latest Post

VYAKULA VYA KUVIEPUKA UNAPOPUNGUZA ENENE WA MWILI WAKO


karibu tena katika site yako pendwa ya kuafit.com siku ya leo tutazungumiza swala zima la vyakula vya kuviepuka endapo upo katika  mazoezi yaa kupunguza enene wa mwili wako.
Inawezekana umefuata kanuni zote za mazoezi za kupunguza enene lakini bado huoni mabadiliko na umeanza kukata tamaa.kumbuka mazoezi na vyakula lazima viendane sawa ili uweze kupata matokeo chanya unayoyategemea, huwezi ukafanya mazoezi ya kupunguza unene huku bado unaendelea kula vyakula ambavyo vinaongeza unene na ukategemea mabadiliko chanya hapana huwa haiendi kwa mtindo huo.Pale unapoamua kuanza mazoezi ya kupunguza unene inakulazimu pia kuacha kula baadhi ya vyakula ambayo vina mchango mkubwa wa kuongeza unene wa mwili wako.Pia wataalamu wa afya wanashauri kufanya mazoezi mbalimbali lazima kuendane na vyakula unavyokula, hii itakusaidia kuona mabadiliko kutokana na mazoezi unayoyafanya.



VYAKULA UNAVYOTAKIWA KUVIEPUKA

1.Vinywaji baridi vya viwandani.


Vinywaji hivi vinavyotengenezwa na kuongezewa sukari ili kuwa vitamu vinatajwa kuwa ni mojawapo vyakula hatari zaidi kiafya duniani.Vinywaji vingi vinavyotengeneza viwandani uwa na virutumbisho vichache sana vinavyoweza kuboresha afya yako ukilinganisha na matunda halisi.Vinywaji vya viwandani huwa na sukari nyingi ndani yake.Hivyo inashauriwa kupenda kunywa juisi za  matunda halisi kwani huwa zina faida nyingi kuliko vinywaji vya viwandani.Matunda halisi yanapatikana kila mahali tena mengine kwa bei nafuu ambayo unaweza ukanunua na kutengeneza juisi yako ukiwa nyumbani na ukainywa wewe pamoja na ndugu au jamaa bila kuleta madhara yoyote mwilini. Vinywaji vya kuviepuka ni soda, bia pamoja na juisi za kopo za viwandani.

2.Baadhi ya vyakula vya kukaanga.


Baadhi ya vyakula vya kukaanga ni mojawapo ya vyakula vinavyopendwa sana na watu hasa wakazi wa mijini,hii ni kutokanana upatikanaji wake kwa urahisi karibu maeneo wakazi wanapoishi.Vyakula hivi  pia huwa vinasababisha kuongezeka kwa unene mwilini kutokana na kuwa na kalori nyingi ndani yake.Tafiti nyingi zinaonyesha kuwa chakula aina ya chipsi pengine ndiyo chakula kinachochangia kuongezeka unene kuliko chakula chochote.Hivyo inashauriwa kupunguza kula vyakula hivi endapo upo katika mazoezi ya kupunguza unene wa mwili wako.Pia kama wewe ni mpenzi wa kula viazi unashauriwa badala ya kuvikaanga penda kuvichemsha na maji safi ndipo ule hiko chakula.Vyakula vingine vya kukaanga vya kuviepuka ni pamoja na sambusa na bagia kwani huweza kuchangia kuongezeka kwa unene katika mwili wako.


3.Mikate, biskuti, chokeleti na keki. 


Vyakula hivi huongezewa na virutubisho vingi ambavyo havina faida katika  mwili wako .Pia wakati mwingine huongezewa mafuta hatarishi ambayo yanahusishwa kuwa chanzo cha magonjwa tofauti. Kwa kawaida vyakula hivi havishibishi hivyo utatamani kuvitumia zaidi na hivyo kupelekea kula sumu zaidi katika mwili wako.


ukizingatia haya katika kipengele cha vyakula utaanza kuona matokeo chanya katika afya yako na hata juhudi zako za kufanya mazoezi ya kupunguza unene yatakuwa na tija na faida kubwa sana kwako. Pia ni vyema ukajua Body Mass Index ya mwili wako (soma hapa  http://www.kuafit.com/2017/12/fahamu-body-mass-index-ya-mwili-wako.html) ili unapofanya mazoezi ya kupunguza unene usijeuzito ukapitiliza( ni vyema kimo chako kiendane na uzito wako ) kumbuka mazoezi bila kuzingatia mlo sahihi na kufanya kazi bure.

Kama umeipenda andiko hili basi gonga NZURI  na  kwa maswali au maoni zaidi basi tuandikie baada ya andiko hili, na pia kama ungependa kusoma andiko jengine kama hili basi jisajili kwa kuweka anuani yako  kwenye linki ya SUBSCRIBE.


Pia waweza tuandikia kwa email yetu Kuafit08@gmail.com 


Kwa number yetu ya Tigo +255 653 009 477  


Instagram account yetu  (KUAFITI), Facebook-(kuafit) na twitter-(kuafit)



About Unknown

Unknown
Recommended Posts × +

0 comments:

KUPUNGUZA UZITO KWA MAJI YA BARIDI

Watu wengi katika jamii hupendelea kuoga na maji ya moto katika majira yote ya hewa lakini kutokana na utafiti uliofanywa na wanasayansi kam...