latest Post

AINA KUU TANO MUHIMU YA VYAKULA


Wataalamu wa lishe wanasema vyakula ni kama mafuta na mwili ni kama injini ambapo vyote viwili kwa pamoja humfanya mtu aweze kufanya kazi zake za kila siku. Kwa kula vyakula mtu anaweza kuongeza virutubisho, kuongeza nguvu na pia kujenga mwili wake. Mtu anaweza kuongeza virutubisho kwa kiwango sahihi ndani ya mwili wake endapo atweza kula mlo sahihi na uliokamilika.

Je! mlo uliokamilika ni upi?
Hili ni sawali ambalo watu wengi hujiuliza na hivyo ni vyema kufafanua swala hili. Mlo kamili ni ule amabo uliojumuisha ania tano ya vyakula ambavyo ni maziwa, matunda, nafaka, nayama zisizo na mafuta/karanga  pamoja na mboga/kunde.

1.Maziwa

  Maziwa ni moja wapo ya aina ya chakula ambacho kina umuhimu sana katika mwili wa mwanadamu hasa kutokana na virutubisho vilivyo ndni yake. Chakula hiki kimebarikiwa na kalisi (calcium) ambayo husaida kuhimarisha mifupa ya mwili.

2.Matunda

  Matunda ni aina ya chakula kilicho barikiwa kwa kuwa na vitamini ukilinganisha na aina nyingine ya vyakula hivyo na pia chakula hiki huwa na kambalishe. kwa kula matunda kunafanya ngozi ya mwili kuonekana yenye afya na mwili kuonekana imara.

3.Nafaka

 Nafaka ni aina ya chakula kilichobarikiwa kwa kuwa na kamba-lishe na wanga ambapo huongeza nguvu na afya ndani ya mwili. Vyakula vilivyotokana na nafaka ni kama vile supageti na mkate.

4.Nyama zisizo na mafuta na karanga


 Nyama kama vile ya ngombe,kuku samaki na karanga  kwa pamoja huongeza mafuta na protini mwilini ambayo husaidia kuongeza na kujenga misuli.

5.Mboga/kunde

Mboga na kunde ni aina moja wapo ya kundi la chakula ambacho huliwa sana na watu wengi katika maisha ya kwaida. Chakula hiki kimebarikiwa kwa kuwa na vitamini, kamba-lishe, pamoja na lishe ya mimea(phyto-nutrients)

Aina hizo za vyakula vikizingatiwa kwa kuliwa katika mlo wa kila siku mtu anaweza akuweka mwili wake katika muonekano mzuri na hata kwa wale wanaopenda kupungua ama kuongeza mwili wanaweza wakafanya hivyo kwa kukadiria kiasi cha kila aina ya chakula wanachokula.

Mfano;-

  •  Kwa mtu anayetaka kuongeza mwili atalazimika kula vyakula vya (Nafaka, Nyama/karanga, Maziwa) kwa sana ili apate kamba-lishe, protini na wanga kwa sana.
  • Kwa mtu anayetaka kupunguza mwili atalazimika kula vyakula vya(Mboga, Matunda) kwa sana ili aweze kupata vitamini na kamba-lishe kwa sana
Kama umeipenda chapisho hili basi gonga NZURI  na  kwa maswali au maoni zaidi basi tuandikie baada ya andiko hili, na pia kama ungependa kusoma andiko jengine kama hili basi jisajili kwa kuweka anuani yako  kwenye linki ya SUBSCRIBE.

Pia waweza tuandikia kwa email yetu Kuafit08@gmail.com 
Kwa number yetu ya Tigo +255 653 009 477  


Instagram account yetu  (KUAFITI), Facebook-(kuafit) 

About benson godfrey

benson godfrey
Recommended Posts × +

DIET YA KUTOA SUMU MWILINI NA KUPUNGUZA UNENE KWA HARAKA

Habari zenu wadau wa KUAFIT! leo tutaongelea kuhusiana na elimu ya lishe ambayo itahusiana na diet ambapo tutaelezea mambo mengi san...