latest Post

FAHAMU FAIDA ZA ASALI KATIKA AFYA YAKO


Asali ni chakula kitamu katika hali kiowevu kinachotengenezwa na nyuki.Nyuki hula mbelewele pamoja na maji matamu ndani ya maua na kuitoa tena katika mzinga wa nyuki kwa kuitunza kwenye sega. Ndani ya sega kiowevu huiva kuwa asali kamili.

Asali inavunwa na watu mbalimbali duniani kote na kuwa chakula muhimu sana katika maisha yetu. Asali husaidia katika kujenga afya zetu. Kipindi cha miaka ya zamani katika nchi za kaskazini ilikuwa njia ya pekee ya kutia utamu kwenye chakula kabla ya kupatikana kwa sukari kwa njia ya biashara ya kimataifa.


Asali imesheheni madini mengi sana yanayohitajika mwilini,yakiwamo ya magenisium na potassium. Kwa asili yake hiyo asali husaidia kusisimua vichocheo vya mwili.
Asali ni chakula muhimu sana katika  afya ya miili yetu kwani inaweza kutumika kama kinga pia kama dawa zidi ya magonjwa mbalimbali.


ZIJUE FAIDA  ZA ASALI KATIKA AFYA YAKO


1.Kwa wanaosumbuliwa na kikohozi mara kwa mara  wanashauriwa kutumia asali kwa kuichanganya na limao kwenye chai,machanganyiko huu husaidia kutibu kikohozi na maambukizi kwenye mfumo wa hewa.

2.katika utunzaji wa ngozi asali yao uweza kusadia kuondoa au kuponya kwa chunusi na kuifanya ngozi ya sura yako kuwa laini.Unashauriwa  kufanya mask ya asali usoni kwa muda wa masaa kadhaa ili ifanye kazi vizuri.

3.Katika afya ya akili chakula hiki cha asali huwa na msaada mkubwa kwani uongeza uwezo wa akili kujifunza,kufikiri na kutunza kumbukumbu.Kwa wale wanaosumbuliwa na hali ya kusahau sahau wanashauriwa kutumia asali mara kwa mara.

4.Asali usaidia kuzuia mtu kutapika ikiwa itachanganywa vizuri na tangawizi.Pia ni msaada mkubwa kwa mama mjamzito.

5.Kwa wale wanaosumbuliwa na kiungulia wanashauriwa kutumia asali mara kwa mara kwa kuichanganya pamoja na maziwa.

6.Asali husaidia kuua fangasi mwilini kwani ina kemikali ya hydrogen peroxide ambayo husaidia kuua fangasi mwlini.

7.Kula asali mara kwa mara husaidia kuboresha kinga ya mwili na kuimarisha mfumo wa chakula na pia husaidia damu kufanya kazi vizuri.

8.Asali ina kemikali za flavonoid na antioxidants zinazosaidia kuzuia magonjwa ya moyo na saratani.

Hizi ni faida chache tu zinatoka na chakula aina ya asali.Kama nilivyosema hapo mwanzo asali husaidia kutukinga na kutibu magonjwa mbalimbali kama vile  kuwa hali ya uchovu wa mwili,uzito mkubwa,bakteria wanaosababisha harufu mbaya ya kinywa,maumivu ya jino,mafua, maradhi ya moyo na pia tatizo la mchafuko wa tumbo utokanano na wingi wa gesi.

Ni matumaini yangu baada ya kufahamu faida chache za chakula hiki cha asali,utaanza mara moja kukipa kipaumbele mara kwa mara katika milo yako ya kila siku.Kumbuka unapoenda kununua asali kuwa makini kwani kuna asali zingine ni feki ambazo ukiitumia hutapata faida nilizotaja  hapo juu na pia inaweza ikaleta madhara katika mwili wako.

Kama umeipenda chapisho hili basi gonga NZURI  na  kwa maswali au maoni zaidi basi tuandikie baada ya andiko hili, na pia kama ungependa kusoma andiko jengine kama hili basi jisajili kwa kuweka anuani yako  kwenye linki ya SUBSCRIBE.

Pia waweza tuandikia kwa email yetu Kuafit08@gmail.com 
Kwa number yetu ya Tigo +255 653 009 477  
Instagram account yetu  (KUAFITI), Facebook-(kuafit)

About Davis David

Davis David
Recommended Posts × +

DIET YA KUTOA SUMU MWILINI NA KUPUNGUZA UNENE KWA HARAKA

Habari zenu wadau wa KUAFIT! leo tutaongelea kuhusiana na elimu ya lishe ambayo itahusiana na diet ambapo tutaelezea mambo mengi san...