latest Post

ZIJUE FAIDA ZA KULA KOROSHO KUIMARISHA AFYA YAKO


Korosho ni zao maarufu sana duniani lenye virutumbisho mbalimbali vinavyoweza kuimarisha afya ya mwili wako.Wengi wetu tunalifahamu zao hili lakini hatujui faida zake katika kuboresha afya zetu.Tafiti mbalimbali zilizofanyika juu ya zao hili la korosho zinaonyesha zao hili lina faida nyingi sana kiafya hasa kwa wagonjwa wanaosumbulia na moyo.


Imegundulika kuwa ndani ya zao hili la korosho kuna vitammini na madini mbalimbali kama vile Thiamin,magnesium, copper,selenium,phosphorus pamoja na pantothenic acid.Hivyo inashauriwa kupenda kula korosho mara kwa mara ili kuboresha afya yako.

Zifuatazo ni faida mbalimbali zinatokana na zao hili pale unapoamua kula mara kwa mara.

1.Korosho husaidia kuimarisha afya ya ngozi yako kwa kuzuia miale ya UV kutoka kwenye jua kuathiri ngozi yako,hivyo kuiacha ngozi ikiwa katika afya njema.

2.Virutumbisho vinavyopatikana katika korosho husaidia mishipa ya damu na fahamu katika mwili wako kufanya kazi zake kwa ufasaha, hali hii upelekea damu kusambaa vyema mwili nzima na kuzifanya hisia za mwili kuwa katika hali nzuri.

3.Madini mbalimbali yaliyopo ndani ya korosho husaidia kuzuia seli za saratani kuendelea kukua zaidi na pia husaidia mtu kutopata saratani ya utumbo mpana.

4.Vijiwe vinavyokuwa katika figo huweza kuleta madhara mbalimbali katika mwili wako.Ikiwa utakuwa unakula korosho itasaidia kuzuia hatari hii kwa asilimia 25.

5.Kama unasumbuliwa na hali ya nywele zako kubadilika rangi kutoka rangi halisi,madini ya shaba yanayopatikana katika kurosho yanasaidia nywele zako kubaki katika rangi yake ya weusi.

6.Kama unasumbuliwa na mifupa yako kuwa na udhaifu, madini ya calcium na magnesium yanayopatikana kwenye korosho yanaweza kukusaidia kuimarisha afya ya mifupa na kuiongezea uimara.

7.Katika umengenywaji wa chakula korosho husaidia kuzalisha baadhi ya enzymes zinazosaidia katika mchakato mzima ya kumengenya chakula mwilini.

8.Sifa nyigine ya korosho ni kuwa na viua sumu mwilini kwa lugha ya kitaalamu ni Antioxidants.Viua sumu hivi husaidia kuzuia na kuua sumu mbalimbali zinazoingia mwilini kwa njia mbalimbali kama vile vyakula pamoja na matumizi ya madawa.


Kama umeipenda chapisho hili basi gonga NZURI  na  kwa maswali au maoni zaidi basi tuandikie baada ya andiko hili, na pia kama ungependa kusoma andiko jengine kama hili basi jisajili kwa kuweka anuani yako  kwenye linki ya SUBSCRIBE.

Pia waweza tuandikia kwa email yetu Kuafit08@gmail.com 
Kwa number yetu ya Tigo +255 653 009 477  

Instagram account yetu  (KUAFITI), Facebook-(kuafit)

About Davis David

Davis David
Recommended Posts × +

DIET YA KUTOA SUMU MWILINI NA KUPUNGUZA UNENE KWA HARAKA

Habari zenu wadau wa KUAFIT! leo tutaongelea kuhusiana na elimu ya lishe ambayo itahusiana na diet ambapo tutaelezea mambo mengi san...