latest Post

FAIDA YA TANGAWIZI KWA MTU MWENYE KISUKARI


    Tangawizi ni kati ya mitishamba maarufu katika jamii zetu na hutumika na watu kwa matumizi mbalimbali kama kuondoa kichefuchefu na hata pia kutatua matatizo ya tumbo kusokota na husaidia kuongeza nakshi na ladha katika vyakula vyetu.
 Ni kweli kwamba kwa kunywa kikombe kimoja cha chai yanye tangawizi ama kula chakula chenye tangawizi yaweza kuleta manufaa mengi katika mwili wa mtu na hasa huleta manu faa zaidi kwa mtu mwenye kisukari.
Kutokana na utafiti usio rasmi uliofanyika mwaka 2015 na taarifa iliyotolewa na jarida la complimentary and integrative  medicine, inaonyesha yakwmba watu wenye kisukari aina ya pili(type 2) miili yao inaweza kuweka sawa kiwango cha sukari mwilini ndani ya miezi mitatu kwa kutumia tangawizi na bila kutumia dawa ama sindano ya insulin. Utafiti huo pia unaeleza zaidi ya kwamba tangawizi ni moja wapo ya miti shamba ambayo huadhiri kemikali ya mwili(enzyme)  ambayo uhusiana na mmengenyo wa chakula aina ya wanga kwa kuongeza kiwanga cha utumikaji wake mwilini, na hivyo basi husaidia kupunguza uwezekano wa kupata matatizo mengineyo ambayo hutokana na kisukari kama tatizo la presha.

  • Adhari za kutumia tangawizi kwa mtu mwenye anina ya pili ya kisukari(type 2) endapo anatumia dawa za kisukari

    Endapo mtu mwenye kisukari(type 2) atatumia tangawizi kwenye lishe yake huku akiwa anatumia dawa alizo pewa na daktari, basi mtu huyo anauwezekano mkubwa wa kupata tatizo la kushuka kwa kiwango cha sukari mwilini. Kulingana na maelezo yaliyotolewa hapo awali kutokana uwezo wa tangawizi kuadhiri uwezo wa kemikali (enzymes) zinazo uhusiana na mmengenyo wa wanga basi ni dhairi ya kwamba kwa mtu mwenye kisukari kuchanganya dawa na tangawizi kunaweza kufanya mwili wa mtu huyo kutumia sukari yake ya mwili kwa kiwango kikubwa  na hivyo kusababisha tatizo hilo.
   Utafiti pia unaonyesha tangawizi haiadhiri tu watu wenye kutumia dawa za kisukari bali pia watu wenye kutumia dawa za presha na matatizo yanayohusiana na moyo.

  • Angalizo juu ya matumizi ya tangawizi kwenye mlo wa kawaida

  Tangawizi iliyopo kwenye mfumo wa vidonge yaweza kutumika na mtu mwenye kisukari endapo ataruhusiwa na daktari wake. Kwa wale watu wenye kisukari wenye kutaka kuweka tangawizi kwenye mlo wao wa kawaida kama kwenye vyakula na vinyawaji kama chai, wanashauriwa kwamba watumie tangawizi iliyopo kwenye mfumo wa poda ambayo makali yake sio kama ya tangawizi iliyopo kwenye mfumo wa vidonge ama katika uhalisia wa mmea wake.
Inashauriwa kwamba mtu mwenye kisukari awe mwangalifu endapo atataka kutumia vinywaji baridi vilivyo na tangawizi kama vili soda, juisi na hata bia kutokana na kwmba vinyawaji hivyo vina kiwango kikubwa cha sukari na hivyo basi kutokuleta tija inayohitajikaa mwilini.

Ushauri
Ni vyema kuonana na daktari kabla ya kutaka kufanya mabadiliko yoyote katika utaratibu wako wa kula  kama ni mgonjwa wa kisukari na unatumia dawa

Kama umelipenda andiko hili basi gonga NZURI  na  kwa maswali au maoni zaidi basi tuandikie baada ya andiko hili, na pia kama ungependa kusoma andiko jengine kama hili basi jisajili kwa kuweka anuani yako  kwenye linki ya SUBSCRIBE.


Pia waweza tuandikia kwa email yetu Kuafit08@gmail.com 


Kwa number yetu ya Tigo +255 653 009 477  


Instagram account yetu  (KUAFITI), Facebook-(kuafit) na twitter-(kuafit

About Kuafit

Kuafit
Recommended Posts × +

0 comments:

KUPUNGUZA UZITO KWA MAJI YA BARIDI

Watu wengi katika jamii hupendelea kuoga na maji ya moto katika majira yote ya hewa lakini kutokana na utafiti uliofanywa na wanasayansi kam...