latest Post

ELIMU KUJENGA MISULI NA KUPUNGUWA MWILI KWA PODA NA VIDONGE

Wanamazoezi wengi huniuliza "je! kuna faida ya kutumia vidonge na poda za kujenga miili?", swali hilo ni zuri sana hasa pale mtu anapo tamani kuona matokeo ya haraka hasa kwa wa beba vyuma na wanaotamani kupunguza uzito wa mwili na kuweka mwili sawa.
Kwanza kabisa ningependa ni wajuze watu kuwa inashahuriwa mtu kutumia vidonge(suppliments) endapo mtu atakuwa na upungufu wa vitamini au madini mengine, ambapo hutokana na mtu kuto kula lishe kamili yenye virutubisho vyote vinavyo hitajika na mwili.  Kutokanan na utafiti uliyofanyawa na mtaalamu wa lishe Benaedot et al unasema kuwa ni vyema sana mtu kupata virutubisho kama vitamini na madini kutoka kwenye vyakula vya kawaida na sio kupitia vidonge bali mtu akiwa na matatizo ya kiafya basi ndipo anapo shahuriwa kutumia vidonge

Kwa wale wanao tamani kujenga mwili au kupunguza kwa kutumia vidonge inabidi kujua kwamba wengi huambiwa kuwa vidonge hivyo husaidia kuchoma ama kufanaya mwili kutumia zaidi mafuta (FFAs-free fatty acids) haraka bila mazoezi mengi kuhitajika, bali kwa kiasi flani sio kweli. 

Watu ambao hawajaanza mazoezi na wantaka kutumia vidonge na poda za kusaidia mwili kutumia zaidi virutubisho  mna kumbushwa kuwa miili ya  watu wa dizaini hiyo kwa kawaida hutumia zaidi wanga(carbohydrate) na mafuta(FFAs) kwa wingi bila mazoezi , hvo basi vidonge hvyo havitakuwa na msaada maana mwili umeshazoea kuanya kitendo hiko na mwili hutokuwa na mabadiliko yoyote zaidi ya kuongezeka uzito.  

Watu ambao wanaofanya mazoezi na wantaka kutumia vidonge na poda za kusaidia kuchoma mafuta na kujenga misuli wanakumbushwa kuwa kutokana na utafiti wa Cole vidonge na poda hizo huwa na insulini ambayo ni kimengenya cha wanga na huzuia mafuta(FFAs) kuchomwa mwilini. hivyo basi bado haitaleta matokeo yanayo hitajika mwilini.Hivyo mazoezi ndio jibu sahihi ya kupata matokeo yanayo hitajika.

Kwa wale wanao kula lishe iliyo kamili hawana haja ya kutumia vidonge na poda hizo maana hakuna utafiti wowote wa kisayansi unao kubaliana na swala la kutumia vidonge vya protien,misuli na hata poda vyake kuwa unaongeza ukubwa wa misuli.Bali kwa vidonge vilivyo fanyiwa utafiti kama vile creatine huonyesha matukio mazuri hasa kwa wau wanaofanya mazoezi kwa mda mrefu
Kama umeipenda andiko hili basi gonga NZURI  na  kwa maswali na maoni zaidi basi tuandikie baada ya andiko hili, na pia kama ungependa maandiko mengine kama haya basi jisajili kwa kuweka anuani yako juu kwenye linki ya KUJISAJILI.

About benson godfrey

benson godfrey
Recommended Posts × +

DIET YA KUTOA SUMU MWILINI NA KUPUNGUZA UNENE KWA HARAKA

Habari zenu wadau wa KUAFIT! leo tutaongelea kuhusiana na elimu ya lishe ambayo itahusiana na diet ambapo tutaelezea mambo mengi san...