Kikawaida ujauzito kwa mwanamke hudumu ndani ya wiki 40 ambapo kwa jumla ni sawa na miezi tisa. Ndani ya kipindi hicho mwilii wa mwanamke hupata mabadiliko mengi ambapo hutokana na ukuaji wa mtoto ndani ya tumbo la uzazi. Mabadiliko hayo ndani ya mwanamke mjamzito kwa kitaalamu hutokea kwa vipindi vitatu ambavyo ni kipindi cha kwanza (first trimester), kipindi cha pili( second trimester), kipindi cha tatu( third trimester). Ni ndani ya vipindi hivi ambapo mtoto huchukua hatua ndogo ngogo za ukuaji na vipindi hivi hufahamika kulingana na wiki ambazo mwanamke mja mzito amezifikisha.
Ni kweli kwamba kuna haja kubwa ya wanawake wajawazito kufanya mazoezi kutokana na kwamba miili yao huitaji kuwa na nguvu na imara ili afaya ya mtoto iweze kuhimarika pia.
Tazama faida ya wanawake wajawazito kufanya mazoezi
Ukuaji wa mtoto ndani ya mwanamke mjamzito huathiri mwili wa mwanamke kwa namana nyingi kama vile uvutaji pumzi, mzunguko wa damu, mapigo ya moyo na pia bila kusahau upanganyikaji wa misuli ndani ya mwili wake.
Mazoezi kwa wanawake wajawazito hupaswa kufanywa kwa kuzingatia vipindi vitatu vya ujauzito kama nilivyo elezea awali. Ndani ya vipi hivyo vitatu mwanamke mjamzito anapaswa kufanya mazoezi kulingana na kipindi alichopo ili aweze kupunguza uwezekano wa majeraa kutokana na mabadiliko yaliyoletwa na ujauzito pia kuepusha kuhatarisha maisha ya mtoto.
- Kipindi cha kwanza(first trimester)
-Yoga
ambapo atanyoosha misuli ya mwili na kumfanya ajisikie vizuri na mwenye afya
-Kutembea
ambapo kwa kutembea kutamfanya aweze kupunguza uwezekano wa mwili wake kuvimba kwa kukaa sehemu moja na pia kujenga pumzi.
-Kucheza aerobics
kwa kufanya mazoezi ya aerobics kutamwezesha kufanyisha moyo mazoezi kwa kusukuma damu kwa wingi na pia kutamsaidi kutokuvimba kwa mwili
Kwa mwanamke mwenye uzoefu katika ulimwengu wa mazoezi anaweza akafanya mazoezi zaidi kuliko mwanamke ambaye hana historia ya kufanya mazoezi. Mazeozi ya nyongeza ukitoa yale ambayo mwanamke asiye nahistoria ya mazoezi anayoweza kufanya ni kama vile;-
-Squat
ambapo kwa kufanya hili mwanamke mja mzito mwenye uzoezi wa mazoezi anaweza akajenga nguvu zaidi ya miguu.
- Kunyanyua vyuma
ndio! kwa mwanamke mwenye ujuzi wa mazoezi aliyekuwa mjamzito anaweza kunyanyua vyuma vyenye uzito mdogo ili kuongeza nguzu na kukaza misuli(toning) na pia viungo vya mwili.
-Kuogelea
kwa kufanya mazoezi ya kuogelea mwanamke mjamzito anweza kuongeza nguvu ya viungo vyake vya mwili na pia kujenga pumzi.
- Kipindi cha pili(second trimester)
-Mazoezi ya kujinyoosha
kwa kuanfya mazoezi ya kujinyoosha(stretching) kunaweza kuweka mwili wake katika hali nzuri ambapo hatopata maumivu ya viungo kama vile mgongo na mengineyo.
-Kutembea
kwa kufanya mazoezi haya ya kutembea kunaweza kumsaidia mjamzito kutokuvimba kwa miguu yake na pia kusaidia kwenye swala la pumzi.
kwa kufanya mazoezi haya ya kutembea kunaweza kumsaidia mjamzito kutokuvimba kwa miguu yake na pia kusaidia kwenye swala la pumzi.
-Yoga
kutokana na ukubwa wa tumbo kwa kipindi hiki na kushindwa kufanya mazoezi mengi kwa mama mjamzito basi ni vyema kufanya zoezi hilli ili aweze kujinyoosha na kutengeneza afya nzuri ya akili yake mbali na msongo wa mawazo.
kutokana na ukubwa wa tumbo kwa kipindi hiki na kushindwa kufanya mazoezi mengi kwa mama mjamzito basi ni vyema kufanya zoezi hilli ili aweze kujinyoosha na kutengeneza afya nzuri ya akili yake mbali na msongo wa mawazo.
-Mazoezi ya kucheza muziki
mwanamke mjamzito anaweza akafanya mazoezi ya kucheza muziki kama vile salsa ambapo hatotumia nguvu nyingi ya mwili wake.
mwanamke mjamzito anaweza akafanya mazoezi ya kucheza muziki kama vile salsa ambapo hatotumia nguvu nyingi ya mwili wake.
- Kipindi cha tatu(third trimester)
-Kutembea
mwanamke mjamzito ndani ya kipindi hiki hushauriwa sana kufanya mazoezi ya kutembea kwa umbali mdogo ili aweze kupunguza uwezekana wa kuvimba miguu yake, na pia humsaidia kwenye swala la pumzi.
-Mazoezi ya kujinyoosha
kwa kufanya mazoezi ya kujinyoosha(stretching) kwa mwanamke mjamzito wa kipindi hiki cha mwisho kunaweza kumsaidia mwili wake kwa kuuweka katika hali nzuri ambapo hatopata maumivu ya viungo kama vile mgongo na mengineyo.
ANGALIZO!! Katika kipindi hiki cha ujauzito inashahuriwa yakwamba mwanamke mjamzito asifanye mazoezi ya tumbo hasa zoezi la crunches ili asijeakatengeneza madhara kwa mtoto aliyopo tumboni
Kama umeipenda andiko hili basi gonga NZURI na kwa maswali au maoni zaidi basi tuandikie baada ya andiko hili, na pia kama ungependa kusoma andiko jengine kama hili basi jisajili kwa kuweka anuani yako kwenye linki ya SUBSCRIBE.
Pia waweza tuandikia kwa email yetu Kuafit08@gmail.com
Kwa number yetu ya Tigo +255 653 009 477
Instagram account yetu (KUAFITI), Facebook-(kuafit) na twitter-(kuafit
0 comments:
Chapisha Maoni