latest Post

FAIDA YA KULA SAMAKI



 Nyama ya samaki ni kati ya chakula kinachofahamika sana na watu wengi na husifika sana kwa utamu wake. Japokuwa kuna aina nyingi ya samaki bali kwa ujumla wake ni kwamba nyama ya samaki ina faida nyingi kwa afya ya mwili wa mtu.


1.Husaidia katika ukuwaji wa mwili na ubongo wa mtu na hii ni kutokana na kwamba nyama ya samaki ina omega -3 fatty acid ambayo ni muhimu kuhakikisha ukuaji unatokea




2.Hupunguza uwezekano wakupata maradhi ya moyo. Utafiti unaonyesha kwa kula samaki mara kwa mara kunachangia mtu kutokupata maradhi ya moyo na mshtuko wa mwili unaopelekea ugonjwa wa kupooza(stroke).



mtu mwenye shida ya kumbukumbu
3.Huongeza ufanisi wa ubongo na pia kupunguza kasi ya uzeekaji na hii nikutokana na tissue itwayo (grey matter) ambayo ni muhimu katika swala la kumbukumbu. Hivyo kutokana na samaki kuwa na kiasi kikubwa cha(grey matter) basi nyama ya samaki ni muhimu sana kwa afya ya ubongo wa mtu.



4.Huongeza kiwango cha vitmini D ambayo ni muhimu sana kwa mwili wa mtu hasa kwa watu ambao hawajabahatika kupata vitamini hii kutoka kwa mwanga wa jua . vitamini hii husaidia mtu kuepuka kuwa na miguu ya matege na bila kusahau kuongeza nguvu ya mwili na inawezekana kuipata eidha kwa kula samaki ama kula mafuta ya samaki.



5.Husaidia kuhimarisha macho hasa kwa wazee wenye ugonjwa wa kuona(vision impairment) ambapo mtu anaweza akaona vizuri bila ya shida angali uzee utakuwa unamkabili mtu huyo.

Kama umelipenda andiko hili basi gonga NZURI  na  kwa maswali au maoni zaidi basi tuandikie baada ya andiko hili, na pia kama ungependa kusoma andiko jengine kama hili basi jisajili kwa kuweka anuani yako  kwenye linki ya SUBSCRIBE.


Pia waweza tuandikia kwa email yetu Kuafit08@gmail.com 


Kwa number yetu ya Tigo +255 653 009 477  

About Kuafit

Kuafit
Recommended Posts × +

0 comments:

KUPUNGUZA UZITO KWA MAJI YA BARIDI

Watu wengi katika jamii hupendelea kuoga na maji ya moto katika majira yote ya hewa lakini kutokana na utafiti uliofanywa na wanasayansi kam...