latest Post

UMUHIMU WA KUPUMZIKA NA KUPATA USINGIZI WA KUTOSHA Ni kweli kwamba watu wengi bado hawajui umuhimu wa kuwa na mapumziko katika maisha yao. Hivyo inapelekea kukosa faida nyingi kama wangeamua kupumzika vya kutosha katika shughuli zao za kila siku.

 wakati betri ya simu au tablet inapokuwa na kiwango kidogo cha umeme(charge), huwa tunaiweka kwenye charge ili ipate umeme zaidi.Watu wengi hatujui tunaweza kufanya hivyo kwa ajili yetu wenyewe kwa kuwa na mapumziko katika shughuli zetu za kila siku.karibu asilimia 67 a watumiaji wa simu wanakubali kwamba wanaangalia simu zao hata kama hakuna ujumbe, na asilimia 44 wanalala karibu na simu zao kulingana na utafiti uliofanywa (mobile technology fact sheet).

Ili kuweza kuendelea na shughuli zetu hata kama tumechoka, huwa tunaishia kutumia  stimulants kama kahawa na baadhi ya vinywaji(energy drinks) ambavyo vinapatikana kila mahali.


ikiwa unahitaji msukumo mdogo wa kupumzika hapa kuna faida 5 za kumpumzika zitakazo kushangaza.


1.kuweza kutatua matatizo kwa ufasaha.

Ubongo unapopata muda mzuri wa kupumzika,uchochea mtandao mpya katika ubongo kwa kuruhusu vipande  vya habari kuunganishwa kwa njia mpya na tofauiti.Hivyo kuuwezesha ubongo kuchanganua matatizo au changamoto kwa ufasaha na kupata utatuzi sahihi.
Sara Mednick, mwandishi wa kitabu cha "Take a Nap, change your life" anasema "Tunahitaji kupumzika. Tunahitaji kuchukua mapumziko zaidi. Kwa sababu, kuwa na  mapumziko ni sehemu ya maisha. Ni sehemu ya kuwa hai, ni sehemu ya kuwa na uzalishaji na pia ni sehemu ya kuwa wabunifu, ni sehemu ya kuwa na furaha"


2.kuboresha uwezo wa kukumbuka

Ukosefu wa usingizi unaweza kufanya iwe vigumu kwako kuzingatia na kuhifadhi habari au matukio husika.Unapokuwa usingizini, ubongo wako unaupa nafasi ya kupitia shughuli zote na hisia za siku husika ambapo ni muhimu kwa uundaji wa kumbukumbu katika ubongo wako, hivyo kukuwezesha kukumbuka mambo yako wa urahisi.Hivyo unashauriwa kulala angalau masaa 6 mpaka 7 kwa siku.

3.kupunguza msongo wa mawazo

Msongo wa mawazo umekuwa changamoto kwa watu wengi, watu wengi wameishia kuwaza muda wote bila kupata majibu ya changamoto zinazowakabili.unapoamua kupumzika vya kutosha kunaweza kupunguza kiwango cha msongo wa mawazo na kuboresha afya yako ya akili na mwili wako.


4.Husaidia kufanya maamuzi yaliyo sahihi.

Si jambo la kushangaza kwamba unapokuwa katika msongo wa mawazo, uwezo wako wa kufikiri kwa usahihi unakuwa upo katika kiwango cha chini sana. Hivyo upelekea kufanya maamuzi ambayo sio sahihi na kuja kujutia baadaye.Watu wasio na msongo wa mawazo huwa na uwezo mkubwa wa kuzingatia maamuzi yao vyema na wanaweza kupuuza dhamira ya uamuzi ambao wanakaribia kufanya.


5.kulinda afya ya moyo wako

Utafiti wa mwaka 2010 uligundua kwamba protini ya C-reactive, inayohusishwa na hatari ya mashambulizi ya moyo, ilikuwa ya juu kwa watu ambao walilapata usingizi wa  masaa sita au machache zaidi.Utafiti huo unaonyesh kwa kupumzika vya kutosha uleta faida kubwa katika afya ya moyo. Mkazo(msongo wa mawazo) ni hatari  kwa afya ya moyo wako ukiachilia sababu zingine kama shinikizo la damu na ukosefu wa mazoezi, na mshtuko wa ghafla(shock) unaweza kusababisha kupasuka kwa adrenaline ambayo unasaidia moyo kufanya kazi kwa usahihi.

Faida zingine ni
(a)kupunguza shinikizo la damu
(b)husaidia kuwa na hisia za utulivu na ujasiri
(c)kuboresha uwezo wa kukabiliana na jambo
(d)kupunguza maumivu(magonjwa ya muda mrefu)
(e)Kupunguza wasiwasi na hali ya huzuni

Hata katika vitabu vya dini vinaonyesha Mungu mwenyewe alipumzika baada ya kufanya kazi za uumbaji siku sita.  Hivyo basi unahimizwa kwanzia leo  uwe na utaratibu wa kupumzika vya kutosha na kupata usingizi wa kutosha kwa ajili ya afya ya mwili wako na akili yako.hapa kuna videkezo vichache va kuanzia

1.pangilia muda wako mzuri wa kulala(kupata usingizi wa kutosha)
2.weka siku maalumu ya kupumzika wewe pamoja na familia yako,ndugu na jamaa zako,
3.fanya shughuli ambazo zinaweza kukuchangamsha kama vile kwenda cinema/kuangalia movies/vichekesho au kushiriki katika michezo mbalimbali.

Kama umeipenda andiko hili basi gonga NZURI  na  kwa maswali au maoni zaidi basi tuandikie baada ya andiko hili, na pia kama ungependa kusoma andiko jengine kama hili basi jisajili kwa kuweka anuani yako  kwenye linki ya SUBSCRIBE.
Pia waweza tuandikia kwa email yetu Kuafit08@gmail.com 

Kwa number yetu ya Tigo +255 653 009 477  

Instagram account yetu  (KUAFITI), Facebook-(kuafit) na twitter-(kuafit)


About Davis David

Davis David
Recommended Posts × +

DIET YA KUTOA SUMU MWILINI NA KUPUNGUZA UNENE KWA HARAKA

Habari zenu wadau wa KUAFIT! leo tutaongelea kuhusiana na elimu ya lishe ambayo itahusiana na diet ambapo tutaelezea mambo mengi san...