latest Post

FAHAMU AINA YA MAZOEZI MAALUMU KWA WAZEE


Inasemekana kwamba kadiri unavyozeeka ndivyo unavyoweza kunufaika kwa kufanya mazoezi kwa kiasi. Hata hivyo, wazee wengi husita kufanya mazoezi kwa ukawaida kwa kuogopa kwamba wataumia au watakuwa wagonjwa. Ni kweli kwamba wazee wanapaswa kutafuta ushauri wa daktari kabla ya kuanza kufanya mazoezi magumu. Hata hivyo, wataalamu wanaamini kwamba kufanya mazoezi kunaweza kuboresha sana maisha ya wazee. Wazee wanapofanya mazoezi hupata faida nyingi kama vile kuboresha afya ya kihisia,kupona haraka ugonjwa au jeraha,Kuboresha utendaji wa tumbo na ini, uyeyushaji wa chakula mwilini,kuboresha mfumo wa kinga, kuipa mifupa  nguvu na Kuongeza nguvu nyingi.


Yapo mazoezi ya aina mabalimbali ambapo wazee wanaweza kufanya, mazoezi haya ni pamoja na kutembea,kukimbia kidogo kidogo kuruka kamba,kucheza muziki na hata kufanya shughuli ndogondogo zinazohusisha viungo vya mwili kufanya kazi.Tafiti mbalimbali pia zimegundua kwamba mazoezi mepesi yanarudisha uwezo wa kukumbuka kwa wazee.Ikumbukwe  kwamba wazee wengi waliofikisha umri kuanzia miaka 60,uwezo wa kutunza kumbukumbu huanza kupungua taratibu na wengine hupoteza kumbukumbu kabisa.Ugonjwa maarufu wa kupoteza kumbukumbu unaojulikana kama "Alzheimer disease" ingawa si wote wanaopoteza kumbukumbu wana ugonjwa huu.Wazee wenye tabia ya kufanya mazoezi ya kuendesha baiskeli au kujinyosha viungo, huongeza uwezo wao wa kukumbuku kuliko wale wasiofanya hivyo, hivyo kama wewe umri wako ni kuanzia miaka 60 na kuendelea au nyumbani kwako kuna mzee ni vyema ukamshauri aanze tabia ya kufanya mazoezi mara kwa mara badala ya kukaa muda mrefu bila mazoezi hii itasaidia kuboresha afya yake kwa kiasi kikubwa.


Nini cha kufanya?

Uzuri ni kwamba wazee hawahitaji kufanya mazeozi mazito katika vituo maalumu vya mazeozi, mazoezi ni kama kutembea,kunyoosha viungo na hata kucheza muziki.Ukiwa nyumbani penda kujishughulisha mwili wako ili misuli ya mwili kwa ujumla ifanye kazi, hii itasaidia kuimarisha misuli ya mwili wako.


Unashauriwa unapoamka asubuhi cha kwanza unapaswa kukaa angalau dakika tano huku ukivuta pumzi ndefu na kutulia ,kisha ukaanza kunyoosha viungo vya mwili wako kwa dakika kadhaa.Unaweza kutumia chumba unacholala kutembea umbali mfupi mara nyingi kwenda na kurudi.Usijaribu kuanza ,mazoezi kwa haraka kwani inaweza kuleta shida katika mwili wako kwa sababu haujazoea hali hiyo hivyo ni vyema kuanza kidogo kidogo ili kujenga mazoea mpaka iwe ni kwawaida yako.kama afya yako ni dhaifu(unaumwa) ni vyema ukapata ushauri kwa daktari ni mazoezi gani ufanye katika hali ya kiafya uliyonayo wakati huo.


Kwa wale wazee ambao bado wanafanya kazi ofisini pendelea kutembea mara kwa mara badala ya kumtuma mtu kuwenda kuchukua kitu fulani nenda wewe mwenyewe ili mwili wako uwe katika hali ya mazoezi muda wote,pia kama unatumia usafiri wa umma,unaweza ukawa unashukia mbali kidogo na kituo chako ili utembee kuushughulisha mwili.


Kumbuka bima namba moja ya afya ya mzee ni mazoezi.Inashauriwa kujenga tabia ya kutembea angalau kilometa mbili kwa siku ukitumia kati ya dakika 30 hadi 45.Fanya hivyo mara tano kwa wiki.

Kama umeipenda chapisho hili basi gonga NZURI  na  kwa maswali au maoni zaidi basi tuandikie baada ya andiko hili, na pia kama ungependa kusoma andiko jengine kama hili basi jisajili kwa kuweka anuani yako  kwenye linki ya SUBSCRIBE.

Pia waweza tuandikia kwa email yetu Kuafit08@gmail.com 
Kwa number yetu ya Tigo +255 653 009 477  

Instagram account yetu  (KUAFITI), Facebook-(kuafit)

About Unknown

Unknown
Recommended Posts × +

0 comments:

KUPUNGUZA UZITO KWA MAJI YA BARIDI

Watu wengi katika jamii hupendelea kuoga na maji ya moto katika majira yote ya hewa lakini kutokana na utafiti uliofanywa na wanasayansi kam...