latest Post

VIGEZO VYA KUPATA MATOKEO YA HARAKA KWA WABEBA VYUMA
Watu wengi hupenda kuwa na muonekano mzuri kwa kujenga miilii yao, na hasa kwa wanaume na wanawake wenye kutaka kuonekana na mvuto kwa jinsia ya pili. Mara nyingi kujenga huko kwa mwili huwa kwa namna mbili eidha kwa kupungua ama kwa kuongezeka, ambapo kwenye kuongezeka wengi hupendelea kunyanyua vyuma vizito.

Kujenga mwili ni jambo lenye changamoto nyingi, ambazo zinaeza kupelekea kukata tamaa hasa pale unaposhindwa kupata matokeo ya haraka uliyotazamia. Kujenga mwili kwa vyuma kunahitaji maarifa mbalimbali ya mazoezi ambayo yatakayo tumika kukuhakikishia kwamba matokeo unayoyatazamia yanawezekana kupatikana kwa wakati. Ingawa vyakula ni muhimu katika mazoezi lakini sitogusia, bali nitaongelea elimu ya mazoezi ambayo ni muhimu kuifahamu.
Maarifa haya yamegawanyika kwa vipengele vitatu ambavyo ni kama ifwatavyo;


  • Jinsia 
Jinsia ni moja wapo ya vigezo na elimu muhimu katika ufanyaji wa mazoezi hasa yanayohusiana na unyanyujai wa vyuma vizito. Wanaume wametofautiana na wanawake na wana uhakika wa matokea ya haraka wakibeba vyuma, kutokana kwa kigezo kuwa wanaume wana homoni nyingi ya testosteron ambayo inauwezo wa kusababisha utumikaji wa protien kuwa mkubwa.  Hvyo basi kuwa na misuli mikubwa kwa wanaume hua ni haraka ukilinganisha na mwanamke

  • Maumbile(genetic)
Kwa mbeba vyuma yeyote anapaswa kujua maumbile kwa vigezo kwamba anaweza akawa mwenye misuli ya twitch fiber yenye speed ama mwenye misuli ya twitch fiber iliyo taratibu. Kwa wale wenye twitch fiber yenye speed ina maanisha ya kwamba anaweza kupata matokeo ya haraka kwa kupata misuli mikubwa ukilinganisha na mtu mwenye misuli ya twitch yenye speed ndogo. Utafiti huo ulifanyika uwingereza mwaka 2002  ambapo wakufunzi wa mazoezi walipopata malalamiko kutoka kwa wanafunzi wao wa mazoezi.


  • Ufanyaji wa mazoezi
Ufanyaji wa mazoezi ni moja wapo ya elimu inayompasa mbeba vyuma kuipata ambapo hua ina umuhimu kama kigezo kikuu cha kupata matokeo. Mazoezi ufanywa kulingana na matakwa ya mtu husika, ambapo kuna wale wanaopenda kujaza miili na kuwa na mwili mkubwa bali wengine wastani. Wale wanautaka miili mikubwa wanapaswa kufanya mazoezi mengi kwa marudio mengi kwa zoezi moja( many reps for each set), wakati wenye kutaka miili ya wastani wanabidi wafanye marudio machache kwa zoezi moja( small reps for each set).

Kwa kuyatambua hayo basi inampasa mwanamazoezi yeyote anyayebeba vyuma kuwa na elimu hiyo na kuifanyia kazi ili kupata matokeo ya haraka.
Kama umeipenda andiko hili basi gonga NZURI  na  kwa maswali na maoni zaidi basi tuandikie baada ya andiko hili, na pia kama ungependa maandiko mengine kama haya basi jisajili kwa kuweka anuani yako juu kwenye linki ya KUJISAJILI

About benson godfrey

benson godfrey
Recommended Posts × +

DIET YA KUTOA SUMU MWILINI NA KUPUNGUZA UNENE KWA HARAKA

Habari zenu wadau wa KUAFIT! leo tutaongelea kuhusiana na elimu ya lishe ambayo itahusiana na diet ambapo tutaelezea mambo mengi san...