latest Post

TATIZO LA TUMBO KUJAA GESI NA TIBA YAKE

 

Tatizo la tumbo kujaa gesi limekuwa kubwa kwa siku za hivi karibuni. Hii inatokana na lishe mbovu tunayokula kila siku kwa kutegemea zaidi vyakula vya haraka na bei rahisi (fast foods & snacks), msongo wa mawazo, matumizi ya vidonge mara kwa mara na mazingira yenye sumu yanayotuzunguka kama moshi wa magari na kemikali za viwandani.

Kuwa na gesi tumboni ni tofauti kabisa na kitambi, kitambi kinaweza kuwa cha muda mrefu lakini tumbo la gesi ni la muda tu baadae husinyaa na kurudi katika hali ya kawaida kwani husababishwa na hewa kukwama tumboni na kufanya tumbo kutanuka. Kwa watu wengine tumbo linaweza kuwa kubwa kama mjamzito.
  • Sababu 6 Zinazoletekeza Tumbo Kujaa Gesi


1.Matatizo kwenye Mmeng’enyo wa Chakula
2.Maji kubakizwa mwilini (fluid retention)
3.Mwili kukosa maji (Dehydration)
4.Alegi ya Chakula
5.Majeraha Kwenye Mfumo wa Chakula
6.Mabadiliko ya Homoni
7.Kula vyakula vyenye Gas sana
  • Vyakula vya Kuepuka pale Unapotaka Kutibu Tatizo la Tumbo Kujaa Gesi


>Vyakula vya sukari (snacks)
>Nafaka na vyakula vya nafaka hasa ngano na Maharage huongeza uzalishaji wa gesi tumboni
>Vinywaji vilivosindikwa kama soda (Carbonated drinks)
  • Njia zingine za Kukusaidia Kuondokana na Tatizo la Tumbo Kujaa Gesi


  1. Maziwa mtindi (YOGURT) ni mazuri sana kusaidia kupunguza gesi tumboni
  2. Ulaji wa mbogamboga zenye kiasi kidogo cha wanga kama vile (njegere, karoti, nyanya)
  3. Ulaji wa matunda kama vile(ndizi, matikiti,mizabibu)
  4. Kutumia mchele kwa niaba ya ngano na viazi
  5. Kunywa maji ya kutosha: Maji hurahisisha usagaji wa chakula na utolewaji wa choo

Kama umelipenda andiko hili basi gonga NZURI  na  kwa maswali au maoni zaidi basi tuandikie baada ya andiko hili, na pia kama ungependa kusoma andiko jengine kama hili basi jisajili kwa kuweka anuani yako  kwenye linki ya SUBSCRIBE.


Pia waweza tuandikia kwa email yetu Kuafit08@gmail.com 


Kwa number yetu ya Tigo +255 653 009 477 

About Kuafit

Kuafit
Recommended Posts × +

0 comments:

KUPUNGUZA UZITO KWA MAJI YA BARIDI

Watu wengi katika jamii hupendelea kuoga na maji ya moto katika majira yote ya hewa lakini kutokana na utafiti uliofanywa na wanasayansi kam...