latest Post

MAZOEZI 5 YA KUKAZA MISULI YA MIKONO ILIYOLEGEA


 Mikono yenye unene wa kupitiliza kwa mara nyingi huwa ni tatizo kubwa sana hasa ukizingatia ya kwamba hupoteza uasilia wa mwonekano wa mtu.  Watu wengi hudhani tatizo hili hukumba wanawake zaidi kuliko wanaume bali sio kweli, na ni kweli yakwamba wote huathirika kutokana na tatizo hili.
Sababu ya mikono kuwa minene kupitiliza ni kutokana na mtu kula vyakula vingi vyenye mafuta na wanga mwingi bila ya mwili kufanyia kazi chakula hiko. Vyakula hivyo visivyofanyiwa kazi hulazimika kuhifadhiwa na mwili kwaajili  ya matumizi ya badae endapo mwili ukihitaji nguvu ya ziada.
Utafiti unaonyesha yakwamba watu wenye uwezekano mkubwa wakuwa na tatizo la mikono yenye unene wa kupitiliza ni watu wenye umri zaidi ya miaka 30. Kutokana na kwamba ili mtu akuwe lazima ahitaji kula sana na ukuaji kwa kawaida hufanyika kwanzia wadogo hadi umri wa miaka 25 na ndipo mwili huachana na swala la ukuaji, basi ni rahisi mwili kuhifadhi chakula kingi baada ya miaka 26 na ndipo matokeo yake huonekana akiwa 30 na kuendelea.
Pia watu hupata tatizo la kuwa na mikono minene  kutokana na kuto kushughulisha zaidi mwili na hivyo mwili kutokuwa na haja ya kutumia chakula chake kwa lolote, na hivyo basi hulazimika kuhifadhi zaidi chakula kwa matumizi ya badae.

Kutoa mafuta yaliyo hifadhiwa mikononi kwa mara nyingi huwa ni kazi zaidi ukilinganisha na kutoa mafuta yaliyo hifadhiwa sehemu nyingine ya mwili, kutokana na changamoto hiyo basi jitihada na mazoezi uhitajika.
Hivyo basi tutaangalia mazoezi ambayo yanayoweza kuleta mabadiliko ya haraka na kumwezesha mtu kupunguza miko iliyozidi unene.

  1Dumbells bicep curl

  Hili zoezi ni kati ya mazoezi ya (spot training) ambapo hulenga msuli moja tu, zoezi hili helenga msuli wa ndani wa mkono(bicep) na hufanywa kwa kuzingatia yafwatayo;

  • Mtu anapaswa kusimama akiwa ametanua mikono na miguu usawa wa mabega.
  • Mtu anapaswa kushikilia uzito(dumbells) kwa kila mkono na kunyoosha mikono kuelekea chini huku viganja vikielekea mbele.
  • Sasa mtu anapaswa kukunja mikono yote miwili  kuelekea kwenye mabega na kukunjua kwa kunyoosha kuelekea chini.
  • zoezi hili linapaswa kufanywa kwa angalu hesabu ya 10 mara 3 jumla 30 na kuendelea.
 2. Tricep dumbell kickback

  Zoezi hili pia ni kati ya mazoezi ya (spot training) ambapo hulenga msuli mmoja kwa zoezi. zoezi hili hulenga msuli wa nje wa mkono(tricep) na mtu anweza kufanya kwa kuzingatia yafwtayo;
  • Mtu anapaswa kukunja kidogo miguu yote wakati ikiwa imewekwa pamoja na kisha mikono ikiwa imeshikilia uzito(dumbell), 
  • Kunja mikono ikiwa imeshikilia uzito karibia na usawa wa kifua huku viwiko vikiwa vimekaa sehemu moja bila kulega, nyoosha mikono kuelekea nyuma mpaka unyooke uswa wa mgongo na kisha kunja mkono na rudisha hadi uswa wa kifua.
  • Fanya zoezi hili kwa hesabu ya 10 kila mkono mara 2 kwa jumla ya 40 na ikiwezekana fanya zaidi.
 3. Pushups

  Zoezi hili ni kati ya mazoezi ambayo ni maarufu na yenye kuhusisha mwili mzima na pia huleta mabadiliko ya tija kwa mwili hasa kwenye kukaza misuli ya kifua na mikono. Mtu anyaetaka kufanya zoezi hili hupaswa kuzingatia yafwatayo;

  • Kwanza weka mikono chini sehemu iliyonyooka huku  ikiwa imetanuka kwa usawa wa mabega wakati miguu imekaa pamoja.
  • Hakikisha umenyoosha mgongo na kiuno na kisha kunja mikono huku ukikaribia kugusa chini bila kifua wala tumbo kugusa chini,  kunjua na nyoosha mikono tena na kisha rudia zoezi hili.
  • Fanya zoezi hili angalau kwa hesabu ya 10 mara 2 ikiwa jumla ya 20 ili kuweza kupata matokeo ya haraka zaidi. 

  4. Dips


   Hili ni moja wapo kati ya mazoezi mazuri ya kukaza msuli wa nje na pia zoezi hili halihitaji kutumia kifaa chochote, mtu akihitaji kufanya zoezi hili anahitaji kuzingatia yafwatayo;

  • Kalia kiti au benchi huku mikono ikiwa imenyooka na kushikilia mwanzo wa kiti au benchi karibu na usawa wa makalio.
  • nyoosha miguu mbele na peleka makalio mbele na kisha shusha kuelekea chini bila makalo kugusa chini huku ukiwa umekunja mikono na kisha nyoosha kujinyanyua juu.
  • Fanya zoezi hili kwa hesabu ya 10 mara 3. jumla ya 30.
  5. Counter pushups


 Zoezi hili ni kati ya mazoezi ambayo ni marahisi na yenye kuhusisha viungo vingi vya mwili  na pia huleta mabadiliko ya tija kwa mwili hasa kwenye kukaza misuli ya kifua pamoja na mikono. Mtu anyaetaka kufanya zoezi hili hupaswa kuzingatia yafwatayo;

  • Kwanza weka mikono sehemu ya juu iliyoinuka kama counter ama meza huku  ikiwa imetanuka kwa usawa wa mabega wakati miguu imekaa pamoja.
  • Hakikisha umenyoosha mgongo na kiuno na kisha kunja mikono huku ukikaribia kugusa pahali palipo inuka wakati miguu ikiwa imerudi futi mbili nyuma, bila kifua wala tumbo kugusa chini,  kunjua na nyoosha mikono tena na kisha rudia zoezi hili.
  • Fanya zoezi hili angalau kwa hesabu ya 10 mara 2 ikiwa jumla ya 20 ili kuweza kupata matokeo ya haraka zaidi. 

Kama umeipenda andiko hili basi gonga NZURI  na  kwa maswali au maoni zaidi basi tuandikie baada ya andiko hili, na pia kama ungependa kusoma andiko jengine kama hili basi jisajili kwa kuweka anuani yako  kwenye linki ya SUBSCRIBE.
Pia waweza tuandikia kwa email yetu Kuafit08@gmail.com 


Kwa number yetu ya Tigo +255 653 009 477  


Instagram account yetu  (KUAFITI), Facebook-(kuafit) na twitter-(kuafit)

About Kuafit

Kuafit
Recommended Posts × +

0 comments:

KUPUNGUZA UZITO KWA MAJI YA BARIDI

Watu wengi katika jamii hupendelea kuoga na maji ya moto katika majira yote ya hewa lakini kutokana na utafiti uliofanywa na wanasayansi kam...