latest Post

JE UNA MALENGO JUU YA AFYA YAKO MWAKA HUU 2018?kwanza kabisa  nikupe hongera kwa kuvuka mwaka 2017 na kuingia mwaka 2018,tuzidi kumshukuru Mungu kwa hii neema aliyotupa.kila  mwaka unapoanza wengi wetu huwa tunamalengo mengi ya kufanya malengo ya kifedha, biashara elimu,ndoa au mahusiano,kifamilia na malengo mengine mengi tu.Dhumuni la malengo  haya ni kuakikisha mtu anatoka hatua moja na kufikia hatua nyingine katika nyanja mbalimbali za kimaisha.Je umeandaa malengo yako ya kiafya.Ni vyema ukatambua kuwa usipozingatia afya yako mapema inaweza ikaleta shida kutimiza malengo yako mengine uliyopanga.kumbuka afya yako ndio maisha yako, uwezi endesha biashara yako kama unaumwa, uwezi fanya kazi zako kikamilifu kama mwili wako upo katika hali dhaifu na mengineyo mengi.Haya mambo huwa  yanategemea sana afya yako ikiwa imara mambo mengine utafanya kwa ufasaha sana na kupata faida katika shughuli zako.Hivyo ni muhimu tunapoanza mwaka huu 2018 katika malengo yetu ambayo tunaipa kipaumbele tukumbuke kuweka malengo yako ya kiafya pia.

Leo nitakupa dondoo ambazo zitakusaidia kuweka malengo yako ya kiafya  kwa ufasaha ili mwaka huu wa 2018 uwe na manufaa kwako.
1.TAMBUA KUSUDI LAKO LA KUWA NA MALENGO YA AFYA YAKO (know your why).

Kila unalopanga lazima liwe na sababu, kama vile unapoamua kupanga malengo yako ya kibiashara dhumuni kubwa ni kukua kiuchumi au unapokuwa na malengo ya kusoma zaidi dhumuni kubwa inaweza kuwa ni kupandishwa cheo ofisini kwako au kuongezwa mshahara pia unapokuwa na malengo ya kuwekeza mwishoni unataka upate faida zaidi.Hivyo hivyo katika afya yako lazima uwe na kusudi unalotaka kulitimiza.makusudi yanaweza yakatofautiana kati ya mtu na mtu, mwingine kusudi lake ni kupunguza unene au kupunguza mafuta mwilini au kuwa na shape nzuri au kukuza kifua chake.hakikisha unajua kusudi lako ni nini unapoweka malengo yako ya kiafya.

2.ANDIKA MALENGO YAKO

Kuna msemo unasema "watu ambao wanaandika malengo yao huwa na asilimia kubwa ya kuyatimiza".hakikisha unaandika malengo yako katika daftari(notebook) na malengo yako yanaweza yakawa ni ya muda mrefu hivyo ni vyema ukayagawa na kuwa malengo ya muda mfupi.Mfano kama una malengo ya kupiga push 240 mpaka mwaka unaisha anza na push 20 kila mwezi na unaongeza push 20 kila mwezi unaofuata.Hivyo hivyo hata katika lishe yako uwezi ukaacha mara moja kula vyakula ambayo vilikuwa  vinaleta madhara katika mwili wako anza taratibu kwa siku,kwa wiki kwa mwezi mpaka hapo utakapoacha kabisa.Pia kwa upande wa mazoezi kama ulikuwa na mpango wa kufanya mazoezi ndani ya lisaa limoja anza taratibu kwa dakika 20 alafu unaongeza muda wa mazoezi kila baada ya muda fulani(kila baada ya wiki mbili).

