latest Post

TAMBUA VYAKULA VINAVOIMARISHA AFYA YA NGOZI YAKO


Siku zote katika maisha njisi unavyoonekana ni matokeo ya lishe yako ya kila siku.Tangu unapokula asubuhi mpaka jioni huamua afya ya mwili wako iweje.Hivyo basi hata katika swala zima la afya ya ngozi yako inategemea unakula nini.Kumbuka chakula unachokula kinaweza kikajenga afya yako na kuwa imara au kudhorota afya yako na kuwa dhaifu.

Afya ya ngozi yako ni sehemu moja muhimu sana kuipa umakini.Watu wengi huwa hawajui siri iliyopo katika vyakula tunavyokula katika kuboresha au kubomoa afya ya ngozi zetu.Baadhi ya watu huwa wanaangaika kutafuta  mafuta ya kikemikali kuhakikisha ngozi zao zinakuwa vizuri pasipo kutambua kile wanachokula ndio kitaamua afya ya ngozi yako iwe katika hali gani. Leo nataka nikufumbue macho katika hili ili ufahamu umuhimu wa vyakula tunavyokula katika afya ya ngozi zetu.

Wataalamu wa afya wanasema kila kitu tunachokula ni sehemu ya miili yetu ikiwa ni pamoja na muonekano wa nje(ngozi).Hivyo kadiri utakavyoendelea kula chakula bora ndivyo afya ya ngozi yako itazidi kuimarika zaidi.

Vyakula tunavyokula vinaweza kuchangia katika muonekano wa ngozi zetu na kusaidia kupambana na maradhi mbalimbali ya ngozi mfano kupunguza mikunjano ya uso na suala zima la afya na muonekano wa ngozi.


Hivyo basi tambua vyakula hivi ambabyo  vinaweza kusababisha kudhorota kwa afya
ya ngozi yako


1.Chumvi 


Matumizi ya chumi yapo kila siku katika vyakula tunavyokula hasa mida ya mchana na jioni hivyo ni muhimu kuzingatia kiwango cha chumvi kinachoitajika.Chumvi yenye madini ya iodine ni hatari kwa afya ya ngozi yako,husababisha chembechembe za nyama yako katika ngozi kuvimba.

2.Sukari 


Sukari huwa inatumiwa na watu wengi kila siku katika vyakula mbalimbali,lakini kiwango cha sukari kikiwa kingi husababisha ngozi kuwa kavu na kufanya mwili kutengeneza makunyazi kwa sababu inaharibu kemikali ya collegen na elastin zinazofanya kazi ya matengenezo ya ngozi.


3.Nyama Nyekundu 


Nyama nyekundu ni chanzo mojawapo cha kudhoofisha afya ya ngozi yako endapo utakuwa unaila sana(mara kwa mara).Nyama nyekundu ina kemikali ya carnitine ambayo inafanya mishipa ya damu kukakamaa na kusababisha ngozi kuanza kuzeeka.


4.Vyakula vya kukaangwa


Vyakula hivi vimetokea kupendwa na watu wengi sana hasa maeneo ya mijini, vyakula kama chipsi, nyama za kukaanga n.k .Vyakula hivi huweza sababisha  mafuta mengi kujaa mwilini hasa sehemu za ngozi na kusababisha uzibaji wa vijitundu vidogo vidogo vilivyopo katika ngozi yako.

5.Unywaji wa kahawa 


katika kahawa huwa kuna kemikali ya caffeine ambayo usababisha ukosefu wa maji ya kutosha katika ngozi yako na kuifanya kuwa kavu wakati wote.Pia kemikali hii ya caffeine husaidia kutengeneza kimekali ya cortisol inayosababisha  ngozi kuzeeka mapema.


Swali:Je kuna vyakula vinavyoweza kuboresha afya ya ngozi yangu?

Jibu ni ndio ,kama nilivyosema mwanzo ulaji wetu husababisha kuboresha au kudhoofisha afya ya ngozi zetu.Mpaka sasa umeona vyakula vinavyodhoofisha afya ya ngozi yako. Ni vyema ukaanza kula vyakula hivi ambayo vitaboresha afya ya ngozi yako.


1.Mboga mboga za majani


Vyakula hivi ni muhimu sana kwa afya ya ngozi yako huwa vimesheeni aina mbalimbali za vitamini vyenye faida katika ngozi na mwili wako kwa ujumla .Mboga za majani husaidia katika uzalishaji wa seli mpya katika mwili wako na kuondoa seli zile zilizokufa.Hivo upelekea ngozi kuwa yenye kung'ara na kuvutia pia.

2.ulaji wa Machungwa na Limao 


Matunda haya pia yanasifika katika kuboresha afya ya ngozi yako,kwa sababu husaidia katika utengenezaji wa vitamini C ambayo huondoa uvimbe na mikunjo ya ngozi na kuifanya ngozi kutozeeka mapema.

3.Asali  


Asali ni chakula kinachotumika mara kwa mara ambacho utengenezwa na nyuki.chakula hiki pia husaidia kuboresha afya ya ngozi yako kwa kutunza na kuhifadhi unyevu kwenye ngozi yako,pia ina asidi ambayo huzuia vijidudu mbalimbali wanaozaliwa kwenye ngozi. Hivyo unashauriwa kupendelea kutumia asali mara kwa mara na pia kuipaka kwenye ngozi ili iweze kunawiri.


Kumbuka vyakula nilivyovitaja hapo juu kwa ajili ya kuboresha afya ya ngozi yako ni vyakula asili kabisa ,hivyo unahuakika wa kupata matokea chanya kama utachukua hatua sasa ya kulinda na kuboresha afya ya ngozi yako kupitia ulaji mzuri wa vyakula mbalimbali.


Kama umeipenda chapisho hili basi gonga NZURI  na  kwa maswali au maoni zaidi basi tuandikie baada ya andiko hili, na pia kama ungependa kusoma andiko jengine kama hili basi jisajili kwa kuweka anuani yako  kwenye linki ya SUBSCRIBE.

Pia waweza tuandikia kwa email yetu Kuafit08@gmail.com 
Kwa number yetu ya Tigo +255 653 009 477  
Instagram account yetu  (KUAFITI), Facebook-(kuafit) 

About Davis David

Davis David
Recommended Posts × +

DIET YA KUTOA SUMU MWILINI NA KUPUNGUZA UNENE KWA HARAKA

Habari zenu wadau wa KUAFIT! leo tutaongelea kuhusiana na elimu ya lishe ambayo itahusiana na diet ambapo tutaelezea mambo mengi san...