latest Post

MUDA SAHIHI WA KULA MATUNDA NI UPI?


katika maisha yetu watu wengi wamejiwekea utaratibu wa kula matunda kila mara na hili ni jambo jema kabisa.Utaratibu  huu uliozoeleka ni kuanza kula chakula cha kawaida hasa mchana na jioni na mwisho kula matunda aina mbalimbali.Unakuta mtu anakula wali nyama na mwishoni anamalizia na tunda aina ya ndizi au embe, utaratibu huu umekuwa wa kawaida hata katika sehemu za sherehe mbalimbali iwe harusi au kwenye tafrija  mtu anachukua chakula mwishoni anabeba na kipande cha ndizi au tikiti maji.Mara nyingine unakuta mtu anakula chakula pamoja na tunda kwa wakati mmoja mfano unakula wali unakata ndizi kidogo hadi unamaliza kula.

SWALI: je utaratibu huu hudhihirisha faida ya matunda wakati wa kula katika miili yetu                           ipasavyo??

Jibu ni HAPANA utaratibu huu sio sahihi kabisa kwa ulaji wa matunda na kupata  faida zake mwilini.Hayo ni makosa miongoni mwa makosa mengi yanayofanyika kwa sababu ya mazoea tu.Hivyo ushauriwi kula kwanza chakula mwishoni ukala matunda kwanza.

Swali je ni muda gani mzuri wa kula matunda??


MUDA SAHIHI WA KULA MATUNDA

1.Kula matunda tumbo likiwa tupu


Unashauriwa kula matunda kwanza kabla hujatia chakula kingine tumboni. Matunda hayaliwi baada ya mlo kama ilivyozoeleka na watu wengi. Unapokula matunda katika hali hii, matunda husagika haraka na virutubisho vyake husambaa mwilini kwa urahisi. na kufanya kazi yake ipasavyo kama vile kusafisha mfumo wa damu (detoxification) na kuupa mwili nguvu.Baada ya saa moja au zaidi, unaruhusiwa kula mlo wako mwingine kama kawaida.

SWALI:ukila matunda baada ya kula nini kinatokea?

Jibu ni kwamba ulaji wa matunda baada ya mlo siyo sahihi kwa sababu matunda huyeyuka haraka kuliko chakula cha kawaida unachokula. Tunda linapokuwa tayari kupita tumboni kuelekea kwenye utumbo mwembamba, huwa  linazuiliwa na chakula ulichokula. Baada ya muda tunda linachanganyika na chakula na kuoza na hatimaye kuzalisha asidi  ambayo humfanya mtu kuumwa tumbo baada ya kula matunda. Lakini pia virutubisho sahihi katiba matunda uliokula baada ya chakula hupotea.

Baadhi ya watu wanapokula tunda au kunywa juisi huku wakila pamoja na chakula matumbo yao huanza kuunguruma na hata kuuma na kujisikia kwenda chooni. Hii hutokea hasa wanapokula ndizi mbivu. Hiyo yote inatokana na kuchanganya chakula na matunda. Hali hii inaweza kuepukwa kama matunda yataliwa kwanza kabla ya chakula kingine.


2.Kula matunda masaa mawili baada ya kula chakula 


Njia nyingine kama njia ya kwanza itakuwa ngumu kwako kula matunda tumbo likiwa tupu unashauriwa kula matunda baada ya kupita masaa mawili baada ya kula chakula chako iwe asubuhi mchana au jioni.


3.Kula matunda kabla ya mazoezi


Muda mwingine mzuri wa kula matunda ni kabla ya kufanya mazoezi.Unapokula matunda kabla ya mazoezi unaupa mwili wako nishati(nguvu) za kukuwezesha kutekeleza mazoezi yako na pia kujaza viwango vya nishati vilivyoondolewa baada ya kufanya mazoezi.Matunda unayoshauriwa kula kabla ya mazoezi ni ndizi pamoja na maembe.


pia unashauriwa kula  matunda na nyama zake, kama vile chungwa, ni bora zaidi kuliko kunywa juisi yake kwani nyama za matunda hayo zina kambalishe (fibres) muhimu zenye faida nyingi mwilini. Unywapo juisi, kunywa taratibu kwa kujaza mdomoni ili juisi ipate nafasi ya kuchanganyikana na mate yako kabla ya kumeza.

Kama umeipenda chapisho hili basi gonga NZURI  na  kwa maswali au maoni zaidi basi tuandikie baada ya andiko hili, na pia kama ungependa kusoma andiko jengine kama hili basi jisajili kwa kuweka anuani yako  kwenye linki ya SUBSCRIBE.

Pia waweza tuandikia kwa email yetu Kuafit08@gmail.com 
Kwa number yetu ya Tigo +255 653 009 477  
Instagram account yetu  (KUAFITI), Facebook-(kuafit) 

About Unknown

Unknown
Recommended Posts × +

0 comments:

KUPUNGUZA UZITO KWA MAJI YA BARIDI

Watu wengi katika jamii hupendelea kuoga na maji ya moto katika majira yote ya hewa lakini kutokana na utafiti uliofanywa na wanasayansi kam...