latest Post

UMUHIMU WA KUFUNGA KULA KIAFYA


Wengi wetu tunafahamu jambo hili la kufunga kula(kwa luga ya kiingereza ni fasting), kila mwaka tunawaona wa dini mbalimbali kama wakristo kwa waislamu wakifunga katika misimu tofauti kwa sababu za kiimani.Je! kufunga huku kunafaida zozote katika afya zetu?.Jibu ni Ndiyo kufunga kuna faida kubwa katika afya zetu, wengi wetu hatujui jambo hili tumekuwa watu wakula chakula kila siku mara tatu kwa siku 365 kila mwaka.Leo nataka nikujuze faida za kufunga kula na naimani baada ya kusoma ujumbe huu utachukua hatua ili upate faida za kufunga kula na kuimarisha afya yako.

kwanza kabisa naomba uondoe dhana ya kwamba kufunga ni kama kujitesa hapana! kufunga kunaleta faida nyingi katika afya yako.Kwa mfano, mitambo ya viwandani ambayo imeundwa kwa vyuma imara tena vyenye nguvu hufika wakati ambao hulazimika kusimamishwa kwa marekebisho ili kuiendesha kwa ubora zaidi. ,vivyo hivyo hata katika upande wa chakula tumbo nalo linabidi lipumzike.
Watu mara nyingi hudhani kuwa kufunga ni  kuto kula kabisa bali sio kweli, kufunga kuna aina nyingi  ya kufunga. aina ya kufunga ambayo hutumika sana siku hizi ni (inter-mate) ambapo mtu hufunga kwa kipindi cha siku 30, na mtu hupaswa kutumia vyakula ambavyo ni vitamini,protini na wanga kwa wingi.

NINI FAIDA YA KUFUNGA KIAFYA?

1.Kuboresha Kinga ya mwili.


   Faida za kufunga kimwili ziko nyingi tu,faida mojawapo ni kuboresha kinga ya mwili wako,mwili wako unahitaji kinga ili kujiepusha na mradhi mbalimbali unapofunga hufanya kinga ya mwili wako kujiimarisha ili kuweza kukabiliana na hali yoyote.


2.Kuimarisha afya ya Ubongo


 Kufunga kula kumeonesha kuboresha utendaji kazi wa ubongo kwa  kunachochea uzalishaji wa protini ya brain-derived neurotrophic factor (BDNF) ambayo ni muhimu sana katika afya na utendaji kazi wa seli za fahamu za ubongo.

3.Husaidia kupunguza uzito mwilini.


 Kufunga kunaweza kuwa ni njia salama kupunguza uzito wa mwili  kwa kuwa tafiti nyingi zimeonyesha kuwa kufunga kwa muda fulani(saa 12),inaruhusu mwili kwa kuchoma kupitia seli za mafuta kwa ufanisi zaidi ya kula mara kwa mara.

4.Kuishi kwa muda mrefu.


 Unapopunguza kula mara kwa mara ndivyo utakavyoishi kwa muda mrefu.Uchunguzi umeonyesha jinsi muda wa kuishi(lifespan) kwa watu katika tamaduni fulani kuongezeka kutokana na ulaji wao.Watafiti wa afya wanashauri kupunguza kula ili kuzuia kuzeeka mapema.


5.Ngozi kuwa na muonekano mzuri.


Wengi wetu tunapenda kuwa na muonekano mzuri wa ngozi zetu na njia moja wapo ni kufunga,unapofunga kiwango cha sukari kinapungua mwilini na kufanya ngozi kuwa na muonekano mzuri.


Faida zingine ni kupunguza shinikizo la damu mwilini,husaidia uzalishaji wa seli mpya mwilini,kuboresha afya ya moyo na kusadia kutawala sukari mwilini.


kama tulivyo elezea hapo awali kwamba kuna aina mbalimbali za kufunga, unaweza ukaamua kufunga kula(bila kunywa maji) tangu asubuhi mpaka jioni(saa 12 jioni).Aina nyingine ya kufunga ni ile ya kutokula chakula chochoe ila unakunywa maji tu peke yake kwa muda maalumu.Pia unaweza ukawa unakula matunda tu tangu asubuhi mpaka jioni.Hata hivyo inashauriwa mtu kujua hali yake ya kiafya kwanza kabla ya kuanza kufunga, hivyo ni vyema ukaonana na mtaalamu wa afya akupe ushari zaidi kutokana na hali ya afya yako.
Kwenye kufunga kunampasa mtu kuzingatia mda wa kula kwa sababu kwa kukaa mdaa mrefu ya zaidi ya masaa 12 huweza kudhoofisha afya yake, jambo hilo hutokea maana mwili uhitaji nguvu itokanayo na chakula itwayo(calorie).



Kama umeipenda andiko hili basi gonga NZURI  na  kwa maswali au maoni zaidi basi tuandikie baada ya andiko hili, na pia kama ungependa kusoma andiko jengine kama hili basi jisajili kwa kuweka anuani yako  kwenye linki ya SUBSCRIBE.


Pia waweza tuandikia kwa email yetu Kuafit08@gmail.com 


Kwa number yetu ya Tigo +255 653 009 477  


Instagram account yetu  (KUAFITI), Facebook-(kuafit) na twitter-(kuafit)





About Unknown

Unknown
Recommended Posts × +

0 comments:

KUPUNGUZA UZITO KWA MAJI YA BARIDI

Watu wengi katika jamii hupendelea kuoga na maji ya moto katika majira yote ya hewa lakini kutokana na utafiti uliofanywa na wanasayansi kam...