latest Post

FAIDA YA MAZOEZI KWA WANAWAKE WAJAWAZITO

Nikweli kuwa wanawake wajawazito hupaswa kupewa matunzo na mda wakupumzika wakutosha, bali pia hupaswa kupata mda wakufanya mazoezi kwa faida yao na watoto wao tumboni.
Faida hizo ni

Kuongezeka kwa mzunguko wa damu mwilini 
kutokana na mazoezi basi utafiti unaonesha kua wanawake wajawazito wanaweza kupata mzunguko mzuri kwake na kwa mtoto tumboni. Kutokanan na hivyo basi humwakikishia mama kuwa mtoto atakua na afya njema kwa kua mzunguko wa hewa na damu utakua  mkubwa baina yao mwilini.


Kupungua kwa uzito kirahisi baada ya ujauzito
Kulingana na madaktari wa afya ni kwamba wanawake wajawazito wana hatihati kubwa kuongezeka kilo kumi(10) hadi ishirirni(20) pale wanpotoka kujifungua na hua ngumu kwao kupungua. Kutokana kwa utafiti huo basi imewalazimu madaktari kuwashaahuri wanawake wajawazito kufanya mazoezi marar kwa mara kabla kujifungua

Urahisi kwenye kujifungua
wanawake wajawazito wanao fanya mazoezi hua kwa kiasi kikubwa wanauwezekano mkubwa kujifungua salama bila matatizo yoyote kutokana na kwamba misuli yao katika njia zao za uzazi kua na nguvu hivyo kutokuchukua mda mrefu kujifungua

Kupunguza kuvimba kwa miguu
Wanawake wajawazito wengi husumbuliwa mara kwa mara na kuvimba kwa miguu. Hali hii husababishwa hassa na kukaa pahali pamoja kwa mda mrefu, lakini kwa kufanya mazoezi  hupunguza uwezekano wa kuvimba migu.

Hupunguza  kichefuchefu cha mara kwa mara
utafiti unaonesha kua kwa kufanya mazoezi hupunguza adha za kichefu chefu cha mara kwa mara kutokana na mwili kua mchangamfu na akili huwekwa sawa

Urahisi wa kurudi katika hali ya kawaida baada ya kujifungu
Nirahisi sana kwa wanawake wajawazito kurudi katika hali zao za kawaida bila kuchukua mda mrefu katika kipindi cha uzazi kama watazingatia mazoezi kipindi cha ujauzito wao

Kulala vizuri 
Wanawake wajawazito wanuwezo mkubwa wakulala vizuri kama wanafanya mazoezi mara kwa mara , hio hupunguza msongamano wa mawazo na mwili kua katika hali nzuri.

Kupunguza uwezekano wa magonjwa madogo_madogo
Wajawazito wengi wano fanya mazoezi wanauwezekano mkubwa kuto kupata magonjwa kama vile mafua na homa kutokana na mwili kujenga kinga kubwa mbali na magonjwa

About Kuafit

Kuafit
Recommended Posts × +

0 comments:

KUPUNGUZA UZITO KWA MAJI YA BARIDI

Watu wengi katika jamii hupendelea kuoga na maji ya moto katika majira yote ya hewa lakini kutokana na utafiti uliofanywa na wanasayansi kam...