latest Post

VYAKULA MUHIMU KWA MTU ANAYEHITAJI 6-PACKS


Vyakula huchangia zaidi ya silimia 60 ya mabadiliko ya mwili ambapo mazoezi huchukua asilimia 30 na asilimia zilizo baki huchangiwa na juhudi binafsi kutekeleza .
Kutokana na hayo basi ni vyema mtu kufahamu umuhimu wa vyakula kulingana na mabadiliko yanayohitajika mwilini.
Kutengeneza misuli ya tumbo itwayo rectus abdominis ama 6-packs uhitaji mtu kuzingatia mazoezi bila kusahau kuzingatia vyakula muhimu ili kutengeneza misuli hiyo. Vyakula hivyo kwa mara nyingi huwa ni vyakula visivyo na mafuta na pia vyakula vyenye kemikali zenye uwezo wakufanya mwili kutokufadhi mafuta.
Kulingana na maelezo hayo basi tutaangalia vyakula sita ambavyo hufanya kazi kwa ufanisi ili kuhakikisha matokeo ya haraka, na vyakula vyenyewe ni

  1. Viazi vitamu
  Kutokana na kwamba viazi vitamu huwa na kemikali itwayo carotenoid ambayo husaidia mwili kuwianisha kiwango cha sukari na pia husaidia kuzuia vyakula vyenye calorie kubwa kuhifadhiwa kama mafuta mwilini. Viazi vitamu pia vinafahamika kuwa na fiber na virutubisho vinanvyosaidia mtu kukaa mda mrefu bila kula hivyo kufanywa kuwa vyakula sahihi kwa mtu mwenye kutaka kupunguza mafuta ya tumbo na kujenga 6-pack.    2. Green tea

  Kwa mtu anayetamani kuoana matokeo ya haraka zaidi hasa katika kupunguza unene na mafuta basi anashauriwa kunywa chai ya kijani (green tea) japo mara mbili kwa siku. Utafiti unaonyesha kwamba chai hii huwa na kemikali itwatyo catechins ambayo funya kazi kama antioxidant inayozuia mafuta kuhifadhiwa mwilini. Hivyo basi green tea imeonekana kuwa ni muhimu sana kwa mwanana-mazoezi anyaetaka kupunguza mafuta ya mwili na kujenga 6-packs.   3. Apple

 Kulingana na utafiti uliofanywa na Forest Babtist Medical Center inasemekanan yakwamba kutokana na tunda la apple kuwa na kiasi kikubwa cha fiber basi kwa kila gram 10 ya fiber inayoliwa kutokana na ma-apple kwa siku huchangia kutoka kwa mafuta ya tumbo kwa asilimia 3.6.
Tunda la apple husifika kwa kuwa na kemikali itwayo flavonoids (antioxidant) ambayo husaidia kuunguza mafuta yasiyohitajika mwilini.


  4. Spinach

  Spinach ni kati ya mbogamboga ambazo ni muhimu sana hasa kwenye kumsaidia mtu kutokusikia njaa mara kwa mara kutokana na kemikali itwayo  thaylakoids. kutokana na kwamba spinach inakiwango kikubwa cha protini basi husaidia misuli kuweza kujihimarisha hasa pale mtu anapotoka kufanya mazoezi ya kujenga misuli kama (body building).


  5. Mayai

  Mayai huwa na kirutubisho kiitwacho cholin ambacho husaidia kuongeza uwezo wa mwili kutumia chakula kwa wingi na kupunguza kiwango cha mafuta yanayohifadhiwa mwilini. 
Utafiti unaonyesha yakwamba mtu anayetumia mayai ya kuchemsha katika mlo wake wa asubuhi na jioni anauwezo wa kupunguza mafuta ya tumbo kwa asilimia kubwa kuliko anae kula mayai yaliyokaangwa.


 6. Mafuta ya olive

  Kutokana na sifa ya mafuta ya olive kuwa na uwezo mkubwa wa kupunguza cholestrol na kuongeza kinga ya mwili  basi mafuta hayo husemekana ni mafuta sahihi yanayopaswa kutumika kwenye kupika pale mtu anapotaka kupunguza mafuta ya tumbo.
Mafuta ya olive husaidia kupunguza uwezekano wa mtu kupata maradhi ya moyo, cancer na hata pia utapiamlo.


Kumbuka kutengeneza misuli ya tumbo (6-packs) sio rahisi wala sio ngumu, bali ni jitihada zako ndizo zitakazokuwezesha kutimiza nia uliyokuwanayo.

Kama umeipenda andiko hili basi gonga NZURI  na  kwa maswali au maoni zaidi basi tuandikie baada ya andiko hili, na pia kama ungependa kusoma andiko jengine kama hili basi jisajili kwa kuweka anuani yako  kwenye linki ya SUBSCRIBE.
Pia waweza tuandikia kwa email yetu Kuafit08@gmail.com 

Kwa number yetu ya Tigo +255 653 009 477  

Instagram account yetu  (KUAFITI), Facebook-(kuafit) na twitter-(kuafit)


About benson godfrey

benson godfrey
Recommended Posts × +

DIET YA KUTOA SUMU MWILINI NA KUPUNGUZA UNENE KWA HARAKA

Habari zenu wadau wa KUAFIT! leo tutaongelea kuhusiana na elimu ya lishe ambayo itahusiana na diet ambapo tutaelezea mambo mengi san...