latest Post

MADHARA YA KUZIDISHA KWANGO SAHIHI CHA MAZOEZI

 


Kuna baaadhi ya watu ambao wanafanya mazoezi kwa kupita kiasi,kwa maana hiyo hufikiria kufanya mazoezi kwa muda unaozidi lisaa limoja na nusu ndio utakuwa unapunguza uzito ama kujenga misuli na wengine hudiriki kufanya mara saba kwa wiki tena sio chini ya masaa mawili.
Hii siyo sahihi kwa sababu mwili wa binadamu unahitaji muda wa kupumzika na kuupa nafasi ya kujenga misuli ya mwili kwa mpangilio ulosahihi kutokana na maumbile yake.
Muda maalum unaotakiwa kufanya mazoezi usizidi saa moja na nusu hasa unapofanya mazoezi mangumu kama kunyanyua uzito(vyuma) chini ya hapo ni pale unapofanya mazoezi ya pumzi kama kukimbia, aerobics, kuruka kamba na kadhalika na ikiwa imepungua sana ni dakika 20 kwa siku mara tano kwa wiki,hii inasaidia kupunguza kaloriz ambazo hazihitajiki mwilini.Kwani Mara nyingi binaadamu hupata kaloriz 800 hadi 1500 kwa siku kutokana na chakula anachokula hii humsaidi awe na afya njema na kutokuwa namaradhi yanayosababishwa na mafuta kwa wingi mwilini.
Madhara wanayopata wale wanaofanya mazoezi kwa muda mrefu bila ya kupumzika.


muonekano uliochoka

  • Kuwa na muonekano wa uchovu hasa katika maenei ya sura. Muda wote huonekana kuzeeka hararaka, sura kukunjamana na macho kuingia ndani



  • Kutengeneza matatizo ya afya Kama matatizo ya moyo. Mtu anayefanya mazoezi kwa kuzidisha kiwango nirahisi kuufanya moyo kuzidisha kazi unaofanya wa kusambaza damu mwilini hivyo kupelekea misuli yake(moyo) kutanuka ili kuwezesha damu kusambazwa kwa wingi na hivyo kupunguza ufanisi wa moyo kutanuka na kupelekea mapigo ya moyo kubadilika na hata kusimama



  • Kutopata matokeo mtu anayoyatamani; kwa kuongeza kiwango Cha mazoezi ni rahisi sana kuuchosha mwili na kuupelekea kuzalisha Homoni iitwayo Cortisol(stress hormone) ambayo huzalishwa kwa wingi endapo mtu anapitia kipindi kigumu Kama uchovu uliopitiliza ama msongo wa mawazo. Homoni hiyo ulazimu mwili kuhifadhi chakula kwa mdumo wa mafuta na kupelekea unene.



  • Kupunguza ufanisi wa mwili kufanya kazi na shughuli zingine za maisha. Mwili uliochoka Sana hushindwa kuzingatia na kufanya kazi kwasababu huwa dhaifu na usio na nguvu, na hata pia inasadikika kwamba watu wengi wenye hali hii hupelekea watu kuwa na msongo wa mawazo.



  • Hupunguza ufanisi wa tendo la ndoa kwa wanaume. Wanaume wengi wanaozidisha mazoezi ama shughuli zingine zinazotumia nguvu hulalamika kutokuwa na hamu ya tendo la ndoa(low libido libido).Hivyo inashauriwa watu kupunguza kiwango Cha mazoezi na kutafuta mdawakutosha ili kupumzika.

Epuka kuzidisha mazoezi na pata muda wa kuupumzisha mwili ili kujenga seli mpya za mwili.
Kama umeipenda andiko hili basi gonga NZURI  na  kwa maswali au maoni zaidi basi tuandikie baada ya andiko hili, na pia kama ungependa kusoma andiko jengine kama hili basi jisajili kwa kuweka anuani yako  kwenye linki ya SUBSCRIBE. 
Pia waweza tuandikia kwa email yetu Kuafit08@gmail.com 

Kwa number yetu ya Tigo +255 653 009 477  

Instagram account yetu  (KUAFITI), Facebook-(kuafit) na twitter-(kuafit)

About Kuafit

Kuafit
Recommended Posts × +

0 comments:

KUPUNGUZA UZITO KWA MAJI YA BARIDI

Watu wengi katika jamii hupendelea kuoga na maji ya moto katika majira yote ya hewa lakini kutokana na utafiti uliofanywa na wanasayansi kam...