latest Post

FAIDA ZA JUISI YA UKWAJU


Ukwaju ni tunda lenye rangi ya kahawia linalofahamika na asilimia kubwa ya watu duniani na hata hapa nchini kwetu Tanzania ambapo hutumia kwa kutengeneza kwa vinywaji baridi kama vile juisi. Tunda hili linalotokana na mti wa mkwaju ambao huota hasa maeneo ya porini lakini hata hapa nchini kwetu Tanzania hupatikana katika maeneo mbalimbali. Kikawaida ukwaju una ladha ya uchachu ukiwa bado mchanga, lakini unavyozidi kukomaa unakuwa na ladha tamu, lakini kiujumla ukwaju una ladha ya uchachu. Wengi wao  ambao hutumia tunda hili lenye ladha ya uchachu uchachu kwa kutengenezea hasa juisi ambayo hutumika kama kinywaji kinachoburudisha bila kujua endapo tunda hili lina faida nyingi katika afya zao.Pia hata wataalam wa afya wamekuwa na mtazamo tofauti na kueleza kuwa juisi ya ukwaju inafaida nyingi katika afya ya  binadamu tofauti na wengi wanavyodhani.


FAIDA ZA JUICE YA UKWAJU

1.Husaidia myeyusho na mmeng'enyo wa chakula mwilini

Chakula tunachokula kila siku lazima kimeng'enywe katika mfumo mzima wa chakula mwilini.Hivyo kwa kutumia juisi ya ukwaju utarahisisha kazi ya mmeng'enyo katika mwili wako.

2.Husaidia kurahisisha choo na kutoa mngurumo wa  tumbo

Hii ni dawa tosha kwa wale wanaosumbuliwa na kupata choo mara kwa mara,unapotumia juisi ya ukwaju itakusaidia kurudi katika hali yako ya kawaida ya kupata choo cha kawaida 


3.Huongeza vitamini mwilini

Unapokunywa juisi ya ukwaju unajiahakikisha kuongezeka kwa vitamini muhimu katika mwili wako na kukulinda dhidi ya magonjwa mbalimbali. Juisi ya ukwaju husaidia kuongeza vitamin A, B na C, lakini pia ina madini ya chuma, ‘calcium’ na ‘zink’ ambazo zinafaida katika afya yako.


4.Ukwaju unakusaidia kutibu matatizo ya nyongo.

kwa wale wanaosumbuliwa na matatizo ya nyongo wanashauriwa kutumia juisi hii ya ukwaju ili kutibu tatizo hilo.


5. Ukwaju unasaidia kupunguza homa na kukupa ulinzi dhidi ya mafua.

Mara kwa mara watu wamekuwa wakisumbuliwa na homa za mara kwa mara na kupata magonjwa ambukizi kama mafua.Unapotumia juisi ya ukwaju inasaidia kupunguza homa pia na kukuepushia mashambulizi ya kupata ugonjwa wa mafua.Kumbuka homa inapozidi unashauriwa kumuona mtaalamu wa afya mapema ili kujua tatizo  zaidi na kupata matibabu mapema.


6.Husaidia ngozi kuwa nyororo,pia inasaidia ngozi kupona baada ya kuugua au yenye vidonda

Juisi ya ukwaju pia inafaida katika kuboresha muonekano wa ngozi yako na kuwa katika hali bora zaidi.Kwa wale wenye majeraha ya vidonda juisi hii usadia ngozi kurudi katika hali yako ya awali.


JINSI UNAVYOWEZA TENGENEZA JUISI YA UKWAJU

Ukwaju unapatikana kwa wingi sana maeneno mbalimbali kwenye ukanda wa mashariki mwa Africa mashatiki na huuzwa katika masoko mengi. Unaweza kutengeneza juisi yako ya ukwaju  kwa kuandaa maji kwenye bakuli au sufuria na kuosha kidogo tuu  ili kuhakikisha usalama wa afya yako, baada ya kuuosha chukua ukwaju wako weka kwenye sufuria yenye maji ya wastani na injika jikoni, uache uchemke kwa wastani wa dakika 15  ili uuwe vijidudu. Baada ya hapo toa sufuria kwenye jiko iache ipoe kwanza, ikishapoa juice yako inakuwa tayari cha kufanya ni kuchukua glass au jagi na kuichuja toka kwenye sufuria mpaka kwenye jagi lako,baada ya hapo weka sukari kidogo kwenye juisi yako ya ukwaju,ukishamaliza hatua hizo utakuwa umemeliza kutengeneza juisi ya ukwaju.




Kutokana na faida hizo za juisi ya ukwaju  tunashauriwa kuongeza juhudi za upandaji miti hii ambayo wengi wanaamini ni miti ya porini kwani inaweza kuzisaidia afya za watu  wengi kuimarika bila kutumia gharama kubwa kununua dawa za viwandani ambazo zinazalisha sumu mwilini.Pia unashauriwa ujaribu kuweka ukwaju karibu katika kila mlo wako kwa kila siku kwasababu ukwaju una faida nyingi kiafya ambazo hakika zitakufanya uwe na afya njema au kukuimarisha afya yako kiujumla..Kama wewe unapenda kula hotelini au kwenye vioski basi agizo juisi ya ukwaju ikusaidie kushushia chakula.

Kama umeipenda andiko hili basi gonga NZURI  na  kwa maswali au maoni zaidi basi tuandikie baada ya andiko hili, na pia kama ungependa kusoma andiko jengine kama hili basi jisajili kwa kuweka anuani yako  kwenye linki ya SUBSCRIBE.


Pia waweza tuandikia kwa email yetu Kuafit08@gmail.com 


Kwa number yetu ya Tigo +255 653 009 477  


Instagram account yetu  (KUAFITI), Facebook-(kuafit) na twitter-(kuafit)

About Unknown

Unknown
Recommended Posts × +

0 comments:

KUPUNGUZA UZITO KWA MAJI YA BARIDI

Watu wengi katika jamii hupendelea kuoga na maji ya moto katika majira yote ya hewa lakini kutokana na utafiti uliofanywa na wanasayansi kam...