya kumi na tatu(13) mpaka wiki ya ishirini na sita(26)
  3. Trimester ya tatu ni kwanzia wiki ya ishirini na saba mpaka(27) mpaka kujifungua kwa mama mjamzito
Vipindi hivyo vya ujauzito ni pamoja na:- 

  • kipindi cha kwanza(first trimester)


Ndani ya kipindi hiki cha kwanzia wiki ya kwanza hadi wiki ya 12 mazoezi yanayoweza kufanyika ni .Yoga
.Mazoezi ya kutembea
.Kazoezi ya aerobics
.Kunyanyua vyuma vidogo
.Kuogelea

  • kipindi cha pili(second trimester)


Ndani ya kipindi hiki cha kwanzia wiki ya 13 hadi 27
mazoezi yanayoweza kufanyika ni pamoja na .Mazoezi ya kujinyoosha
.Yoga
.Mazoezi ya kutembea
.Mazoezi ya kucheza muziki (mfano salsa)

  •  kipindi cha tatu( third trimester)


Ndani ya kipindi hiki cha kwanzia wiki ya 28 hadi wiki ya kujifungua mjamzito anaweza akafanya mazoezi ya .Mazoezi ya kutembea
.Mazoezi ya kujinyoosha.


ANGALIZO! mazoezi ya tumbo hasa mazoezi ya situps na crunches hayashauriwi kufanywa hii ni kwajili ya kuepusha kuhatarisha maisha ya mtoto.

Kama umelipenda andiko hili basi gonga NZURI  na  kwa maswali au maoni zaidi basi tuandikie baada ya andiko hili, na pia kama ungependa kusoma andiko jengine kama hili basi jisajili kwa kuweka anuani yako  kwenye linki ya SUBSCRIBE.


Pia waweza tuandikia kwa email yetu Kuafit08@gmail.com 


Kwa number yetu ya Tigo +255 653 009 477  


Instagram account yetu  (KUAFITI), Facebook-(kuafit) na twitter-(kuafit





About Kuafit

Kuafit
Recommended Posts × +

0 comments:

KUPUNGUZA UZITO KWA MAJI YA BARIDI

Watu wengi katika jamii hupendelea kuoga na maji ya moto katika majira yote ya hewa lakini kutokana na utafiti uliofanywa na wanasayansi kam...