latest Post

FAIDA ZA KIAFYA ZA KUNYWA MAJI YA UVUGUUVUGU



Unywaji wa maji ni sehenu nuhimu katika kuboresha afya zetu.Maji husaidia kuboresha afya zetu kwa kutukinga na maradhi mbalimbali pamoja na kuwa kinga dhidi ya magonjwa mbalimbali.


Leo nitazungumzia faida ya matumizi ya maji ya uvuguvugu katika kuboresha afya yako.Maji ya uvuguvugu yanatajwa kuwa na manufaa zaidi kuliko maji ya baridi.Wataalamu wa afya wanasema yanasaidia uyeyushaji wa chakula, yanazilinda figo na ogani muhimu mwilini.


Ni vyema ukatambua kuwa unatakiwa kunywa maji ya uvuguvu na sio maji ya moto kwani ukijaribu kunywa maji ya moto utaleta madhara katika seli za ulimi wako.


Unapokunywa maji ya baridi huwa na tabia ya kugandisha mafuta ya miili yetu,ikiwa ni pamoja na mishipa ya damu hali hii ikiiendelea inaweza kusababisha shinikizo la damu kutokana na ukosefu wa mzunguko wa damu pamoja na magonjwa mengine mengi.Kama haikufanyiwa kazi inaweza hata kusababisha saratani.


SOMA: Madhara ya kunywa Maji Baridi


Hivyo ni vyema ukaanza kuwa na tabia ya kunywa maji ya uvuguvugu ili kujiepusha na maradhi mbalimbali.Madaktari wanashauri kutumia maji ya uvuguvugu yaliotiwa limao au ndimu ili kupunguza radical ndani ya mwili na kuleta radha katika maji na pia ni vyema ukanywa maji hayo kabla ya kifungua kinywa ili kurahisisha mfumo wa mwili kwa siku nzima.



FAIDA ZA KUNYWA MAJI YA UVUGUVUGU

1.Yanasaidia kupunguza uzito

Kama unasumbuliwa na uzito wa mwili wako na ungependa kupunguza unashauriwa kunywa maji ya uvuguvugu kwani huweza kuongeza joto la mwili ambalo linabadilisha ongezeko la kiasi cha metabolic, kuongezeka kwa metabolic mwili unakuwa na uwezo wa kuchoma carories siku nzima.


2.Yanaboresha Mzunguko wa damu mwilini.

Mwili unapokuwa na mlimbikizo wa mafuta ambayo unaweza sababishwa na unywaji wa maji baridi husababisha madhara mbalimbali katika afya yako.Lakini unapotumia maji ya uvuguvugu yanaenda kuyeyusha na kuondoa hiyo migando ya mafuta mwilini.Hatua hii husaidia kuondoa sumu yote ndani ya mwili na kuufanya mzunguko wa damu kuwa mzuri na kufanya misuli kupumzika.


3.Yanasaidia kuondoa mikunjo mwilini.

Hakuna mtu anayependa kuzeeka mapema,pia mwili wako unapokuwa na sumu hukufanya ezeeke mapema.Unapokunywa maji ya uvuguvugu yanasaidia kuondoa sumu na yanasafisha kabisa.Zaidi sana yanasaidia kurejesha seli za ngozi ili iwe na  muonekano wa kuvutia na kuwa nyororo.


4.kuondoa sumu mwilini

Faida nyingine ya kunywa maji ya uvuguvugu ni kutoa sumu zilizopo kwenye mishipa ya fahamu na kuisadia figo kufanya kazi kikamilifu,hii ni tofauti kabisa na maji ya baridi ambayo yanagandisha na kuilazimisha figo kuyeyusha kwanza na kisha kuchuja.

5.Kupata choo kwa urahisi

Maji ya uvuguvugu ni mazuri hata kwa kupata choo,kwa vile yanarahisisha uyeyushaji na uchambuaji wa kinachotakiwa na kisichotakiwa,wanaokunywa maji ya baridi wana uwezekano mkubwa wa kupata haja kubwa kwa shida.


Faida zingine ni pamoja na kusafisha haja ndogo na kuchangamsha utendaji kazi wa ubongo wako.

Ni vyema kunywa maji ya moto yaliyochemshwa na kuyaacha yapoe na kuwa vuguvugu na kuongeza limao na asali mbali na kuongeza ladha,asali na limao vina faida kiafya.Fanya hivi Kila unapo amka Asubuhi kabla ya kula kitu Kunywa Maji ya Uvuguvugu Glasi 3 kisha kaa kwa muda wa saa moja bila ya kula kitu. Baada ya saa moja kupita waweza kula chakula.

Kama umeipenda chapisho hili basi gonga NZURI  na  kwa maswali au maoni zaidi basi tuandikie baada ya andiko hili, na pia kama ungependa kusoma andiko jengine kama hili basi jisajili kwa kuweka anuani yako  kwenye linki ya SUBSCRIBE.

Pia waweza tuandikia kwa email yetu Kuafit08@gmail.com 
Kwa number yetu ya Tigo +255 653 009 477  
Instagram account yetu  (KUAFITI), Facebook-(kuafit)

About Unknown

Unknown
Recommended Posts × +

0 comments:

KUPUNGUZA UZITO KWA MAJI YA BARIDI

Watu wengi katika jamii hupendelea kuoga na maji ya moto katika majira yote ya hewa lakini kutokana na utafiti uliofanywa na wanasayansi kam...