Watu wengi wakiwa wanafanya mazoezi ya kujenga misuli hupuuza umuhimu wa kuzingatia ukubwa wa mwili na hivyo hupelekea mtu kutopata matokeo mazuri na hata pia kutokuona matokeo kabisa
Inafahamika kwamba Kuna aina 3 ya miili ikiwemo
- Ectomorph - ni aina ya mwili ambapo mtu huwa mwembamba na hujaza misuli lakini kwa shida na kwa kazi kubwa
- Mesomorph - ni aina ya mwili wa wastani ambapo mtu huweza kuongeza misuli kirahisi ukilinganisha na makundi mengine
- Endomorph - Aina hii ya mwili huwa mkubwa na mwili wa haina hii huwa ni mrahisi kuongezeka kutokana na seli za mafuta hivyo kupelekea mtu kuwa mnene asipokuwa mwangalifu
Hivyo ufanywaji wa mazoezi wa watu lazima utofautiane hasa kwenye swala la unyanyuaji wa vyuma vizito na mazoezi ya cardio(mazoezi ya kujenga pumzi na kupunguza mwili kama kukimbia nakadhalika) kamaifwatavyo-
- Ectomorph - Kwenye ufanyaji wa mazoezi wa mtu wa kundi hili hulazimika kufanya mazoezi ya kunyanyua uzito kwa kiasi kikubwa kuliko mazoezi ya cardio. Endapo mtu wa kundi hili ataongeza mazoezi ya cardio kuliko ya kunyanyua uzito basi mwili wake utapungua Sana. Mtu wa kundi hili hupaswa kufanya mazoezi ya kunyanyua uzito angalau mara tano (5) hadi sita (6) kwa wiki na mda usiopungua lisaa na robo.
- Mesomorph - Watu wa kundi hili huwa urahisi mkubwa Sana kwenye kuongezeka misuli kuliko kundi lingine. Hivyo mtu wa kundi hili hushauriwa kufanya mazoezi kulingana na mahitaji yake ikimaanisha Kama anatamani kuwa na mwili mkubwa Sana atalazimika kufanya mazoezi kwa mda wa lisaa na nusu lakini endapo atakuwa na hitaji lakuongezeka kidogo basi atapaswa kutofanya mazoezi kwa mda wa lisaa kwa siku na ni kwa siku nne(4) hadi tano (5) ndani ya wiki. Ufanywaji wa cardio utategemea na kiwango cha mafuta aliyokuwa nacho na kwa maranyigi huwa ni kiwango cha kawaidi hivyo inawezekana ikawa Mara tatu (3) hadi nne (4) wiki.
- Endomorph - kundi hili la watu hulazimika kufanya mazoezi ya cardio na kunyanyua uzito kwa viwango sawa maana watu Hawa huwa na seli za mafuta nyingi. Ufanyaji wake wa mazoezi hautofautiani na mesomorph kwenye unyajuaji uzito Bali kwenye mazoezi ya cardio ambapo watu wa kundi hili hulazimika kufanya mazoezi ya cardio sio chini mara sita (6) kwa wiki na kwa dakika thelathini (30) kwa siku
Mambo haya ndio yamsingi Sana kuzingatia pamoja na mlo sahihi ili kupata matokeo mzuri.
Kama umeipenda andiko hili basi gonga NZURI na kwa maswali au maoni zaidi basi tuandikie baada ya andiko hili, na pia kama ungependa kusoma andiko jengine kama hili basi jisajili kwa kuweka anuani yako kwenye linki ya SUBSCRIBE.
Pia waweza tuandikia kwa email yetu Kuafit08@gmail.com
Kwa number yetu ya Tigo +255 653 009 477
Instagram account yetu (KUAFITI), Facebook-(kuafit) na twitter-(kuafit)
0 comments:
Chapisha Maoni