3.ANZA TARATIBU

  kama ilivyoelezwa hapo awali kwamba inampasa mtu asianze mazoezi au kubadilisha lishe yake kwa haraka sana,mfano unapoanza mazoezi kwa kasi sana unasababisha maumivu katika mwili wako badala ya kuujenga.Anza taratibu au weka mipaka baada ya kila mwezi unaongeza kiwango chako cha mazoezi.Kuna msemo unasema tabia ni kama ngozi,katika swala la lishe inaweza ikawa kwako ni ngumu sana kuacha chakula fulani ambacho kinaleta madhara katika mwili wako.Hivyo uwezi ukaacha mara moja, njia rahisi ni kupunguza kula hicho chakula kila muda unapozidi ongenzeka, mfano kama ulikuwa unakula chakula icho mara 5 kwa wiki unaweza ukaamaua kupunguza kula kila wiki inapoongezeka.Pia kama kuna vyakula vinavyoboresha afya yako lakini unakuwa na ugumu wakati wa kula,anza taratibu kula mara moja wiki ya kwanza ,mara mbili wiki ya pili endelea Hivyo hivyo mpaka utaanza kuzoea.

4.PANGILIA ULAJI WAKO

Unapokuwa huna mpangilio mzuri katika ulaji wako, hata mazoezi yako hayatakuwa na faida yoyote katika mwili wako.Mfano kama una malengo ya kupunguza mafuta mwilini na unafanya mazoezi ya kupunguza mafuta mwilini lakini bado unakula vyakula vinavyoongeza mafuta mwilini hapo utakuwa unapoteza muda wako.Hivyo ni ushari wangu kuwa mwaka huu utakuwa na utaratibu mzuri katika ulaji wako.Yakupasa kuwa na msimamo si kila chakula kinachokuwepo mbele yako ni cha kukila tu.Kumbuka vyakula vingine huwa na radha nzuri sana kinapokuwa mdomoni lakini kina madhara makubwa katika mwili wako.

5.PANGA RATIBA YAKO

Hapa uwa tunatofautiana sana kutokana na shughuli zetu za kila siku,hivyo ni vyema ukaweka muda wako ambao utakusaidia kufanya mazoezi yako kwa ufasaha pasipo kuharibu ratiba zako zingine mfano kazini,familia au biashara.Si lazima ufanye mazoezi kila siku unaweza ukachagua siku chache katika wiki ambazo utatenga muda wako wa kufanya mazoezi kwa ufasaha.


6.PIMA AFYA YAKO.

Hili ni jambo muhimu sana, upimaji wa afya yako utakusadia kujua hali yako ya kiafya ikoje pia itakusadia kujua ni vyakula gani unatakiwa ule na vyakula gani unatakiwa usile.katika swala zima la mazoezi upimaji wa afya utakusaidia kujua mazoezi gani uatakiwa kufanya na mazoezi gani utakiwi kufanya,kumbuka si kila aina ya zoezi unafaa kulifanya hii huwa inategemea na hali ya afya yako na kusudi lako unalotaka kulitimiza kama nilivyoeleza kwenye kipengele cha kwanza.
7.ANZA SASA

Anza kufanya mabadiliko hayo sasa. Usisubiri mwezi ujao au hata Jumatatu ijayo. Anza sasa hivi.Chukua  daftari na anza kuandika malengo yako mapya katika kipengele cha afya kisha kuchukua hatua.Unapochukua hatua mapema ndiyo utakavyoanza kuweka malengo yako katika vitendo na baada ya muda kuaanza kuona mabadiliko chanya katika mwili wako.


Ni matumaini yetu dondoo hizi zitakuwa msaada kwako katika afya yako unapoanza mwaka huu mpya.Tegemea vitu vingi vizuri kutoka KUAFIT

Kama umeipenda andiko hili basi gonga NZURI  na  kwa maswali au maoni zaidi basi tuandikie baada ya andiko hili, na pia kama ungependa kusoma andiko jengine kama hili basi jisajili kwa kuweka anuani yako  kwenye linki ya SUBSCRIBE.
Pia waweza tuandikia kwa email yetu Kuafit08@gmail.com 


Kwa number yetu ya Tigo +255 653 009 477  


Instagram account yetu  (KUAFITI), Facebook-(kuafit) na twitter-(kuafit)

About Davis David

Davis David
Recommended Posts × +

DIET YA KUTOA SUMU MWILINI NA KUPUNGUZA UNENE KWA HARAKA

Habari zenu wadau wa KUAFIT! leo tutaongelea kuhusiana na elimu ya lishe ambayo itahusiana na diet ambapo tutaelezea mambo mengi san...