latest Post

NJIA 4 ZA KUPUNGUZA UNENE HARAKA KWA KUPUNGUZA HOMONI YA INSULINI

 


Watu wengi hudhani kwamba kwa kula vyakula vya mafuta na wanga pekee hupelekea mtu kuongezeka mwili na hivyo hudhani kwa kupunguza ulaji wa vyakula hivi ndio sababu pekee ya kupunguza mwili. Dhana hii ni robo ya ukweli ukizingatia kwamba kuongezeka kwa mwili huchangiwa zaidi na homoni hasa Insulin. Insulin ndio homoni ambayo hufanya kazi ya kubadilisha chakula hasa wanga ndani ya mwili kutumika kama chanzo cha nguvu na husaidia misuli ya mwili kufyonza wanga huo kwenye sehemu mbalimbali za mwili Kama vile misuli ya mikono na pia kwenye Ini.



Kiwango cha insulin mwilini huashiria kiwango Cha unene wa mtu na pia huweza kutambuliwa kutokana na  kuwa na tumbo(kitambi) pamoja na ukubwa wa maeneo ya Kati ya mwili mfano: kiuno na mgongo wa chini. Watu wengi Hawa wenye matatizo yanayohusiana na kisukari cha aina ya pili hasa(Diabetes type 2) huwa na kiwango kikubwa cha insulin na kiashiria kikubwa ni kuwa na tumbo kubwa.


Hivyo basi mtu akitaka kupunguza unene na uzito napaswa kufahamanu yakwamba anapswa kupunguza kiwango cha insulin mwilini, na jambo hilo linawezekana kwa kufanya Mambo yafwatayo


1. Kubadili mpangilio wa ulaji na hapa hasa kwa kupunguza kiwango cha wanga na kupunguza idadi mlo mtu anakula kwa siku. Vyakula vya wanga husababisha kiwango cha insulin kuongezeka na hivyo kwa kupunguza wanga utaulazimisha mwili kuzalisha kiwango hicho cha insulin kuwa kidogo. Mtu akiweza kupunguza idadi mlo(KUFUNGA ) itaulazimu mwili kutumia mafuta yaliyojiifadhi kwenye mwili Kama chanzo cha nguvu hivyo kupunguza unene wa mtu.



2. Kupunguza msongo wa mawazo husaidia mwili kupunguza uzalishaji wa homoni ya cortisol ambayo huchangia homoni ya insulin kuzalishwa kwa wingi na hivyo kupelekea mwili kuongeza Kasi ya uhifadhi wa wanga kwa njia ya mafuta. Njia za kupunguza mawazo ni pamoja na kufanya mazoezi ya tahajudi na hata pia kujishughulisha na shughuli mbalimbali kama vile michezo.



3. Kufanya mazoezi ni njia moja wapo ambayo husaidia mwili kutumia nguvu kubwa iliyopokwa mfumo wa wanga bila kutumia homoni ya insulin. Kwa kufanya mazoezi ya kutumia uzito(weight training/strength training) angalau mara tatu (3) kwa wiki na mazoezi makali ya pumzi(HIIT)) Mara mbili(2) kwa wiki kutasaidia mtu kuchoma wanga uliyojifadhi Kama mafuta kwenye mwili na kupunguza uzalishaji wa homoni ya insulin.



4. Kupata mda mrefu wa kupumzika ni kigezo kikubwa Sana cha kupata matokeo mazuri hasa kwenye swala la kupunguza mwili. Mwili unapopumzika hasa kwanzia masaa sita(6) hadi nane(8) huongeza kiwango cha homoni ya ukuaji(Growth hormone) ambayo kazi yake hasa ni kujenga misuli na katika uzalishwaji wake homoni ya insulin huzalishwa kwa kiwango kidogo.

Kama umeipenda andiko hili basi gonga NZURI  na  kwa maswali au maoni zaidi basi tuandikie baada ya andiko hili, na pia kama ungependa kusoma andiko jengine kama hili basi jisajili kwa kuweka anuani yako  kwenye linki ya SUBSCRIBE.

Pia waweza tuandikia kwa email yetu Kuafit08@gmail.com 


Kwa number yetu ya Tigo +255 653 009 477  


Instagram account yetu  (KUAFITI), Facebook-(kuafit) na twitter-(kuafit)

About Kuafit

Kuafit
Recommended Posts × +

0 comments:

KUPUNGUZA UZITO KWA MAJI YA BARIDI

Watu wengi katika jamii hupendelea kuoga na maji ya moto katika majira yote ya hewa lakini kutokana na utafiti uliofanywa na wanasayansi kam...