latest Post

MAMBO KUU SABA YAKUZINGATIA KABLA YAKUANZA AU KUTAKA KUANZA MAZOEZI GYM


Nikweli kwamba mara nyingi watu wengi hua na hofu pindi wanapotaka kunza mazoezi na kwanza kujiunga na GYM na hua wanajiuliza je ni vitu gani muhimu vyakujua kabla yakuanza mazoezi. watu wengine pia hua wakijiunga  kujiunga na GYM hua wanafanya mambo isivyopaswa.
sasa mambo yakuzingatia kwa wanaoza na wanaotaka kuanza na mazoezi ni

  1. Unapswa kujua Afya yako kikamilifu - watu wengi hujisahau kuijua afya zao na hvyo hua wanataka kujiunga na GYM na kufanya mazoezi makali, na hio sio sahihi. Kuijua afya yako kwa kupima magonjwa kama vile (kisukari, UKIMWI na presha)  inakupa uwigo mpana yakutambua ni kwa kiwango gani mwili waweza staimili mazoezi. Hivyo inashauriwa kuchukua vipimo na kama kuna tatizo lolote basi lifikishe kwa managment ya GYM ili wajue jinsi ya kukusaidia
  2. Usiogope kuuliza maswali pale usipoelewa - Ni vyema kuuliza maswali pale unapo kua mgeni GYM , usipende kujiaminisha sana kwakudhani unaweza kila kitu. bali penda kuchukua ushahuri kutoka kwa mwalimu wako wamazoezi ili akupe mwongozo wa kitu gani cha kufanya na nisa ngapi na wakati gani sahihi kufanya zoezi au jambo husika
  3. Hakikisha una taulo la jasho na maji ya kunywa kila uendapo zoezini - kwakufanya hvyo itakusaidia kuepusha  kuambukizana magonjwa ya ngozi  endapo utatumia kifaa ambacho mwenzio katumia. Maji ni muhimu sana hasa pale unapo tokwa na jasho jingi  kupita kiasi na mwili unapoishiwa maji (dehydrated), na inapaswa kunywa maji kiasi kidogo ili kupunguza uwezekano wakupali na maji.
  4. Usitegemee matokeo ya papo kwa papo - jambo hilo haliwezekani watu wengine wanadhani wakiingia GYM basi mabadilliko yatatokea  kwa siku moja na hiyo sio kweli. Mazoezi sio mateso bali yanakuhitaji ujitoe kikamilifu ili kupata mabadiliko unayotaka. Hvyo basi inakupasa ujitoe kwa moyo na uweke nia mbele ili kupata matokea yanayo hitajika.
  5. Usikubali kukatishwa tamaa ya kua huwezi zoezi flani na mtu asiyekua mwalimu wako wa mazoezi - watu wengi wanapenda kutatisha wenzio pale wanapotaka kufanya mazoezi flani kama kunyanyua vyuma vizito( power lifting) na hivyo kuondoa morali aliokua nayo awali. Fanya mazoezi madogomadog mpaka makubwa kulingana na utakavyo elekezwa na mwalimu wako wa mazoezi.
  6. Penda kuzingatia mdaa wako vizuri - jua kua mda nikitu muhimu sana kwa maisha ya mtu yeyote na hiyo ni hadi kwenye mazoezi. ukitaka kufanya mazoezi jaribu kujiwekea mdaa maalumu ambao utakuwezesha kupangilia mazoezi yako na wakati utakao fanya, na sio kufanya pale unapo jisikia ama kuacha unapo jisikia. Anza na maliza mazoezi kwa wakati sahihi


  7. Jua aina ya vyakula unavyo paswa kula na kwa kiasi gani unapaswa kula - mazoezi huenda sambamba na vyakula tunavyokula hvyo basi ni muhimu kulinganisha malengo yako sambamba na vyakula unvyokula. kwa mfano unataka kupungua basi huwezi kula vyakula vyo mtu anyetaka kuongezeka maana hutopata  matokeo unayotaka

About benson godfrey

benson godfrey
Recommended Posts × +

DIET YA KUTOA SUMU MWILINI NA KUPUNGUZA UNENE KWA HARAKA

Habari zenu wadau wa KUAFIT! leo tutaongelea kuhusiana na elimu ya lishe ambayo itahusiana na diet ambapo tutaelezea mambo mengi san...