latest Post

FAHAMU VYAKULA 6 VINAVYOWEZA KUONGEZA UWEZO WA AKILI YAKO


Watu wengi duniani hutamani kuwa na uwezo mkubwa wakufanya  mambo makubwa kwa kuwa na uwezo wakufikiri zaidi ya binadamu wa kawaida. Madaktari na wataalamu mbali mbali duniani wamefanya tafiti nyingi kuhusiana na akili na uwezekano wa binadanu kuongeza uwezo wa kutumia ubongo wake zaidi ya 10% ambacho ndicho kiwango cha ubongo kinachotumika.  Kulingana na tafiti zilizofanywa kumegundulika yakwamba kuna vyakula vinavyweza kusaidia mtu kongeza uwezo wa akili yake.

 Vyakula hivi vinavyosaidia kuongeza uwezo wa akili viko vya aina nyingi, bali kati ya vyote tutaangalia vyakula 6 vinavyo shauriwa zaidi kutokana na kuonyesha matokeo ya haraka.vyakula hivyo ni kama vifwatavyo.



1.Mayai



  Mayai ni mojawapo kati ya vyakula vyenye virutubisho vingi na vyenye kuleta tija kubwa kwenye mwili wa mtu. Mayai yana  cholesterol ambayo ni muhimu sana kwa ubongo maana huchangia asilimia kubwa ya ubongo, na pia mayai yanakiwango kikubwa cha choline(neurotransmitter) ambacho husaidia kwenye mawasiliano kati ya ubongo na mfumo mkubwa wa mawasiliano wa mwili kupitia uti wa mgongo.


2.Mafuta ya Nazi



 Nazi ni aina moja wapo ya bidha ambayo hupatikana kirahisi katika jamii zetu na hutumika kwa kazi nyingi kama vile chakula, kutengeneza vinywaji, vipodozi na hata mafuta ya nywele.Mafuta ya nazi husifika kwa kuwa na asilimia kubwa wa kuweza kuongeza uwezo wa mishipa ya ufahamu kwenye ubongo kupitisha mawasiliano mengi kwa wakati.Hivyo inashauriwa sana kwa watu wanaotamani kuweza kuwaza kwa haraka na kupata ufumbuzi wa mambo watumie mafuta ya nazi.

3.Tunda aina ya Parachichi




Maparachichi ni matunda yaliyo barikiwa kwa kemikali(monounsaturated fatty acid)  ambayo ni muhimu kwenye mwili wa mtu hasa ubongo. Kutokana na kitabu cha "Federation of American Societies for Experimental Biology" inasemekana ya kwamba mafuta hayo husaidia hasa kulinda mishipa ya fahamu ya ubongo(astrocytes nerve cell), ambayo husaidia mishipa ambayo hupitisha mawasiliano.

4.Mboga aina ya Spinach



Spinach ni aina moja wapo kati mboga za majani zinazofahamika na hutumika kwa chakula. Mboga hizi za spinach ina chembechembe ya flavonoids ambayo husaidia kupunguza kasi ya ubongo kuchoka mapema kulingana na umri unavyozidi. Spinach pia ina potassium ambayo husaidia mzunguko wa damu kuwa mzuri hasa kwenye maeneo ya ubongo, na hivyo kusaidia mtu kuwa na uwezo mkubwa wa kuzingatia vitu vingi kwa wakati bila kupoteza kumbukumbu.

5.Mbegu za Maboga




 Mbegu za maboga ni kati ya mbegu tamu na huliwa na watu wengi kutoka jamii mbali mbali duniani. Mbegu za maboga zinasemekana kuwa ni kati chakula pekee ambacho husaidia ubongo kutokana na kuwa chembe za kemikali ya fatty acids ambazo zina (omega 3&6) . Mbegu hizi husaidia kumbukumbu,uwezo wakufikiri mkubwa na hata pia ukuaji wa ubongo kwa watoto.

6.Wine Nyekundu



Wine nyekundu ni matokeo ya uzindikaji wa matunda ya mizabibu ambayo imebarikiwa kwa kuwa na polyphenols kemikali ambayo hutumika kama kinga ya mmea huo. Polyphenol kwa mwili wa mwanadamu hufanya kazi nyingi na moja wapo ikiwa ni  kuongeza mzunguko mzuri kwenye ubongo na hivyo kuhimarisha uwezo wa ubongo kufikiri kwa wakati .

Kama umeipenda chapisho hili basi gonga NZURI  na  kwa maswali au maoni zaidi basi tuandikie baada ya andiko hili, na pia kama ungependa kusoma andiko jengine kama hili basi jisajili kwa kuweka anuani yako  kwenye linki ya SUBSCRIBE.

Pia waweza tuandikia kwa email yetu Kuafit08@gmail.com 
Kwa number yetu ya Tigo +255 653 009 477  
Instagram account yetu  (KUAFITI), Facebook-(kuafit)

About Kuafit

Kuafit
Recommended Posts × +

0 comments:

KUPUNGUZA UZITO KWA MAJI YA BARIDI

Watu wengi katika jamii hupendelea kuoga na maji ya moto katika majira yote ya hewa lakini kutokana na utafiti uliofanywa na wanasayansi kam...