latest Post

MAJERAA YANAYOTOKANA NA MAZOEZI NA JINSI YA KUYAKABILI


 Kutokana na maombi ya watu wengi leo tutaongelea majeraa ambayo yanayoweza kuletwa na ufanyaji wa mazoezi usio sahihi. Nitaanza kwa kutoa ufafanuzi mdogo juu ya misuli ya mwili na mazoezi, alafu nitaongelea matatatizo na majeraa yanayoweza tokea kwa ufanyaji mbaya wa mazoezi.
Nikweli kuwa mwili wa mwanadamu umeundwa kwa misuli mingi na viungo vingi sana ambavyo hutusaidia katika maisha yetu ya kila siku kama vile kutembea, kusogezea viungo vingine vya mwili na kadhalika, na huchangia sana katika swala la miuonekano yetu na pia huwa tunapenda kufanyisha mazoezi ili izidi kuwa imara na kuwa na muonekano mzuri. Kutokana na hayo, basi inabidi watu kuelewa kuwa kuna mambo kadha wa kadha kuyafahamu kabla ya kutaka kufanyisha misuli hiyo mazoezi.

Moja ya mambo ni kwamba misuli ya mwili hua imejengwa na asilimia kubwa ya protini ambayo huchangia utanukaji ama kujikunja kwa misuli na pia hua ni migumu na laini kwa kutegemea na sehemu na sehemu. Watu wengi wameshindwa kuwa na elimu ya kutambua kuwa misuli ya mwili hupaswa kuangaliwa kwa jicho la tatu maana yaweza kuumia, bali wengi hufanyisha mazoezi misuli isivyo bila kujua athari zake . Kutokana na hayo basi leo ntagusia majeraa na maumivu yanayoweza kuletwa na ufanyaji mbovu wa mazoezi.
 Mazoezi hayo ni.


  •  Misuli kuvuta 
Hii ni hali ya kuhisi maumivu makali kwenye misuli  inayohusiana na jointi za mikono na miguu. Maumivu hayo husababishwa na kufanya mazoezi mengi makali kuliko kawaida . Kuzuia hali inawapasa wanamazoezi kujinyoosha vizuri kabla na baada ya mazoezi  • Misuli kukaza
Hii ni hali inayotokea pali misuli ya mwili hujikaza na kusababisha maumivu makali ambayo hutokea na kuisha nda ni ya mda mchache. Maumivu hayo hutokana na kukaa pahali pamoja kwa mdaa mrefu au kufanya tendo moja kwa mda mrefu kama vile kukimbia ama kunyanyua vyuma kwa mda mrefu. Maumivu haya yanaweza kuzuiwa kwa kunyosha misuli ya kiungo kilicho kazwa ama kwa dawa za kuchua na kuchua pahali husika(mara nyingi hua kwenye miguu na mikono).  • Kuteguka kwa kiungo
Kuteguka kunatokana na usimamiaji, ukanyagaji ama ushikiliaji mbaya wa viungo vya mwili (kama vile miguu na mabega) hali husababisha maumivu makali na mda mwingine yaweza kufanya mtu akashindwa kabisa kutembea ama kushika kitu chochote. Marejaa haya huweza kuwa sugu yasipo tibiwa, bali huduma ya kwanza yaweza kusaidia kupunguza maumivu  na kumfanya  mgonjwa kuwa na hauweni. Huduma hiyo ya kwenza inayo weza kufanyika ni kumchua na dawa ya kuchua pili kumpatia vidonge vya kupunguza maumivu na kama hali itakua mbaya sana basi ni vyema kumuona daktari yeyote aliyekuwepo karibu.  •  Jeraa kwenye goti
Goti ni kiungo ambacho huunganisha sehemu ya miguu na paja, kiungo hiko kimetengenezwa na misuli itwayo Aterior cruciate ambayo mara nyingi huleta shida kama vile Aterior cruciate ligament tear( hali ya kuchanika kwa misuli hiyo). Tatizo hilo ni kubwa na mtu yeyote akipata tatizo hili anapaswa kufanya mambo haya yafwatayo;

  1. funga mgu kwa bandage yenye dawa
  2. weka kitu cha baridi(barafu) kwenye goti.
  3. Jaribu kuweka mguu suhemu ya juu palipo inuka kutoka kwenye kiwiliwili unapo lalia mgongo na hakikisha umekunjwa.
  4. Mwisho pumzika kwa mda mrefu

  • Jera la bega
Bega ni sehemu ya mwili yenye umuhimu mkubwa na inapo guswa basi uhathiri ufanisi wa mikono na mwili kwa ujumla. Maumivu. Hali mara nyingi husababishwa na misuli itwayo Bicep tendonitis kuuma ambayo ni misuli inayo unganishwa na misuli ya mikono na misuli ya mwanzo ya mabega. Misuli hiyo maranyingi huumia kwa kunyanyua vitu vizito. Hali hii yaweza kutatuliwa kwa kufanya mazoezi ya kujinyoosha na pia kwa kuchua kwa dawa za kuchua. na maumivu yakizidi basi ni vyema kumuona daktari.


  • Maumivu ya mgongo na kiuno
Majera ya mgongo na kiuno husababishwa hasa na kukaa vibaya ama kufanya mazoezi yanye kutumia uzito mkubwa . Maumivu hayo yaweza kutatuliwa kwa kufanya mazoezi ya kujiinyosha na pili kwakufanyiwa masaji ya mgongo.

Natumae umefurahia aandiko hili, kwa maoni na maswali basi tunaomba utuandikie na kama limekubamba basi gonga like baada ya hili andiko.

About benson godfrey

benson godfrey
Recommended Posts × +

DIET YA KUTOA SUMU MWILINI NA KUPUNGUZA UNENE KWA HARAKA

Habari zenu wadau wa KUAFIT! leo tutaongelea kuhusiana na elimu ya lishe ambayo itahusiana na diet ambapo tutaelezea mambo mengi san...