latest Post

TEGEMEA MAMBO YAFUATAYO KAMA HUFANYI MAZOEZI YA MWILI



Habari yako msomaji wa makala za kuafit, karibu tena uzidi kujifunza na kuelimika juu ya afya, lishe na mazoezi.Ni wazi kwamba ili tuwe na afya nzuri tunahitaji kuwa na ratiba nzuri ya kufanya mazoezi mara kwa mara. Hata hivyo, ingawa hatari za kutofanya mazoezi zimezungumziwa sana kupitia njia mbalimbali, watu wengi ulimwenguni hawafanyi mazoezi yoyote. Shirikisho la Moyo Ulimwenguni linaamini kwamba kati ya asilimia 60 hadi 85 ya watu ulimwenguni “hasa wasichana na wanawake, hawafanyi mazoezi ya kutosha ili kupata manufaa ya afya.Shirikisho hilo linadai kwamba “karibu thuluthi mbili ya watoto pia hawafanyi mazoezi ya kutosha ili kupata manufaa ya afya.Kama huna tabia ya kufanya mazoezi mara kwa mara tambua kuwa afya yako ipo hatarini ingawa unaweza ukajiona unafya njema kabisa.Mazoezi yanamchango mkubwa sana katika kuboresha afya yako na kukukinga dhidi ya magonjwa mbalimbali.

Tafiti zinaonyesha kwamba watu milioni mbili duniani hufa kila mwaka kutokana na sababu zinazohusiana na kukosa kufanya mazoezi.Nchi kama Australia hutumia dola million 377 kila mwaka kutibu matatizo ya afya yanayosababishwa na kutofanya mazoezi.Kulingana na shirikisho la Moyo ulimwenguni, katika mwaka mmoja tu nchi ya Canada ilitumia dola za kimarekani zaidi ya billioni mbili kutibu matatizo ya afya yanayosababishwa na kutofanya mazoezi.Takwimu hizi zinatudhiirishia ni jinsi gani mtu ambaye hafanyi mazoezi anahatarisha afya yake.


MADHARA YA KUTOFANYA MAZOEZI


1.Watu wasiofanya mazoezi huwa na mrundikano wa mafuta mwilini na kwenye mishipa ya damu, hali hii hupelekea kusababishwa magonjwa mbalimbali na kudhoofisha afya zao.

2.Mwili unakuwa katika hatari ya kupata magonjwa yasiyoambukizwa kama vile kisukari,aina fulani za kansa, presha, ugonjwa wa mifupa pamoja na  msongo wa mawazo.

3.Kuna hatari ya kuwa na uzito ulizidi kiwango  cha uzito halisi unachochatakiwa kuwa nacho.Tatizo hilo linasababishwa hasa na kula vyakula vyenye kalori nyingi na kutofanya mazoezi.Kumbuka kimo chako lazima kiendani na uzito wa mwili wako ili kuimarisha afya yako, nje ya hapo unaweza kupata magonjwa mbalimbali.
SOMA :Kipimo cha BMI

4.Watu wasiofanya mazoezi wanajiweka katika hatari ya kifo.
Nchini Hong Kong, uchunguzi wa hivi karibuni ulionyesha kwamba huenda asilimia ishirini (20%) hivi ya vifo vyote vilivyotokea miongoni mwa watu walio na umri wa miaka 35 au zaidi, vilisababishwa na kukosa kufanya mazoezi. Uchunguzi huo ulioongozwa na Profesa Tai-Hing Lam wa Chuo Kikuu cha Hong Kong na kuchapishwa na jarida Annals of Epidemiology katika mwaka wa 2004.

5.Kutofanya mazoezi kunaweza kuongeza sana hatari ya kupatwa na magonjwa fulani yanayotishia uhai. Kwa mfano, kulingana na Shirika la Moyo la Marekani, kutofanya mazoezi “huongeza maradufu hatari ya kupatwa na ugonjwa wa moyo na huzidisha kwa asilimia 30 hatari ya kupatwa na shinikizo kubwa la damu. Pia huongeza maradufu uwezekano wa kufa kutokana na ugonjwa wa moyo na kiharusi".

6.kutofanya mazoezi huufanya mwili kutokuwa na umbo zuri ukilinganisha na mtu anayefanya mazoezi mara kwa mara, hii utokana na kuwa na nyama nyingi mwilni(nyama uzembe),kitambi kwa wakina baba na tumbo kubwa kwa akina mama.

Mazoezi huberesha afya, huzuia magonjwa na hata kupunguza uwezekano wa kufa mapema. Fanya mazoezi ili uweze kuishi muda mrefu. Sio lazima ufanye mazoezi magumu, ya gharama au mbali na ulipo – Anza na yale utakayoyamudu kwa urahisi. Unaweza ukaamua kutembea au kukimbia umbali fulani kila siku na ruka kamba.

Kama umeipenda chapisho hili basi gonga NZURI  na  kwa maswali au maoni zaidi basi tuandikie baada ya andiko hili, na pia kama ungependa kusoma andiko jengine kama hili basi jisajili kwa kuweka anuani yako  kwenye linki ya SUBSCRIBE.

Pia waweza tuandikia kwa email yetu Kuafit08@gmail.com 
Kwa number yetu ya Tigo +255 653 009 477  

Instagram account yetu  (KUAFITI), Facebook-(kuafit)


About Unknown

Unknown
Recommended Posts × +

2 comments:

Bila jina alisema ...

nba predictions reddit - thtopbet.com ボンズ カジノ ボンズ カジノ 카지노 가입 쿠폰 카지노 가입 쿠폰 카지노사이트 카지노사이트 792The Habanero Pepper Hot Sauce 4oz (4 FL.OZ. / 240 ml)

igoryokabato alisema ...

welding titanium oxide - Tianium Art
If you how to get titanium white octane want to build titanium nitride coating a ceramic bead you can titanium banger create a ceramic bead for the metals omega seamaster titanium and metals used. These titanium oxide $3.99 titanium body jewelry · ‎In stock

KUPUNGUZA UZITO KWA MAJI YA BARIDI

Watu wengi katika jamii hupendelea kuoga na maji ya moto katika majira yote ya hewa lakini kutokana na utafiti uliofanywa na wanasayansi kam...