latest Post

MAGONJWA YANAYOONGOZA KUSABABISHA VIFO BARANI AFRIKA


Aina ya magonjwa ambayo yanatambulika kwa ujumla ni magonjwa ya kuambukiza na magonjwa yasiyo ya  kuambukiza.Watu wengi wanafahamu magonjwa ya kuambukiza kama vile ukimwi,magonjwa ya zinaa na magonjwa yasiyo ya kuambukiza kama vile malaria,kisukari n.k
Pia kuna ukweli kwamba idadi kubwa ya watu wanaogopa magonjwa ya kuambukiza kuliko magonjwa yasio ya kuambukiza,jambo hili limepelekea dhahania potofu ya mtu anayeumwa ukimwi kuogopwa sana kuliko anayeumwa malaria au ugonjwa mwingine.




je unafahamu magonjwa yasio ya kuambukiza yanaongoza kwa kusababisha vifo vingi kuliko magonjwa ya kuambukiza??. Wengi wetu hatufahamu jambo hili.Ripoti toka katika shirika la Afya duniani(WHO) inaonyesha magonjwa ya kisukari,magonjwa ya moyo,shinikizo la damu,saratani na mengineyo ndio yanayoongoza kwa kusababisha vifo vingi barani afrika.

Imeelezwa pia magonjwa yanayotokana na maabukizi ya bakteria na virusi kwenye njia ya hewa kama na mapafu (lower respiratory tract infections) pia yameshika kasi katika kuongeza idadi ya vifo barani Afrika.


Ugonjwa wa kuharisha imesababisha vifo vingi barani Africa.Ungonjwa huu usababishwa na virusi,bakteria au maambukizi ya vimelea (parastic infections),pia ni ugonjwa wa pili unaosababisha vifo kwa watoto walio chini ya miaka 5 barani afika.

Ugonjwa mwingine unaongoza kwa kusababisha vifo ni kiharusi kitaalamu unaitwa stroke ambao umeongezeka zaidi ya miaka mitano iliyopita kutoka 406,595 (4.4% ya vifo) hadi 451,000 (4.9%) mwaka 2015.

Sababu nyingine inayosababisha vifo katika bara la Afrika ni ugonjwa wa moyo (ischemic) au kikawaida unajulikana kama mashambulizi ya moyo.Mwaka 2010 vifo vya watu 389,785(4.2% ya vifo) vilisababishwa na ugonjwa wa mashambulizi ya  moyo(Heart Attack), lakini  hadi mwaka 2015 iliongezeka mpaka vifo 441,000(4.8%).

Swali!! Tunajifunza nini kutokana na Ripoti hii.?
Jinsi tunavyoishi(lifestyle) ndio itaamua hatima ya afya zetu.Watu wengi hawazingatii afya zao ipasavyo wanaishi kiholela tu,Wanakula kila wanachokiona barabarani,lishe ya watoto wao sio nzuri,kucheki afya zao ni mpaka waone dalili ya  kuumwa,kufanya mazoezi ya mwili ni nadra sana,unywaji wa pombe uliopitiliza na uvutaji wa sigara uliopitiliza imesababisha kuwa na afya zilizozolota.

Watu wengi wanazingatia(focus) kutimiza malengo yao(uchumi,elimu,kazi,ndoa n.k ) lakini wanasahau kutokuwa na afya bora haya malengo yatakuwa ndoto kutimia katika maisha yako(unaweza ukafa pasipo kutimiza ndoto zako kwa sababu hukuzingatia afya yako).Ni vyema tukazingatia afya zetu kama vile tunavyozingatia malengo yetu katka maisha.

Hivyo ni matumaini yangu kuanzia leo baada ya kusoma ujumbe huu,afya yako itakuwa ni jambo moja wapo unalolipa kipaumbele(priority) katika maisha yako.Anza kwa kufanya vifuatavo:-
(a)kula chakula bora na kisafi kinachojenga mwili wako
(b)kapime afya yako(body checkup) angalau mara 3 kwa mwaka
(c)Fanya mazoezi angalau mara tatu kwa wiki
(d)hakikisha makazi yako yapo katika usafi muda wote
(e)Kula matunda mbalimbali kila wiki na
(f)Penda kufuatilia habari/jumbe zinazohusu afya ili ujifunze zaidi jinsi ya kuutunza mwili wako ipasavyo.

Ni matumaini yangu umejifunza mambo mengi kuhusu afya yako siku ya leo.Tukutane siku nyingine hapahapa kuafit.com


Kama umeipenda andiko hili basi gonga NZURI  na  kwa maswali au maoni zaidi basi tuandikie baada ya andiko hili, na pia kama ungependa kusoma andiko jengine kama hili basi jisajili kwa kuweka anuani yako  kwenye linki ya SUBSCRIBE.
Pia waweza tuandikia kwa email yetu Kuafit08@gmail.com 

Kwa number yetu ya Tigo +255 653 009 477  

Instagram account yetu  (KUAFITI), Facebook-(kuafit) na twitter-(kuafit)

 

About Kuafit

Kuafit
Recommended Posts × +

0 comments:

KUPUNGUZA UZITO KWA MAJI YA BARIDI

Watu wengi katika jamii hupendelea kuoga na maji ya moto katika majira yote ya hewa lakini kutokana na utafiti uliofanywa na wanasayansi kam...