latest Post

JE! KUJAMIANA HUPUNGUZA UFANISI NA UWEZO WAKUONGEZA MISULI KWA MWANAUME?


  Kati  ya maswali ambayo huwa tukiyapata kuhusiana na mazoezi  ni hili, "kwa namna gani tendo la kujamiana linaweza adhiri mfanya mazoezi hasa ya vyuma katika swala la kuongeza misuli?"
Swali hili huulizwa na wengi walio ndani ya mahusiano kwa hofu ya kutumia mda mrefu kwenye mazoezi ya kunyanyua vyuma pasipo mwili kuonyesha mabadiliko ya kuridhisha.Hata wanamichezo wengi duniani hujiweka mbali na wenza wao kwa hofu ya kupungua kwa ufanisi wa kazi yake ama kiwango chake cha kuongeza misuli baada ya tendo la ndoa.

Uhusiano wa mazoezi na kujamiana upo kibiolojia na hii ni kutokana na homoni za testosterone, oxytocin na pia kutokana na madini ya zinc.

 Katika mwili wa mwanaume madini ya zinc ni ya muhimu sana hasa ukizingatia kwamba madini haya huchangia katika ukuwaji wa mbegu zake, na pia kwa kukosekana kwa mbegu hizi ndipo mwanaume hufahamika kama tasa. Endapo mwanaume atajamiana sana kupita kiasi basi ana hatari yakuweza kupungukiwa na zinc ambayo pamoja na kuchangia ukuwaji wa mbegu za kiume bali pia huchangia kwa asilimia kubwa ukuaji wa misuli.
Kwa mtu aliyepoteza madini ya zinc kwa wingi huwa na dalili za uchovu na kutotamani tendo la ndoa, na inashauriwa kwa mtu mwenye tatizo hilo aweze kurudisha hali ya kawaida kwa kuongeza kula vyakula vyenye zinc ndani yake kama vile spinach na hata nyama ya ngome isiyo na mafuta.

Homoni ya testosterone ni homoni inayoleta mchango mkubwa sana hasa kwenye ukuwaji wa maungo ya siri ya mwanaume, na  pia homoni hii huchangia uotaji wa nywele na kikubwa zaidi ukuaji wa misuli na mifupa. Mwanaume mwenye kufanya tendo la ndoa sana ana hatari kubwa ya kuweza kupunguza kiwango cha testosterone, na kwa kupungua kwa kiwango cha homi hiyo kinaweza kupunguza kasi ya ukuaji wa misuli. Kwa mwanaume anayetaka kuongeza misuli anapaswa kuzingatia kiwango cha homoni ya testosterone kwa kula vyakula vyenye zinc na pia kwa kuongeza vyakula vyenye mafuta yenye na tija kwenye mwili kama vile mafuta ya ufuta.

Homoni ya oxytocin kwa jina lingine ni homoni ya mapenzi ambayo huachiliwa na mtu pale anapofika kileleni wakati wa tendo la ndoa, na hata pia hutumika pia na madaktari kama njia ya kuasidia kina mama wakati wa kujifungua. Homoni hii ikiachiliwa baada ya tendo la ndoa husababisha mtu kujisikia mchovu na pia kujihisi kama mtu asiye na nguvu. Mwanaume aliyetoka kufanya tendo la ndoa anaweza akarudi katika hali yake ya kawaida endapo atasubiri mda wa masaa mawili ama zaidi baada ya kufika kileleni na kujihisi mchovu. Mtu aliyetoka kufanya tendo la ndoa na kufika kileleni analazimika kutokufanya mazoezi ya kubeba vyuma vizito kabla ya kupumzika kwa angalau masaa mawili, na hii ni kwa sababu ya kupunguza uwezekano wa kupata ajali na kujiumiza wakati wa mazoezi.

Hitimisho
 Kwa  mtu anayefanya mazoezi ya kukuza misuli anaweza kufanya tendo la ndoa ama kujamiana bali kwa kuzingatia mambo muhimu ambayo ni lishe bora, kufanya mazoezi ya cross fitness(mjumuisho wa mazoezi mengi kama na cardio na aerobics)
Kwa kuzingatia maswala hayo ya msingi basi ni rahisi sana kwa mtu kuweza kutengeneza mahusiano himara na mwenzi wake, na pia kuweza kutengeneza mwilil wenye afya na misuli iliyo himara.

Kama umeipenda andiko hili basi gonga NZURI  na  kwa maswali au maoni zaidi basi tuandikie baada ya andiko hili, na pia kama ungependa kusoma andiko jengine kama hili basi jisajili kwa kuweka anuani yako  kwenye linki ya SUBSCRIBE.

Pia waweza tuandikia kwa email yetu Kuafit08@gmail.com 
Kwa number yetu ya Tigo +255 653 009 477  
Instagram account yetu  (KUAFITI), Facebook-(kuafit) na twitter-(kuafit

About Kuafit

Kuafit
Recommended Posts × +

0 comments:

KUPUNGUZA UZITO KWA MAJI YA BARIDI

Watu wengi katika jamii hupendelea kuoga na maji ya moto katika majira yote ya hewa lakini kutokana na utafiti uliofanywa na wanasayansi kam...