latest Post

AINA 5 YA MAZOEZI YANAYOMFAA MTU MWENYE KISUKARI

 
Kisukari ni ugonjwa usio ambukizwa bali pia ni ugonjwa hatari ambao husababisha watu wengi kupoteza viungo vya mwili na hata maisha. Kisukari huadhiri watu wa rika zote bali kwa namna mbili tofauti, namna ya kwanza ni (type1) ambayo huadhiri watoto hadi vijana wadogo na ya pili ni (type2) ambayo huadhiri watu wazima.Utafiti unaonyesha watu wanaosumbuliwa na aina ya pili ya kisukari(type2) ndio wenye hatari kubwa sana kuliko watu wenye (type1) ambapo magonjwa kama presha, matatizo ya moyo huwanyemelea kwa karibu zaidi.
Ufanyaji wa mazoezi kwa watu wenye kisukari unahitaji uwangalifu mkubwa hasa kwa mtu mwenye aina ya pili ya kisukari(type2) maana mwili wake huwa unauwezo kuwa na tatizo zaidi ya moja.
Kutokana na kwamba watu wenye ugonjwa wa kisukari wa aina ya pili(type2) kupata tatizo la seli zao kuharibika(neuropathy) basi mtu huyo anapaswa kuwa mwangalifu sana tazama vitu vya msingi vya kuzingatia kwa mtu mwenye kisukari anyetaka kufanya mazoezi.
Watu wenye matatizo ya kisukari hasa watu wenye kisukari cha aina ya pili ni rahisi kutambulika kutokana na wengi kuwa na matumbo makubwa kama dalili ya utapia mlo. Matumbo hayo ni matokeo ya mafuta ya tumbo yanayohifadhiwa na seli za visceral nadani ya viungo vya ndani ya mwili. Pamoja seli hizo za visceral kujihusisha na mafuta ya tumbo, seli hizo pia hutoa kemikali itwaayo RBP4 ambayo husababisha kupunguza uwezo wa mwili kutumia insulin ili kupunguza kiwango cha sukari mwilini.
Utafiti unaonyesha yakwamba mtu mwenye kisukari anauwezo mkubwa wa kujenga afya yake pale atakapoamua kubadili utararibu wake wa maisha, na swala hili linawezekana eidha kwa kujihusisha na mazoezi ama kwa kuanza kula vyakula vyenye tija kwa afya yake

Mazoezi mazuri kwa mtu mwenye kisukari

. Mtu mwenye kisukari anshauriwa kufanya mazoezi ya kupunguza tumbo ilikupunguza mafuta na kemikali ya RBP4 itokanayo na seli za visceral, na pia kuongeza nguvu kwenye viungo vyake vyamwili na kupunguza uzito na mafuta yasiyohitajika.
  • Bicep curl

Zoezi hili ni kati ya mazoezi ya spot strength training ambapo hulenga kundi la msuli wa mbele wa mkono(bicep) ambapo uhusisha kukunja na kunyoosha mkono huku ukiwa umesimama wima.
umuhimu wa zoezi hili ni kujenga nguvu kwenye mikono.
  • Incline pushup


Zoezi hili ni kati ya mazoezi ya kujenga nguvu kwenye mikono na kifua, na hapo mtu atahitajika kutafuta sehemu iliyoinuka na kisha kufanya zoezi la pushup kwa kurudisha miguu nyuma angalau futi moja na nusu na kuelemea mbele zaidi bila kujikunja. Zoezi hili pia hugusa tumbo hivyo ni kati ya mazoezi mazuri zaidi
  • Dumbbell squat overhead press

Zoezi hili ni mjumuiko ya mazoezi mawili ambapo mtu analazimika kupiga squat huku akiwa amebeba uzito(dumbbell) akiwa amekunja mikono na kisha kunyanyuka akiwa amenyoosha mikono. Zoezi hili hulenga miguu, tumbo, mikono na pia mabega ambapo hujenga nguvu na kutoa mafuta yasiyohitajika.
  • V-ups leg reach

Zoezi hili ni kati ya mazoezi mazuri sana ya tumbo ambapo mtu anapaswa kulala na mgongo kwenye mattress na kisha kunyanyua miguu juu bila kukunja huku mikono ikiwa imenyanyuka kugusa miguu. Kumbuka sio lazima kutumia mpira kama invyoonekana hapo juu.
  •  Knee too elbow 
Zoezi hli ni kati ya mazoezi mazuri ya punguza mafuta ya mwili na pia ni kati ya zoezi zuri la tumbo.
Kufanya zoezi hili mtu analazimika kunyanyua magoti juu na kugusa kiwiko cha mkono tofauti huku mwili ukiwa unageuka kuelekea upande wa goti lililonyanyuka. 

Kumbuka: Mtu mwenye kisukari anapaswa kuwasiliana na daktari awake ili kuweza kupata vipimo staiki na pia kupata muongozo wa jinsi anavyopaswa kuendesha maisha yake huku akiwa anafanya mazoezi.
Kama umelipenda andiko hili basi gonga NZURI  na  kwa maswali au maoni zaidi basi tuandikie baada ya andiko hili, na pia kama ungependa kusoma andiko jengine kama hili basi jisajili kwa kuweka anuani yako  kwenye linki ya SUBSCRIBE.


Pia waweza tuandikia kwa email yetu Kuafit08@gmail.com 


Kwa number yetu ya Tigo +255 653 009 477  


Instagram account yetu  (KUAFITI), Facebook-(kuafit) na twitter-(kuafit

About Kuafit

Kuafit
Recommended Posts × +

0 comments:

KUPUNGUZA UZITO KWA MAJI YA BARIDI

Watu wengi katika jamii hupendelea kuoga na maji ya moto katika majira yote ya hewa lakini kutokana na utafiti uliofanywa na wanasayansi kam...