latest Post

FIAIDA 4 ZA KIAFYA ZA KUFANYA MAZOEZI YA KUKIMBIA


Kwenye jamii zetu nyingi watu hupendelea sana kufanya mazoezi ambayo yanayowaezesha kutunza afya zao, na kati ya mazoezi ambayo ni maarufu, yanayopendwa na yenye tija kwa rika mbalimbali ni mazoezi ya kukimbia.
Mazoezi ya kukimbia ni kati ya mazoezi ya (aerobic) ambapo hufanywa na watu wengi sana duniani, na hata pengine hufanywa kama sehemu ya michezo ya kijamii kama vile (marathon) na pengine hata kama njia ya kukusanya watu ilikuchangisha kwaajili ya kuwezesha miradi ya kijamii.

Watu wengi huwa na sababu mbalimbali za kukimbia huku kikubwa wanacho kitazamia ni kuhimarisha afya zao. Japo kuwa zoezi la kukimbia linaweza lisipendwe sana bali kwa kujua faida zake kunamfanya mtu ajue umuhimu wake, na kwa kujua umuhimu wa mazoezi ya kukimbia basi ni rahis mtu kuweka malengo yake juu ya kile atakacho kitaka.


1. Kinga dhidi ya magonjwa

 Utafiti unaonyesha  kwamba zoezi la kukimbia humsaidia mtu kupunguza uwezekano wa kupata magonjwa kama vile mshtuko, kisukari na presha ya kushuka. Kwa kufanya zoezi la kukimbia mtu huimarisha kinga ya mwili wake na pia hufanyisha mazoezi misuli ya moyo na mirija yake na hivyo basi kupunguza uwezekano wa maradhi ya moyo

2. Kupunguza uzito na unene
  

 Swala la kupunguza unene wa mwili ni kati ya maswala ambayo huwatesa sana watu na mda mwingine hupelekea mtu kuchukua atua kama vile opareshen ya kuto mafuta(contouring). Kutokana na utafiti unaonyesha kuwa zoezi la kukimbia ni kati za mazoezi yanayopunguza sana unene na kumfanya mtu kuwa na mwili mzuri wa mazoezi, basi inashauriwa mtu kufanya zoezi hili angalau mara tatu kwa wiki.

3. Kupnguza msongo wa mawazo

 Kutokana na pilikapilika za kila siku za maisha msongo wa mawazo ni kitu cha kawaida kumpata mtu yeyote. Utafiti unaonyesha yakwamba  kwa kufanya zoezi la kukimbia mtu anaweza kuufanya mwili wake kuweza kuzalisha homoni zenye tija na hivyo kutumia nguvu nyingi ambapo hupunguza uwezekano wa msongo wa mawazo.

4. Uhumarishaji wa mifupa na misuli

 Zoezi la kukimbia husaidia mwili sana hasa kwenye ukazaji na uhimarishaji wa mifupa na misuli. Kulingana na utafiti uliofanywa Dr brok unaonyesha ya kwamba mtu anavyozidi kukimbia na umri wake unavyozidi kuongezeka ndivyo anavyo himarika zaidi kwenye misuli na mifupa yake.

Kumbuka kabla ya kutaka kufanya mazoezi ya kukimbia ni vyema mtu kumwona daktari kwa ushauri  na vipimo vya afya yake. Mtu anayetaka kufanya mazoezi ya kukimbia analazimika kutafuta nguo nyepesi kama bukta ama traksuti  na pia kutafuta viatu vyepesi vya kukimbilia mfano raba.

Kama umeipenda andiko hili basi gonga NZURI  na  kwa maswali au maoni zaidi basi tuandikie baada ya andiko hili, na pia kama ungependa kusoma andiko jengine kama hili basi jisajili kwa kuweka anuani yako  kwenye linki ya SUBSCRIBE.


Pia waweza tuandikia kwa email yetu Kuafit08@gmail.com 


Kwa number yetu ya Tigo +255 653 009 477  


Instagram account yetu  (KUAFITI), Facebook-(kuafit) na twitter-(kuafit)




About Kuafit

Kuafit
Recommended Posts × +

0 comments:

KUPUNGUZA UZITO KWA MAJI YA BARIDI

Watu wengi katika jamii hupendelea kuoga na maji ya moto katika majira yote ya hewa lakini kutokana na utafiti uliofanywa na wanasayansi kam...