latest Post

AINA ZA TAHAJUDI NA HATUA ZA KUCHUKUA WAKATI WA KUFANYA TAHAJUDI


 Kama nilivyoahidi kuwa nitaleta makala inayoelezea namna ya kufanya meditation au kwa kiswahili  Tahajudi lakin i kama hukusoma part 1 ya makala nakushauri uisome kwanza hapa (maana ya meditation(Tahajudi) na faida zake kiafya)  na kisha ufuatane nami katika makala hii

Kuna aina mbalimbali za kufanya tahajudi ambazo zitaleta faida katika kiakili na kiafya pia.Nitazungumzia aina mbili za tahajudi ambazo kwa wale ambao hawajawi fanya tahajudi itakuwa mwanzo mzuri kwao.

AINA ZA TAHAJUDI

1.TAHAJUDI YA PUMZI


Aina hii ni kongwe zaid na ilianza huko bara za Aisa katika nchi ya China na India, ni tahajudi nzuri sana  na ni muhimu kwa wale wanaoanza kujifunza binafsi huwa naifanya asubuhi na mapema baada ya kuamka.

Namna ya kufanya 
Tafuta eneno tulivu na ukae mkao ambao ni mzuri kwako ambao hautaleta kero yoyote.Anza kwa kuvuta pumzi ndani,ukianza weka akili kwenye pumzi, vuta pumzi taratibu na tulia kwa muda  kisha toa pumzi taratibu. Yaani unavuta pumzi, unakaa kidoogo kisha unaitoa taaratibu huku ukitazama jinsi hewa inavyoingia puani na kifua kikitanuka na hewa ikitoka na kifua kikishuka taaratibu.kwa wanaofanya mara ya kwanza utagundua akili yako inahama na kuwaza jambo lingine tena na kuacha kufikiria kwenye pumzi usijali wala usijilaumu au kuona umekosea, ni kitendo cha kawaida akili kuhama bila kujijua. Cha msingi irudishe tena akili yako  kwenye pumzi kama mwazoni. Endelea hivyo hivyo. Akili ikihama unairudisha kwenye pumzi.Unaweza ukavuta pumzi kwa kuhesabu namba moja mpaka 1o na ukarudia tena (ukivuta mara ya kwanza tunahesabu moja,ukivuta mara ya pili tunahesabu mbili na kuendelea) Kumbuka  ni muhimu kuvuta na kutoa pumzi kwa kina angalau mara tatu kabla ya kuanza kufanya tahajudi yoyote.


2.TAHAJUDI YA NAMBA


Hii ni aina nyingine ya tahajudi ambayo ni nzuri watu wanaoanza kufanya tahajudi. Katika ain hii unatakiwa kuhesabu namba kinyumenyume huku ukiwa umefumba macho yako. Unaweza ukaanzia 100, 99, 98, 97, 96, mpaka  ukafikia 1, au unaweza kuanzia 200, 198, 196, 194, 192, mpaka  ukafikia 2. Pia unashauriwa wakati unahesabu namba hizi usikose, na kama ikatokea ukakosea namba yoyote hata kama umekaribia kufika mwisho, itakulazimu kuanza upya. Tahajudi hii ni nzuri sana kwa kurekesbiha uwezo wa kumbukumbu katika akili yako, ingawa pia ina faida nyingine katika afya yako kiujumla.


Baada ya kujifunza aina kazaa za tahajudi ni vyema ukajua hatua za kufanya mazoezi ya tahajudi ili uweze kupata faida zake.Hatua hizi zitakuwezesha kufanya tahajudi kwa ufasha zaidi

HATUA ZA KUFANYA MAZOEZI YA TAHAJUDI


1.kuwa na utulivu

 Tafuta sehemu iliyotulia, isiyo na kelele. Kaa kwenye kiti au chini. Hakikisha huumii mahali popote. Legeza mwili wako pamoja na misuli yote ya mwili wako kwa kadri utakavyoweza.

2.Panga Muda mzuri wa kufanya Tahajudi.

Inawezekana tahajudi ifanye kazi kwako ama isifanye kazi kwako kutokana na maamuzi yako na mpangilio wako  wa muda utakavyokuwa. Jaribu kufanya kwa mda wa mwezi nina  maana  na hakika  utaanza kuona mabadiliko  , ingawa ni kidogo sana bali ni sawa na kuamua kufanya mazoezi kwa ajili ya afya ya mwili wako.Ni vyema ukapanga muda wako vyema wa kuanzia na kumalizia tahajudi yako.

3.Ni vyema ukaanza Kidogo Kidogo.

Ukianza ghafla kwa dakika 30 utafanya kama  unakimbia mbio za  kushindana  bila ya kufanya mazoezi yoyote.Anza kwa dakika chache tu kama dakika 5 halafu ongeza dakika taratibu kadiri siku zinavyozidi.Baadae utaanza kufika dakika 20 hadi 30


4.Tumia Andorid Application


Kwa wale wenye smart phone na wangependa  kusikiliza kitu  chochote wakati wa kufanya tahajudi, basi nawashauri watumie programu hii inaitwa insight timer 
 pakua hapa Insight App  ni njia nzuri ya kuanza nayo, itakufanya uweze kuwajibika.Utaweza kusikiliza  sauti zisizo na maneno, ziwe ni za vyombo(mdundo) tu.

5.Jitahid kutowaza mambo mengine wakati wa kufanya tahajudi

Sahau matatizo au changamoto zako unazozipitia sasa.Sahau matatizo yako ya kazini au nyumbani. Jitahidi usifikirie chochote wakati wa kufanya tahajudi.Ni vyema mawazo  na akili yako iwe sehemu moja tu wakati unafanya tahajudi.


Mwisho kabisa kwa wale wanaopenda kujifunza zaidi kuhusu tahajudi kuna kitabu kinaitwa "Wherever You Go, There You Are" kilichoandikwa na Jon Kabat-Zinn. Kitabu hiki kimeelezea meditation(tahajudi) kwa njia rahisi na ambayo unaweza kuanza kuifanya muda mfupi baada ya kukisoma na ukaanza kupata manufaa ya meditation(tahajudi).

kama utakuwa umeshindwa kukipata mitandaoni weka email yako au namba ya whatsapp  kwenye kipengele cha maoni(comments) nitakutumia.

Naimani umejifunza vitu vingi sana kuhusiana na tajahudi na utaanza mara moja kuifanyia kazi na kupata faida zake  kiakili na kiafya pia 

Kama umeipenda andiko hili basi gonga NZURI  na  kwa maswali au maoni zaidi basi tuandikie baada ya andiko hili, na pia kama ungependa kusoma andiko jengine kama hili basi jisajili kwa kuweka anuani yako  kwenye linki ya SUBSCRIBE.

Pia waweza tuandikia kwa email yetu Kuafit08@gmail.com 
Kwa number yetu ya Tigo +255 653 009 477  
Instagram account yetu  (KUAFITI), Facebook-(kuafit) na twitter-(kuafit

About Unknown

Unknown
Recommended Posts × +

0 comments:

KUPUNGUZA UZITO KWA MAJI YA BARIDI

Watu wengi katika jamii hupendelea kuoga na maji ya moto katika majira yote ya hewa lakini kutokana na utafiti uliofanywa na wanasayansi kam...