latest Post

MAANA YA MEDITATION(TAHAJUDI) NA FAIDA ZAKE KATIKA AFYA

Akili ni sehemu mojawapo muhimu sana  katika maisha yetu, pale tunapokuwa na msongo wa mawazo kutokana na shughuli zetu za kila siku,changamoto tunazokalibiana nazo katika kazi na biashara, majukumu ya kifamilia upelekea mtu kuwa na msongo wa mawazo kama hatakuwa makini.mambo haya upelekea akili zetu kuwa  katika hali ya kufikiri muda wote, unaweza ukawa ofisini lakini akili yako inawaza matatizo yaliyopo katika familia yako hivyo kupelekea kutofanya kazi kwa ufasaha au mambo mengine.

Hali hii ikiendelea kwa muda mrefu upelekea athari mbalimbali katika afya zetu na kusababisha magonjwa mbalimbali na hivyo afya yako kuanza kuzorota lakini chanzo cha  mambo yote limeanzia katika akili yako (kumbuka akili ni sehemu muhimu katika afya yako).Hivyo ni muhimu sana kuwa  utulivu katika akili zetu ili kuwa na afya njema.

Siku ya leo ningependa kuzungumzia jambo ambalo nina nina imani wengi hawalifahamu au wamesikia ila hawajui faida zake ana umuhimu wake katika afya zetu.Neno meditation inawezekana umelisikia  sehemu tofauti tofauti , neno hili kwa lugha yetu ya kiswahili ni TAHAJUDI likiwa na maana ya kufikiri kwa uzingativu au kwa kujali.Neno meditation, nalo limetokana na neno la kilatini linaloitwa 'meditatio' likiwa na maana ya mazoezi ya mwili na akili

Tahajudi ni kitendo cha kutazama hali ya akili na kuongeza utambuzi na umakini. Wengi wanaofanya tahajudi ni kwa lengo la kuituliza akili kutoka katika msongo wa mawazo, kuongeza umakini na utambuzi juu ya mtu binafsi na jinsi alivyo. Pia wengine hufanya Tahajudi kuachana na addictions na mazoea .Wengine hufanya meditation kuongeza umakini, ubunifu (mfano wachoraji, wanamuziki, wasomi n.k). Kuna sababu nyingi ambazo kila mtu binafsi anaamua kufanya meditation.


Watu wa dini mbalimbali huwa wanafanya tahajudi(meditation) kwa njia mbalimbali.Dini ya kikristo wanatumia rozari, hii huwasaidia kujenga uzingativu. Waislamu wanatumia tasbihi ambayo huwasaidia kujenga uzingativu,Wabudha huwa wanafanya tahajudi kila siku kwani ndiyo nguzo yao kuu.Lakni tahajudi inaweza fanywa na mtu yoyote na kupata faida zake. FAIDA ZA KUFANYA MAZOEZI YA TAHAJUDI


Ili uweze kutambua faida za tahajudi, ni muhimu kuifanya kila siku, ikiwezekana asubuhi na jioni. Tahajudi ina faida nyingi sana, faida hizi utaziona tu kama utafanya tahajudi kila siku. Ina faida kubwa sana, hivyo ni vizuri ukajenga mazoea ya kuifanya kila siku. Nakushauri ufanye hata kwa dakika 5, 10 au 15

1.Husaidia kuleta furaha  katika nafsi yako.

2.Husaidia kutibu matatizo mengi ya kisaikolojia(akili) kwani hubadili hali ya mfumo wa fahamu na mawazo (endapo itafanywa kila siku).

3. Husaidia kuratibu msukumo wa damu pamoja na usafirishwaji wa damu mwilini.

4. Husaidia pumzi pamoja na kurahisisha usagwaji au umeng'enyo wa chakula mwilini.

5. Husaidia kuimarisha mfumo wa kinga mwilini na kupelekea kutopata magonjwa mbalimbali katika mwili wako.

6.Tahajudi imenisaidia kuondoa takataka nyingi kwenye akili yangu. Akili zetu binadamu ni kama sumaku ambayo inavuta vitu vinavyoendana nayo bila kujali usafi au uchafu, faida au hasara ya vitu hivyo. Kuna mawazo mengi yanayopandikizwa kwenye kichwa chako kila siku na kila wakati. Ili kuweza kuchuja takataka na kuacha vyenye manufaa meditation ina msaada mkubwa sana.

7. Husaidia kuongeza ubora wetu kiakili, kimwili pamoja na uwezo wetu kwa ujumla. Husaidia kuuburudisha mwili, pia husaidia kupumzisha akili na mwili.

8.Husaidia kuratibu msukumo wa damu katika mwili wako  pamoja na usafirishwaji wa damu mwilini.Kutokana na faida hizi na imani sasa umefunguka na utaanza kufanya tahajudi(meditation) kuwa sehemu ya maisha yako na uone jinsi utakavyofaidika.kama ukifanya vizuri tahajudi, utahisi nafuu fulani kimwili au kiakili ama vyote. Utagundua kwamba, mwili hasa upande wa msukumo wa damu, utakuwa na mabadiliko.

Je Tahajudi ina madhara yoyote?

Hili ni swali muhimu sana kujiuliza kabla hujaanza kufanya tahajudi,Kwa watu wenye matatizo ya kifafa, matatizo makubwa ya moyo au wenye matatizo ya akili, tahajudi inaweza kuwaumiza wasipokuwa waangalifu, ingawa kwa upande mwingine, tahajudi ni tiba/dawa kwao. Hivyo, wanashauriwa wachague tahajudi ambayo haitawaletea matatizo.

makala hijayo nitazungumza aina za tahajudi na  hatua ya kufanya mazoezi ya tahajudi.

Kama umeipenda andiko hili basi gonga NZURI  na  kwa maswali au maoni zaidi basi tuandikie baada ya andiko hili, na pia kama ungependa kusoma andiko jengine kama hili basi jisajili kwa kuweka anuani yako  kwenye linki ya SUBSCRIBE.

Pia waweza tuandikia kwa email yetu Kuafit08@gmail.com 
Kwa number yetu ya Tigo +255 653 009 477  
Instagram account yetu  (KUAFITI), Facebook-(kuafit) na twitter-(kuafit

About Davis David

Davis David
Recommended Posts × +

DIET YA KUTOA SUMU MWILINI NA KUPUNGUZA UNENE KWA HARAKA

Habari zenu wadau wa KUAFIT! leo tutaongelea kuhusiana na elimu ya lishe ambayo itahusiana na diet ambapo tutaelezea mambo mengi san...