latest Post

FAHAMU BODY MASS INDEX YA MWILI WAKO


karibu katika blog yako pendwa ya kuafit.com leo tutaangalia  uwinao uliopo kati ya urefu wako na uzito wako,kitaalamu unaitwa BODY MASS INDEX (BMI).BMI ni njia inayotumia kitaalamu kufahamu mtu yupo katika hali nzuri kiafya au laa kwa kupima uwiano uliopo kati ya uzito na urefu wa mwili wa mtu husika.kama ulikuwa hufahamu uhusiano huu wa uzito wako na urefu wako basi endelea kusoma ujumbe huu utajifunza mengi.

 

Faida za kujua BMI

(a)kutathimi hali ya afya yako

kama nilivyoeleza hapo mwanzo kipimo hiki husaidia kutathmini hali ya lishe ya mtu yeyote.Pia mtu ambaye anaishi na virusi ya ukimwi kipimo hiki usaidia kujua baadhi ya matatizo ya kiafya na kilishe kwa mtu husika.Kupitia kipimo hiki kitakuasaidia kujua kama kiwango cha BMI yako ni kubwa sana,wastani au ndogo sana na hatua za kuchukua ili kulinda afya yako na kujiepusha na magonjwa.

(b)kupata ushauri toka kwa wataalamu wa afya

Kwa madaktari na watoa huduma katika vituo vya afya kipimo hiki huwasaidia kutoa ushauri kwa wagonjwa na kuepusha kupata magonjwa mengine hatari zaidi.Tafiti nyingi zilizofanyika zinaonyesha kuwa kuna uhusiano mkubwa kati ya kipimo cha BMI  na  hatari ya kupata magonjwa mbalimbali pia kusababisha vifo visivyotarajiwa(premature death).kiwango cha BMI kinapozidi kuongezeka kuna uwezekano wa kupata magonjwa yafuatayo
  • saratani ya aina mbalimbali
  • kiharusi
  • shinikizo la damu
  • ugonjwa wa moyo

Jinsi ya kupima BMI

BMI hupatikana pale uzito katika kipimo cha kilogramu(Kg) unagawanya kwa kimo(urefu) katika mita za mraba(mita kipeo cha pili).

KANUNI YA KUPIMA BMI
BMI = uzito(Kg) ÷ kimo(m^2)


Hatua za upimaji


1.Pima uzito wako

Wakati wa upimaji uzito hakikisha mshale wa mizani uko kwenye sifuri na unapopima uzito hakikisha umevaa nguo nyepesi na kuvua viatu.Pia unapaswa kusimama wima katikati ya mizani bila kushirikia kitu chochote.Baada ya kupima uzito jibu utalako pata liandike mahali.


2.Pima urefu wako

Wakati wa upimaji urefu akikisha umevua viatu vyako,simama wima na uangalie mbele.Baada ya kupima urefu jibu liandike mahali.

mfano jinsi ya kukokotoa BMI
kwa mfano ulipata uzito wa kilogram 75 (kg) na urefu wa mita 1.8 (m)

 BMI = 75Kg ÷ (1.8m × 1.8m)

BMI = 75Kg ÷ 3.24m^2

BMI = 23.15  (jibu kamili)


Uzito mzuri ni BMI 18 hadi 24.9.ikizidi uzito kupita kiasi unapaswa kupunguza,pia ikiwa chini ya 18 unakuwa chini ya uzito unaofaa(wastani) hivyo unapaswa kuweka juhudi kuongeza uzito unaotakiwa.BMI kati ya 25.0 na 29.9 huonyesha umezidi mipaka ya kawaida (uzito wako umezidi),ukiwa na BMI inayozidi mipaka upo katika hatari zaidi ya matatizo ya kiafya kama kisukari aina ya pili, maradhi ya moyo na satatani za aina mbalimbali.

BMI ambayo ni 30 na kuendela inaonyesha kuwa unauzito kupita kiasi au kiriba tumbo.Kuwa na uzito kupita kiasi kunakuweka katika hatari zaidi ya matatizo ya kiafya kama nilivyosema hapo mwanzo.Ukipunguza uzito wako utapata faida nyingi kama vile kuimarisha afya yako na kuondoa maumivu ya mgongo na viugo.Ili kupunguza uzito ni vyema ukapunguza vyakula vya wanga na mafuta, pia unashauriwa kufanya mazoezi ya mwili.
 BMI chini ya 18.5 (rangi nyeupe) una uzito ulio chini ya wastani.
 BMI kuanzia 18.5 mpaka 24.9 (rangi ya kijani) una afya ilioimalika.
 BMI kuanzia 25 mpaka 29.9 (rangi ya njano) una uzito ulizidi
 BMI kuanzia 30 na kuendelea (rangi nyekundu) una uzito uliopitiliza.

Kumbuka:kiwango cha mazoezi ya mwili huwa kinaendana na umri wa mtu husika, hivyo ni vyema ukatapa ushauri kutoka kwa wataalamu wa afya kabla hujaanza kuafanya mazoezi ya kupunguza uzito.

swali je unajua BMI ya mwili wako?? usisite kushare nasi hapa.
Kama umeipenda andiko hili basi gonga NZURI  na  kwa maswali au maoni zaidi basi tuandikie baada ya andiko hili, na pia kama ungependa kusoma andiko jengine kama hili basi jisajili kwa kuweka anuani yako  kwenye linki ya SUBSCRIBE.
Pia waweza tuandikia kwa email yetu Kuafit08@gmail.com 

Kwa number yetu ya Tigo +255 653 009 477  

Instagram account yetu  (KUAFITI), Facebook-(kuafit) na twitter-(kuafit)About Davis David

Davis David
Recommended Posts × +

DIET YA KUTOA SUMU MWILINI NA KUPUNGUZA UNENE KWA HARAKA

Habari zenu wadau wa KUAFIT! leo tutaongelea kuhusiana na elimu ya lishe ambayo itahusiana na diet ambapo tutaelezea mambo mengi san...