latest Post

NAMNA KUWA NA FURAHA INAVYOBORESHA AFYA YAKO


"Furaha ni maana halisi  na kusudi la maisha, ni mjumuisho wa kusudi la kuwepo kwa mwanadamu"
mwanafalsafa Aristotle alisema maneno haya zaidi ya miaka 2000 iliyopita and mpaka sasa bado yanaukweli ndani yake.Furaha ni mada pana ambayo inaelezea kuwa na  hisia nzuri (positive emotion)  kama vile kutosheka na kuridhika.Tafiti nyingi zinaonyesha kuwa mtu mwenye  furaha  haikufanyi ujisikie vizuri tu bali huleta faida kubwa katika afya yako.

Furaha na Afya njema  huwa vinaendana pamoja, tafiti za kisayansi zinaonyesha  kuwa na furaha huleta faida katika afya ya moyo na kuboresha mfumo wa kinga mwilini na kuishi maisha marefu.
Pia inaonyesha kuwa  na furaha husaidia kupata usingizi mzuri ambao utakuwezesha kuwa na uwezo mzuri wa kufikiri,uzalishaji bora katika kazi zako pamoja na kuwa na uzito wa wastani.

utafiti uliofanyika kwa watu wazima 700  unaonyesha asilimia 47 ya watu wote walikuwa na matatizo ya kupata  usingizi na kuwa na usingizi wa kukatika katika mara kwa mara  kutoka na kuwa na  kukosa hali nzuri ya kuwa na furaha.

SABABU ZA KUWA NA FURAHA ILI kUBORESHE AFYA YAKO

1.Kuboresha  mfumo wa kinga mwilini


Kuwa na mfumo mzuri wa kinga mwilini ni jambo la muhimu sana kwa sababu hutusaidia kutukinga na magonjwa mbalimbali.Tafiti zinaonyesha kuwa na furaha mara kwa mara husaidia kuboresha nguvu ya kinga mwilini na kupunguza kupata magonjwa ya mafua pamoja maambukizi ya kifua.


2. Husaidia kulinda Moyo wako


Furaha huchangia pia katika  kuboresha afya ya moyo wako wa kupunguza presha ya damu ambayo huchangia  mtu kupata magonjwa ya moyo.Utafiti uliofanyika kwa watu 6500 wenye zaidi ya miaka 65 ulionyesha watu wenye hali nzuri na furaha walikuwa   na  asilimia 9 ya kuwa na presha ya damu ya kiwango cha juu (high blood pressure)
Pia kuwa na furaha uchangia kupunguza kupata magonjwa mbalimbali ya moyo ambayo husababisha vifo vingi duniani.

3.Kurefusha maisha.


Mara nyingi watu ambao huwa na furaha huishi kwa muda mrefu hapa duniani.Hi uchangiwa na hali  kujihusisha katika shughuli mbalimbali ambazo huboresha afya zao.Mfano kupenda kufanya mazoezi.

4.Kupunguza msongo wa mawazo

Kuwa mtu wa furaha pia husaidia kupunguza kuwa na msongo wa mawazo. Kikawaida mtu mwenye msongo wa mawazo  huchangia kudhoofisha  afya ya mwili na kupata magonjwa mbalimbali kama vile type 2 diabetes na  kuwa na presha ya damu ya  kiwango cha juu (high blood pressure).

5.Kupunguza maumivu 


Kuwa na furaha katika nyakati tofauti  pia husaidia kupunguza hali ya kujisikia maumivu mwilini. furaha husaidia kupunguza hali ya kuwa na  maumivu sugu (chronic pain) ambayo hushambulia sehemu za muunganiko(joint) kitaalamu  inaitwa arthritis.


Baada ya kujua faida za kuwa na furaha ni vyema ukajua na namna gani ukaanza  kuongeza hali ya kuwa na furaha katika maisha yako ambayo itaboresha afya yako.

1.Fanya mazoezi

Mazoezi aina ya Aerobic au Cardio huchangia sana mtu kuwa na furaha.Kupenda kutembea (dakika 30) au kucheza mchezo unaopenda  haitachangia kuboresha afya yako  ya mwili pia itaboresha kuwa na hali nzuri na furaha zaidi

2.Pumzika vya kutosha

kukosa usingizi wa kutosha uchangia mtu kukosa furaha .Unashauriwa kupata muda mzuri wa kupumshiza mwili na akili yako, hii husaidia mwili na akili yako kufanya kazi vizuri pale unapoamka asubuhi.


3.Fanya Tahajudi(meditation)

kufanya tahajudi mara kwa mara huchangia kuongeza hali ya kuwa na furaha katika maisha yako,pia huchangia kupunguza hali ya kuwa na msongo wa mawazo.Kama hujuia namna ya kufanya tahajudi soma makala hii  aina za tahajudi

4.Kula chakula bora 

Unashauriwa kutokula chakula bila mpangilio maalumu kwani husababisha afya yako kuzorota.Tafiti zinaonyesha ulaji wa matunda na mboga za majani mara kwa mara uchangia mtu kuwa na hali ya furaha

5.kuwa mtu wa shukrani

Hali ya kushukuru kwa yale mema yalitokea katika maisha yako  uchangia kiasi kikubwa kuwa na furaha.Njia  mojawapo ya kukuwezesha kuonyesha hali ya shukrani ni kuandika mambo matatu  yaliyochangia kuwa na hali nzuri katika siku hiyo.

Kama umeipenda chapisho hili basi gonga NZURI  na  kwa maswali au maoni zaidi basi tuandikie baada ya andiko hili, na pia kama ungependa kusoma andiko jengine kama hili basi jisajili kwa kuweka anuani yako  kwenye linki ya SUBSCRIBE.

Pia waweza tuandikia kwa email yetu Kuafit08@gmail.com 
Kwa number yetu ya Tigo +255 653 009 477  
Instagram account yetu  (KUAFITI), Facebook-(kuafit) 

About Davis David

Davis David
Recommended Posts × +

DIET YA KUTOA SUMU MWILINI NA KUPUNGUZA UNENE KWA HARAKA

Habari zenu wadau wa KUAFIT! leo tutaongelea kuhusiana na elimu ya lishe ambayo itahusiana na diet ambapo tutaelezea mambo mengi san...