latest Post

MAZOEZI 6 MUHIMU KUFANYIKA KWA ASUBUHI



  Kuna aina mbalimbali ya mazoezi ambayo unaweza kufanya kila siku kutokana na uhitaji wako au malengo uliyojiwekea.Ufanyaji wa mazoezi kabla hujaanza kufanya shughuli zako za kila siku huwa na faida kubwa sana katika kukuandaa kukabiliana na majukumu yako ya siku nzima na pia husaidia kuandaa  akili yako kuwa katika hali nzuri.lakini tunafahamu wengi wanaamka asubuhi sana kuwai kazini ili kujiepusha na foleni za barabani au kazi zao zinawazalimisha wafike mapema ofisini hivyo kukosa muda mzuri wa kufanya mazoezi asubuhi.Leo tunakuletea mazoezi 7 marahisi ambayo unaweza kufanya ndani ya dakika 15 dakika tu unapoamka asubuhi hapo hapo nyumbani kwako, mazoezi haya hayahitaji vifaa wala hayakuhitaji uwe katika sehemu ya mazoezi(Gym).Ndani ya dakika 15 tu unaweza fanya mazoezi haya na kufanya siku yako kuwa njema zaidi kimwili na kiakili pia.
Mazoezi haya husisha viungo vingi vya mwili kwa kila zoezi moja(codinative) ambapo huwa ni mazoezi sahihi ya kufanya kwa mtu mwenye pilika nyingi za maisha kama kwenda kazini maana hayachukui mda mrefu kuyafanya

1. Single-Leg Glute Bridge


  • Zoezi hili ni kati ya mazoezi mazuri ambapo husaidia kunyoosha mgongo wa chini  na pia husaidia kujenga misuli ya makalio na hata pia hamstring.
  • Zoezi hili hufanywa kwa kulala kwenye mattress na kukunja mguu mmoja wakati mguu mwingine ukiwa umenyooka,  kiuno hupaswa kunyanyuka kutoka chini na kushuka .

2. Mountain climber


  • Zoezi hili husadia kujenga misuli ya tumbo la ndani itwayo( inner oblique) na pia hukaza misuli ya nje(tricep) na ndani(bicep) ya mkono.
  • zoezi hili hufanywa kwa kuweka mikono yote chini na kisha kukunja na kunyoosha miguu kuelekea mbele na kwa kupishana.

3.Leg raise

                               
                                           

  • Hili ni zoezi zuri la tumbo la chini ambalo hukaza sana misuli ya tumbo la chini iliyolegea
  • Zoezi hili hufanywa kwa kulala kwenye mattress na kunyoosha mikono mbele huku miguu ikiwa imenyooka, miguu hupaswa kunyanyuka juu pamoja na kushuka bila kugusa chini.  


4. Pop Squat

  • Zoezi hili ni aina moja wapo ya squat ambayo hugusa misuli ya ndani ya mapaja(glut) na hamstring.
  • Zoezi hili hufanywa kwa kutanua miguu na kushuka squat na kisha kurudisha katikati kwa kuruka huku mikono ikiwa pamoja.


5. Static Lunge leg kick


  • Lunges leg kick ni zoezi muhimu sana kwa miguu kwa kuwa hulenga sehemu ya mapaja(paja la mbele) na makalio.
  • Zoezi hili hufanywa kwa kupeleka mguu mmoja mbele na mwingine nyuma huku mgongo ukiwa umenyooka, mtu hupaswa kushuka chini na kunyanyuka na teke lililo nyooka.

6. Hand tap Push-Up




  • Hii ni aina moja wapo ya push-up amabayo hujenga kifua kwa kukikata katikati na pia hujenga misuli ya mikono
  • Zoezi hili hufanywa kwa kushuka push-up ya kawaida na kisha mkono mmoja kugusa mwingine baada ya kushuka chini na kuanda juu.
Kumbuka si lazima ufanye mazoezi yote 6 chagua ambayo unayoweza anza nayo kila zoezi jaribu kulifanya ndani ya dakika 2 na nusu.Ukifanikiwa kufanya mazoezi haya utauweka mwili na akili yako katika hali nzuri na kukusaidia kufanya kazi zako kwa ufanisi zaidi

Kama umeipenda andiko hili basi gonga NZURI  na  kwa maswali au maoni zaidi basi tuandikie baada ya andiko hili, na pia kama ungependa kusoma andiko jengine kama hili basi jisajili kwa kuweka anuani yako  kwenye linki ya SUBSCRIBE.


Pia waweza tuandikia kwa email yetu Kuafit08@gmail.com 


Kwa number yetu ya Tigo +255 653 009 477  


Instagram account yetu  (KUAFITI), Facebook-(kuafit) na twitter-(kuafit)

About Kuafit

Kuafit
Recommended Posts × +

0 comments:

KUPUNGUZA UZITO KWA MAJI YA BARIDI

Watu wengi katika jamii hupendelea kuoga na maji ya moto katika majira yote ya hewa lakini kutokana na utafiti uliofanywa na wanasayansi kam...