latest Post

FAIDA ZA PAPAI KWA AFYA YAKO


Tunaambiwa kuishi vizuri ni pamoja  na kula chakula bora na sahihi.Matunda ni sehemu ya chakula ambacho kina umuhimu mkubwa sana katika kuboresha afya zetu. Jamii zetu za kiafrica zimebarikiwa kuwa na ardhi yenye rutuba ambayo husaidia kuzalisha matunda aina mbalimbali katika misimu tofauti.Matunda haya yanaumuhimu mkubwa sana katika afya zetu, Watu wengi wanafahamu umuhimu wa matunda lakini si wote wanachokulia kwa umakini(kuweka katika vitendo).Ulaji wa matunda huleta faida nyingi sana katika afya zetu na ni muhimu kila mtu kula matunda mara kwa mara.Leo nataka ufahamu faida za kiafya zinazoletwa kutokana ulaji wa tunda la Papai.


1.Kurutubisha kinga ya mwili.

Vitamin C and vitamin A ambayo inapatikana mwilini kutokana na kupata virutumbisho vilivyopo kwenye matunda,husaidia kuimarisha mfumo wa kinga mwilini dhidi ya magonjwa mbalimbali yanayojirudia kama vile kikohozi,mafua.Tunda aina ya papai huchanglia mwili kupata vitamini A na vitamini C ili kuukinga mwili na magonjwa mbalimbali.

2.kuimarisha mfumo usagaji chakula mwilini. 

Papai huboresha mfumo mzima wa usagaji wa chakula mwilini na kumfanya mtu kupata choo laini na hivyo kujiepusha na madhara yatokanayo na kukosa choo kwa muda mrefu mbayo humweka mtu katika hatari ya kupata kansa ya tumbo.


3.Kinga  dhidi ya vidonda.

Watu mbalimbali ambao wanasumbuliwa na mauvimbe/vidonda yasiyo ya kawaida mara kwa mara,jambo hili husababishwa na kutokuwa na virutumbisho muhimu ambayo hupatikana katika tunda la papai.Watu wanaosumbuliwa na matatizo haya wanashauriwa kula tunda hili  ili kupata virutumbisho vyake vinavyosaidia uponyaji wa uvimbe au vidonda.

4.kupunguza uzito wa mwili.

Tunda hili husaidia kupunguza uzito wa mwili, papai lina fiba (nyuzi lishe) ambazo husaidia kupunguza uzito, unapokula tunda hili, fiba husababisha kujisikia umeshiba kwa hiyo mtu hupunguza kiasi cha chakula chenye nishati nyingi ambapo hupelekea kupunguza uzito wa mwili.

5.Kuimarisha Nuru ya Macho. 

Tunafahamu tunda aina ya karoti husaidi kuimarisha nuru au afya  ya macho yetu,papai nalo ni moja kati ya matunda ambayo yanasadia kuimarisha afya ya macho yako.Watu wanaotumia tunda hili la papai hujipa kinga madhubuti ya macho yao na kusadia macho yao kuwa imara muda wote.


6.kujiepusha na magonjwa ya Moyo.

Ingawa papai wakati wa kulila ni  tamu, lakini lina kiwango kidogo cha sukari  .Papai ni zuri kwa wale wenye matatizo ya kisukari kwa kuwa lina  vitamini na virutubisho ambavyo huwakinga wenye kisukari wasipate magonjwa ya moyo. Pia wasio na kisukari ni vyema kula papai ili kuweza kujiepusha na maradhi hayo.

7.Kutibu Mapafu.

Moshi wa sigara umeleta madhara makubwa sana wa wavutaji wenyewe pamoja na watu ambayo wameathirika na moshi huu wa sigara katika mazingira mbalimbali. Madhara haya hutokea katika katika mapafu yao, watu walioathirika wanashauriwa kula tunda hili la papai kwani husaidia kuongeza vitamini A ambayo usaidia kukuepusha na madhara yatokanayo na moshi wa sigara.(Kumbuka uvutaji wa sigara ni hatari kwa afya yako).

8.Kuondoa sumu mwilini.

Tunda la papai lililowiva lina kiwango kikubwa cha Vitamini C (62mg) ukilinganisha na chungwa lenye kiwango cha 53mg katika gramu 100 za tunda. Tafiti zimeonyesha faida nyingi za vitamini C ni kuondoa sumu mwilini(sumu hizi hujulikana kama free radicals).


Faida nyinginezo mbali na tulizoziona awali za ulaji wa papai ni pamoja kuondoa msongo wa mawazo, kusaidia kupunguza maumivu ya hedhi, kupunguza hatari ya kupata pumu na husaidia ngozi au majeraha kupona haraka.Hivyo inashauriwa kula tunda hili la papai mara kwa mara ili kupata virutumbisho mbalimbali ambavyo vitaleta matokeo chanya katika afya yako.Pia katika ulaji wa tunda hili usafi ni kitu cha muhimu sana hakikisha mazingira yako yapo katika hali safi na salama ili kuepusha kupata magonjwa mbalimbali.Kumbuka kuosha mikono na tunda kabla hujaaza kulila. 

Kama umeipenda andiko hili basi gonga NZURI  na  kwa maswali au maoni zaidi basi tuandikie baada ya andiko hili, na pia kama ungependa kusoma andiko jengine kama hili basi jisajili kwa kuweka anuani yako  kwenye linki ya SUBSCRIBE.


Pia waweza tuandikia kwa email yetu Kuafit08@gmail.com 


Kwa number yetu ya Tigo +255 653 009 477  


Instagram account yetu  (KUAFITI), Facebook-(kuafit) na twitter-(kuafit)

About Davis David

Davis David
Recommended Posts × +

DIET YA KUTOA SUMU MWILINI NA KUPUNGUZA UNENE KWA HARAKA

Habari zenu wadau wa KUAFIT! leo tutaongelea kuhusiana na elimu ya lishe ambayo itahusiana na diet ambapo tutaelezea mambo mengi san...